Wafuasi wa dini ya Roman Catholic naomba kujibiwa hili swali tafadhali

Wafuasi wa dini ya Roman Catholic naomba kujibiwa hili swali tafadhali

Ni uwongo mkubwa kudai kuwa Papa ana ulinzi mkali.
Walinzi wa papa siyo walinzi wa kivita, ni more ceremonial. Wale walinzi wanatoka Switzerland, nchi ambayo haina jeshi. Nchi ya Switzerland inajitolea kutoa ulinzi kwaajili ya Vatican.

Kama mnakumbuka mwaka ule Papa John Paulo alipopigwa risasi na Mehmet Ali Agca, raia wa Uturuki, walinzi wake walivyoulizwa mazingira ya kupigwa kwake risasi, kiongozi wa walinzi wale alisema kuwa kazi yao ya ulinzi ni ngumu sana kwa sababu wanamlinda mtu asiyependwa kulindwa. Wamemshauri mara nyingi kutoingiliana karibu sana na watu, lakini wameshindwa. Na kila mara Papa alikuwa akiwaambia kuwa chochote kifakachomtokea wakati anapotimiza wajibu wake, kimeandikwa katika akaunti yame ya maisha.

Papa alifanyiwa operation kwa masaa 10, mara tu alipopata fahamu, maneno yame ya mwanzo kabisa yalikuwa, 'kwanza namsamehe yule aliyetaka kuniua; pili nawapa pole walioheruhiwa pamoja nami; na tatu, nayaunganisha mateso yangu na ya Bwana wetu Yesu Kristo). Papa akiwa amedai kuwa Mehmet asamehewe aachiwe huru, serikali ya Italy iligoma, na kumfunga. Baada ya miezi kadhaa, papa alienda kumtembelea Mehmet gerezani, akaongea naye, na akaendelea kusisitiza na kuomba kuwa aachiwe huru. Baadaye Italy iliridhia ombi la Papa.

Kwa leo ulinzi ulikuwa mkali siyo kwa sababu ya papa, bali ni kutokana na viongozi wakuu wa nchi na wageni mbalimbali waliokuwepo kwenye maziko ya papa.

Kumbuka kuwa kuna baadhi ya watu, hasa yale makundi ya kigaidi ya kiislam, kwao kila mkristo ni adui. Hivyo kwenye matukio kama haya ya aweza kutake advantage.
Acha kutupiga kamba

Papa ana ulinzi mkali wa kipekee
Ni kweli kwamba baadhi ya walinzi wa Papa, hasa Swiss Guard, wanaonekana kama wa "ceremonial" kwa vile huvaa mavazi ya kale (mavazi ya karne ya 16), lakini hawako tu kwa mapambo.

Swiss Guard ni maafisa waliopitia mafunzo makali ya kijeshi.

Wanatoka Switzerland, lakini wanatoka kwenye jeshi rasmi la Uswisi (kabla ya kujiunga na Vatican).

Ili kuwa Swiss Guard, kijana lazima awe:

Raia wa Uswisi,

Amepitia mafunzo ya kijeshi Uswisi,

Awe Mkristo Mkatoliki mwaminifu,

Awe na afya na nidhamu kali.


Kwa hiyo, si kweli kwamba wanatoka Uswisi bila mafunzo ya kijeshi.

Switzerland haina jeshi?
Hili pia ni si sahihi

Switzerland ina jeshi lake la kujihami (Swiss Armed Forces), lakini linaendeshwa kwa mfumo wa wajibu wa kijeshi wa kiraia (militia system).

Wanafunzi wengi wa kijeshi Uswisi hupitia mafunzo na kuhitimu kama askari kabla ya kurudi kwenye maisha ya kiraia.

Walinzi wa Vatican (Swiss Guard) ni wale waliopitia mfumo huu wa kijeshi, kwa hiyo wana mafunzo kamili ya kijeshi.

Papa ana aina nyingine za ulinzi zaidi ya Swiss Guard

Mbali na Swiss Guard, Papa analindwa pia na:

Gendarmerie Corps of Vatican City State hii ni jeshi la polisi lenye silaha kamili la Vatican.

Wakati anaposafiri, anaungwa mkono na vikosi vya usalama vya nchi anayokwenda, kwa mfano FBI na Secret Service walimlinda Papa alipofanya ziara Marekani.

Kwa hivyo ulinzi wa Papa ni mchanganyiko wa walinzi wa heshima (ceremonial) na vikosi vya kisasa vilivyojihami vizuri.
 
Mbona Rwanda inaukubwa wa wilaya ya kalambo RUKWA ila ni nchi ina rais wake jeshi kwa nini usiite wilaya au mkoa?
Mfano wako hau-make sense Rwanda yenye mamilioni ya heka huiwezi kuitolea mfano wa Vatican yenye ukubwa wa heka 44 sawa na viwanja 60 tu vya mpira wa miguu? Ukubwa wa Vatican inalingana na Shamba la kikwete kule Msoga ila shamba la kikwete ni kubwa zaidi
 
Swali langu ni kuwa "kwa nini Papa huwa ana ulinzi mkali sana"?

Papa pia ni kiongozi wa mamlaka ya Vatican ambayo hutambulika kama nchi...

"Pope is the head of the Holy See, a sovereign juridical entity under international law, and the head of the Catholic Church."
 
Kwa hiyo vigezo ni vipi kama umekataa yeye kuongoza nchi yenye ukubwa huko? Kama Kuna nyaraka yenye kusema nchi inatakiwa kuwa na ukubwa kiasi Fulani ,iweke mezani ijadiliwe kwa hoja
Ndo maana wenye akili wakaiita Vatican City , Papa na Rais wa Manzese Madee ni ma Rais wa nchi zinazolingana ukubwa
 
Nadhani hamja elewa dhumuni langu. Inshu ya kuwa na ulinzi sio ajabu, ajabu ni kwa nini ana ulinzi mkali sana. Huwezi linganisha ulinzi wa Papa na hao ulio wataja, kwa nini Papa awe na ulinzi mkali kiasi hicho, yeye ni nani hasa hapa duniani ukiachana na upapa wake?
Kama kiboko ya wachawi tu alikuwa na walinzi gwajima ana walinzi Geodavie ana walinzi then papa akoswe ulinzi seriously?
 
Kama ni hivyo basi jamaa ndio kiongozi mkuu wa dunia
Ni top ya viongozi wote duniani that's why.

Kiongozi yeyote duniani lazima ufuate maelekezo kutoka Vaticani. Pope ni kiongozi wa kidini & kisiasa
 
Yaani hiyo ni lazima mzee, huwezi kutoka nchi yoyote eti ukawe mlinzi wa Vatican. Lazima utokee Uswisi na mdhamini wako lazima awe padri.
Kwa hiyo lazima watoke nchi ya uswis?
 
Mwamposa mwenyewe anatembea na mabouncer 😀 unataka akatize kariakoo wahuni wamvamie au mitaani wasioamini katika misimamo yake wamdhuru na kusababisha gharama kubwa na majonzi kwa watu bilioni 1.6? Mungu mwenyewe anataka ujilinde kisha yeye akulinde
 
We watu wanachonga sanamu kwa mikono yao alafu wanalipigia magoti kuliomba baraka, toba na ulinzi, unafikiri Papa ni mjinga ategemee ulinzi wa sanamu , hapo lazima awatafute Suma Jkt guard wa Vatcan
Unapata faida gani zaidi ya kujitafutia laana kwa kunena maneno ya uongo?
 
Hilo sikatai, mimi napata mashaka kuhusu ule ulinzi mkali anapewa Papa. Papa ni nani hasa kwenye hii dunia huenda nje ya box ni mtu mkubwa sana ndio nataka nijue ni nani hasa ukiachana na u Papa wake?
Mrithi halali wa kiti cha Petro
Kiongozi na mchungaji wa wafuasi zaidi ya bilioni 1 duniani kote
Mkuu wa nchi ya vatican
Kwa hayo machache tu anastahili ulinzi zaidi ya marais wote duniani
 
Back
Top Bottom