Hapo kwenye kuhonga wapinzani, hapo mwenye tatizo ni aliehongwa ama aliehonga?
Matatizo ya wapinzani wetu kua wenye njaa na wasio na msimamo ni kosa la Magufuli?
Kugombana na majirani ni kitu cha kawaida pale unapoona maslahi ya nchi yanaingiliwa. Kazi ya rais ni kulinda maslahi ya nchi, rais akiona majirani wanaingilia maslahi yetu lazima akomae, hata Putin ndio maana ameivamia Ukraine kulinda maslahi ya nchi yake, Kikwete aligombana na Kagame kulinda masilahi ya nchi yetu.
Hoja kwamba Magufuli aligombana na majirani haina msingi wowote, hata Nyerere aligombana na Iddy Amin kulinda maslahi ya Tanzania. Ama ulitaka Magufuli awachekee wakenya wanavyoiba nchini kwetu?
Sekta binafsi ipi iliyokufa? Sekta binafsi ingekua imekufa banks zisingekua zinaogelea kwenye faida, ama husomi hata machapisho ya mapato ya mabenki nchini? Banks zisingekua zinafungua matawi kila kona. Hakuna sekta binafsi iliyokufa, huo ni uongo na uzushi.
Mapato ya Kodi yasingefik 2T kama sekta binafsi ingekua imekufa. Hoja ya sekta binafsi kufa haina mashiko.
Vyombo gani vya habari vilifungiwa? Hivi bijigazeti uchwara vinavyopika habari kina Tanzania Daima, Machweo sijui mawio? Hebu kua serious basi. Hakuna taifa linaweza kua na vyombo vya habari ambavyo kazi yake ni kutunga stori na kuzusha uongo na uzandiki kwenye jamii, hakuna Duniani.