Mkuu 'Tindo', naona una maswali mengi ya udadisi tu huku ukweli ukiujua mwenyewe.
Huko "...kushikamana na vyombo vya dola" kusikutishe hata kidogo.
Leo hii CCM ikifurumishwa utaona vyombo hivyo hivyo ndio vitakuwa mbele kuinanga CCM.
CHADEMA ingeendeleza ilipokuwa imefikia na Magufuli (sina maana ya siasa za uanaharakati); ungeona jinsi nchi hii ilivyobadilika. CHADEMA wanakosea sasa hivi kuwapa CCM nafasi ya kujipanga upya. Kinana akiwa kinara wa kazi hiyo.
EeeenHeee,Iliendeleza ila Mbowe mkatishia kumfunga kwa kesi ya ugaidi, Mimi nadhani Rais akiwa diplomat hakuna haja ya kutunishiana misuli ila kwa type ya JPM kweli Mtu wa siasa za Lissu was a better fit yaani jino kwa jino.
Having said that, CHADEMA na Samia wamechagua meza kama suluhu. Kuanza kuinanga serikali wakati meza ipo wazi ni siasa za kizamani ngoja wamalizane na mambo ya tume huru na katiba utaona moto unavyowaka tena.
Hata kule Kenya unaona Odinga Yuko kimya kwa madhaifu ya Kenyatta maana ndio anamsafishia njia ya Ikulu, ila akiingia wote mtashangaa atakvyowasha moto kwa mafisadi akiwemo Kenyatta mwenyewe!!
Siasa ni kama karata Kila move inahesabiwa, hivyo ukikosea timing tu hii chance ya tume huru haitarudi milele
Hapana. Wazunguke naye, mlango kwa mlango. Hiyo ndiyo kazi muhimu kwa CHADEMA wakati huu, na siyo kutafuta kumwaga damu za waTanzania.CDM wafanyeje labda, au wamzuie Kinana kuzunguka nchi nzima?
"Nia njema" umeipima kwa kipimo gani ukajua ipo?Maadam Nia njema ipo basi tuwe na subira kunaweza patikana suluhu kwenye mchakato huu mpya wa katiba
1. Fidia kwa Lissu na Mbowe."Nia njema" umeipima kwa kipimo gani ukajua ipo?
Mbona wanazunguka, last week walikua Mbagala kusajili kidijitali na kugawa kadi za kielektroniki.Hapana. Wazunguke naye, mlango kwa mlango. Hiyo ndiyo kazi muhimu kwa CHADEMA wakati huu, na siyo kutafuta kumwaga damu za waTanzania.
Nadhani tumeelewana, mkuu wangu 'Tindo'.
Hamna lugha ilibadilika ila Hilo Mnyika alisema wazi kabisa, hata issue ya Mdee alisema maamuzi yatatokana na "negotiations" kwa Mama na sio procedure za kimahakama!!EeeenHeee,
Mkuu 'zitto junior', kwanza kabla ya yote, naona jinsi lugha inavyobadilika, bila shaka kuna mambo huko yanapikwa kama tulivyohisi wengi wetu.
Haya uliyoandika hapa, ngoja niyape tafakuri, kwa maana naona makisio yetu juu ya CHADEMA na Samia yalikuwa sahihi.
Nitatafuta muda mzuri knirudi kwenye bandiko hili kwa utulivu wa akili.
Lakini tafadhari, naomba tusikoseane heshima mara hii ,kwa kutumia maneno kama haya ""iliendeleza ila Mbowe 'mkatishia'kumfunga kwa kesi ya ugaidi"
Sikumbuki ni lini hasa nilijihusisha katika jambo la namna hii!
Hapana. Wazunguke naye, mlango kwa mlango. Hiyo ndiyo kazi muhimu kwa CHADEMA wakati huu, na siyo kutafuta kumwaga damu za waTanzania.
Nadhani tumeelewana, mkuu wangu 'Tindo'.
Hivi hili la "kushambulia" linatoka wapi?Na alichosema ni wanachama tuwe "watulivu" huku meza ikitumika. So usitegemee Lissu au Mbowe kuanza kufanya mikutano ya kuishambulia CCM na Samia huku unataka wabunge hao hao wa CCM waipitishe sheria bungeni!!
Haya sasa.CCM wana ruzuku, na hata raslimali za serikali zinatumika kufanikisha ziara za viongozi wa CCM. Je CDM wanatoa wapi hela ya kuweza kumfuatilia Kinana kila apitapo? Vyama vikongwe vilivyo madarakani muda mrefu hasa vyenye vimelea vya kijamaa, havitoki madarakani kwa box la kura. Na ushahidi wa hilo uko wazi peupe.
Fair enough.1. Fidia kwa Lissu na Mbowe.
2. Kuachiwa wafungwa wa kisiasa
3. Kuunda tume ya kuchukua maoni juu ya reforms za kisiasa.
Hayo yote yanaonyesha kuna Nia njema ya negotiations hizi kuzaa matunda.