Wafuatao wasipokunjua nafsi Rais atakwama au itamlazimu awaweke pembeni Taifa lipone

Wafuatao wasipokunjua nafsi Rais atakwama au itamlazimu awaweke pembeni Taifa lipone

Usijili
Acha kujilinganisha na prof kabudi wewe kilaza mkubwa kabisa elimu ya kuungaunga. Unadhani kabudi hata akiacha hiyo siasa atalala njaaa? vilaza mnashida sana
Kuna kitu nilitaka kuandika, nimeamua kuacha. Baki na upumbavu wako.
 
''Mama fanya mabadiliko ya mfumo mzima, ruhusu katiba inayokubalika kisha 2025 ng'atuka tuachie Taifa lenye nidhamu na historia itakukumbuka wewe na familia yako. Hakuna kiongozi wa kitaifa amemwahi kukumbukwa kwakusimamia maslahi ya chama chake Bali anakumbukwa kwa kusimamia maslahi ya Taifa''............................................................. Kauli hii ya kutaka mtu kung'atuka imeharibu hoja zako zote na kuonekana kuwa lengo lako ni kutaka Mama atoke madarakani,kama atafanya yale ambayo watu wanayahitaji haitaji heshima ya kung'atuka,kung'atuka kunatokana na mtu kufanya mambo nje ya muda wake lakini alie ndani ya muda wake na anafanya kulingana na wajibu wake na kutimiza matakwa ya watu, anafaa kuendelea kudumu hadi mwisho kulingana na sheria inavyotaka, kung'atuka bila sababu ya msingi ni kujitengeneza mazingira ya kujionyesha kuwa haufai na umepisha wengine wakusaidie.
Naunga mkono kuboresha mifumo yetu, napinga Mama kung'atuka kabla ya kusimamia maboresho hayo Hadi yatakapokuwa yamesimama Barabara.
 
Biteko mama amesema kitalu c mirerani ni reserved lakini sasa hivi kinagaiwa kinyemela na watu wanachimba, madini yanatoroshwa sana kama kipindi cha nyuma na huyo dogo muda mwingi yupo arusha.. alimwambia cdf adhibiti utoroshaji huu wa tanzanite (think as a great thinker)
Du hapa sasa inabidi naye asaidiwe kam vipi
 
Mleta uzi umewataja watu hatari kwa utawala wa mama kwa usahihi kabisa, japo umemsahau na Mwigulu. Huyo mama kama anataka kufanya kazi bila kuhujumiwa, awaweke mbali hao, vinginevyo watamkwamisha.
Naweka NUKTA
 
Mleta uzi umewataja watu hatari kwa utawala wa mama kwa usahihi kabisa, japo umemsahau na Mwigulu. Huyo mama kama anataka kufanya kazi bila kuhujumiwa, awaweke mbali hao, vinginevyo watamkwamisha.
Naweka NUKTA
 
Timu ya jiwe ilipaswa ing'oke yote
 
Katiba hii mnayoilalamikia ndiyo imemuingiza Samia madarakani tena bila kupigiwa kura na akaapa kuilinda!
Guys, CCM ipo madarakani , kikubwa ni opposition kujipanga, kutegemea CCM ilete mabadiriko ni ujuha
 
Hio yote ulioitaja ni "MISUKULE YA MAREHEMU", ila kuna misukule ipo ambayo haujaigusia kabisa, ya Mikoa na Wilaya. Licha ya Rais kuwakosoa baadhi yao kweli kweli hadharani ila hayapati akili na kuandika barua za kujiuzulu.

1) Kamanda Mambosasa - Kinondoni.
2) Ally Hapi - Mkuu Wa Mkoa Iringa.
3) Ole Sabaaya - Mkuu Wa Wilaya Hai.
4) Kenani Kihongosi - Mkuu Wa Wilaya Arusha (Aliewachapa Wafanyabiashara viboko).
5) Heri James UVCCM TAIFA (Zamani kipindi akisoma alikua anaitwa Eric Ngambeki).
6) Alfred James - Kaimu Mkurugenzi Wa Bodi Ya Korosho.
7) Doto Biteko - Waziri Wa Madini.
Mkuu huyo namba 4 namtetea. Kenan Kihongosi aliwachapa wale watu baada ya kukutwa na "kizibiti" Cha wizi. Walikuwa na madawati tena wakiwa wameshayaharibu.

Wanafunzi wanaoiba madawati walibanwa na wakaonyesha ni wapi wanapeleka madawati wakishayaiba. Na walikiri hua wanatumwa na wale mafundi. Wale sio wafanyabiashara , bali ni mafundi (staff) wa hizo sehemu zilizokutwa na hayo madawati. Fikiria Taifa linapambana watoto wetu wasome wakiwa wamekaa kwenye madawati, halafu watu wazima wanawashawishi watoto waibe madawati kwa ujira mdogo Sana. Kwanza wanawafundisha watoto wetu tabia mbaya ya wizi. Kitendo hicho kinatia hasira Sana.

Sifa ya yule Kenan ni kufatilia na kulinda miradi ya serkali. Nachoona hapo ni hiyo kuwachapa ilikotafsiriwa ni kuchkua Sheria mkononi. Lakini Nina imani kabisa amejifunza, maana yule hata ukimkuta na wananchi sio mtu wa kupandisha mabega.

Kwa muda mfupi aliokaa Arusha amejitahid Sana, kafanya Mengi makubwa simply because ni mbunifu. Arusha ni ngumu laanaa.
Naongea haya nikiwa na uzoefu na Arusha, siasa zake na lifestyle yake.

KWA maoni yangu huyu aachwe Ili amalizie aliyoyaanzisha, atamsaidia mama Sana.

Combination ya Idd kimanta na Kenan Kihongosi hapa Arusha imekaa sawa kabisa.
 
1. Mama aendelee kuondoa genge la ukabila.

2. Mama aachane na project za marehemu kutumia fedha za ndani.

3. Ile midege ya Jiwe aikodishe tu, kama tunaendlea kula hasara haina haja ya kupata faida, biashara ni kutengeneza fedha ili kuinua pato.

4. Mama aongee vizuri na upinzani, watu kama akina Lissu, Lema na Msigwa ni assets za Taifa.

5. Wekeza sekta ya kilimo, watanzania wakila vizuri tu tunaridhika. Wala hutosikia kelele mitandaoni wala mitaani, hii kete ndio aliyoiweza Hayati Mkapa, watu walikula na wakashiba, wakaridhika.

6. Wanafki kama akina Gwajima aka Rashid waogope sana, kama mtu ameweka kaz ya Mungu kuwa namba mbili kisha kaz ya mwanadamu namba moja elewa kuwa hata wewe ipo siku atakumaliza.

7. Fanya unavyoweza kufungulia ajira.

8. TRA isuke upya.

9. Nna mengi sana ila mazingira yamenibana
Kitu pekee ambacho kimeniuma mno ndani ya hii nchi ni kumuona maguful kazikwa kiheshima vile, kwa uchafu ulioachwa na maguful hata kaburi lake kubaki kuwa historia ndani ya taifa ni aibu.
Hao wote hawamuwezi kwa kuwa rais katiba inampa nguvu kubwa sana ya kushughulika na wakorofi na kuwa silence fasta.
 
Miruzi mingi humpoteza mmbwa.awaache wafanye kazi hata miezi mitano kwanza huku akifuatilia mienendo yao baada ya yeye kuingua madarakani.labda kama mtu amestaafu kwa mkataba au umri.

Awaite wabadilishane nao mawazo halafu awaache ,MWENDAZAKE huku mwishoni alijua watz ndivyo tulivyo alituachsa na akawa anasubiria muda wKe mtu uishe.
Mwendazake alishawahi sema nitabadilisha mara ngapi?kauli hii ilimaanisha makosa ya watendaji ni mengi anayajua ila anawaacha.
 
Usijili
Acha kujilinganisha na prof kabudi wewe kilaza mkubwa kabisa elimu ya kuungaunga. Unadhani kabudi hata akiacha hiyo siasa atalala njaaa? vilaza mnashida sana
Bora umemjibu. Mimi nahisi humu JF tuna watoto wadogo ama ni watu wazima wasiojua kufikiri. Mimi inapofika suala la Tanzania Chama Baadaye. Akina Kabudi wamesaidia sana tuwe na 16% Barick na pia kupata USD million 300. Na pia Kupata hisa Airtel ambako tulikuwa tumepigwa changa la Macho. Ana changamoto zake lakini si kwa kiasi hicho. Hashimu umemjibu vyema
 
.

Mama fanya mabadiliko ya mfumo mzima, ruhusu katiba inayokubalika kisha 2025 ng'atuka tuachie Taifa lenye nidhamu na historia itakukumbuka wewe na familia yako. Hakuna kiongozi wa kitaifa amemwahi kukumbukwa kwakusimamia maslahi ya chama chake Bali anakumbukwa kwa kusimamia maslahi ya Taifa.
naunga mkono hoja
p
 
Hio yote ulioitaja ni "MISUKULE YA MAREHEMU", ila kuna misukule ipo ambayo haujaigusia kabisa, ya Mikoa na Wilaya. Licha ya Rais kuwakosoa baadhi yao kweli kweli hadharani ila hayapati akili na kuandika barua za kujiuzulu.

1) Kamanda Mambosasa - Dar Es Salaam.
2) Ally Hapi - Mkuu Wa Mkoa Iringa.
3) Ole Sabaaya - Mkuu Wa Wilaya Hai.
4) Kenani Kihongosi - Mkuu Wa Wilaya Arusha (Aliewachapa Wafanyabiashara viboko).
5) Heri James UVCCM TAIFA (Zamani kipindi akisoma alikua anaitwa Eric Ngambeki).
6) Alfred James - Kaimu Mkurugenzi Wa Bodi Ya Korosho.
7) Doto Biteko - Waziri Wa Madini.
Doto James ....ana kashfa nyingi mno plus mikono yenye damu
 
Back
Top Bottom