Wafariki wakimgombania mwanamke

Wafariki wakimgombania mwanamke

Mtwara. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamtafuta Hadija Msamati kwa mahojiano akidaiwa kuhusika katika vifo vya wanaume wawili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Septemba 30, 2022, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema watu wawili wamefairiki dunia kwenye ugomvi wa kupigana wao kwa wao wakigombea mwanamke wilayani Masasi.

Amesema watu hao walitambulika kwa majina ya Ibrahimu Shaban (21) na Mussa Bakari (28) ambao wamefariki dunia baada ya kupigana kwa kutumia magongo ya miti na kupigana wao kwa wao wakigombea mpenzi.

Katembo alisema kuwa Septemba 29, 2022 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga wilayani Masasi watu hao waligombana.

"Hili tukio limesababishwa na wivu wa mapenzi ambapo imebainika baada ya ugomvi huo mwanamke huyo amekimbilia kusiko julikana ambapo kwa taarifa ya Daktari baada ya uchunguzi walibaini chanzo ni kuvuja damu kwa wingi mwilini," alisema Katembo
Cc: Mwananchi newspaper
Polisi bana
Kwa hiyo Hadija alikuwa mwamuzi wa mpambano?
 
Ngojeni na nyie polisi muamze kupigana na kuuana.
 
Mwanamke ashitakiwe kwa kupunguza nguvu kazi ya taifa ni kosa la uhujumu uchumi hilo.
 
Sasa kama wamepigana na kuuana wenyewe dada wa watu wanamtafutia nini!!!
 
Sasa huyo bint anatafutwa na polisi kwa kosa gani?

Polisi buana wanashangaza sana ,watu wamepigana kwa magongo wameuana kwa kumgombania khadija then polisi wanamtafuta binti khadija sijui wanataka wamuone anafananaje labda.

Kama kuchukua maelezo kwa khadija sio kusema kwamba wanamtafuta as if kama yeye ndio aliyewaua.
 
Nimewahi kushuhudia knock out katika ngumi kwa maboxer wote wawili, lakini hii ni kali zaidi.

Yaani mtu kapigwa gongo la kichwa akaanguka, halafu akainuka na yeye katoa kipigo cha gongo la kichwa, wote wakaanguka na kufa!
Inasikitisha sana najiuliza tu hiyo mibanzi walivyokuwawanashushiana mpaka wakafa pamoja dah jamaa wavumilivu sana huku mbunye Iko pembeni inaangalia.
 
Bi khadija sasa ...
Screenshot_20220810-122745_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom