Wafungwa wa kisiasa kutoka jimbo la Ukerewe washinda rufaa yao na kuachiwa huru

Yaani na huko wanadai wamejaa wabobevu wa sheria. Ilani watu WAOGA HATARI.

Msomi anayetumikia Serekali zinazoingia madarakani kwa kunajisi chaguzi, hana tofauti na mtu ambaye hajasoma. Huko elimu yake hugeuzwa kutekeleza matakwa ya watawala na sio kinyume na hapo.
 
TOKA MAKTABA :

7 May 2021
Dodoma, Tanzania

Serikali imekanusha kuwa na wafungwa wa kisasa na kwamba Rais Samia Suluhu hajaamuru wafungwa wowote watolewe magerezani kama ilivyotangazwa na kituo cha televisheni cha Citizen cha Kenya. Msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesisitiza kuwa Tanzania haina wafungwa wa kisiasa na wala hakuna wafungwa wa kisiasa Tanzania bali zipo kesi za makosa ya kijinai yanayoendelea kusikilizwa mahakamani ili haki ipatikane .

Tanzania yakanusha, yasema hakuna wafungwa wa kisiasa

Source : Zanzibar Kamili TV
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Hali ilikuwa ngumu sana ngazi zote wapinzani walizogombea kuanzia udiwani, ubunge na uRais hali ilikuwa mbaya.

Nchi ilikuwa na watu wenye uvumilivu mkubwa sana 2020.

Sio uvumilivu mkuu, ni uoga. Na watawala wameshajua kuwa wananchi ni waoga, hivyo wanafanya lolote watakalo. Bila uoga kututoka wananchi mambo mabaya zaidi yataendelea kutokea.
 
JamiiForums753274111.jpg
 
Sio uvumilivu mkuu, ni uoga. Na watawala wameshajua kuwa wananchi ni waoga, hivyo wanafanya lolote watakalo

Nakubaliana nawe asilimia 110, masuala muhimu kama haki katika mfumo haki jinai, hali ngumu ya kiuchumi ya kila raia, katiba mpya au iliyoboreshwa, demokrasia, haki ya elimu bora na huduma za afya haya ni mambo msingi kwa binadamu lakini waTanzania wanasita kujiunga na wana harakati au vyama vya upinzani wapate hicho kitu muhimu.

Mfano mwingine mpya Ongezeko la Mishahara kiduchu waTanzania wanaishutumu CHADEMA kwa kuonekana ipo kimya lakini wakiambiwa wasimamie kidete kura zao wapate wakilishi wao halali wanaowataka ngazi ya udiwani, ubunge n.k wanaruka kimanga na kudai wahataki kujibainisha na wanasiasa waroho wa madaraka waliopo upinzani.

Yaani waTanzania magumu yakiwafika kama nyongeza ndogo za mshahara, huduma mbovu za afya, matumizi ya anasa na ufahari ya viongozi wateuliwa wa CCM ndiyo huanza kuikumbuka CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI n.k
 
Kabisa mkuu, wananchi hawajui kwa viongozi wa kiafrika huwa hawaogopi sheria, wala sijui katiba, bali huogopa nguvu ya umma tu. Iwapo wananchi wataendelea na huu ukondoo, tutegemee uhuni zaidi ya huu.
 
Katiba ya kukaa mezani na CCM bila kutokea machafuko, usitegemee kuheshimiwa.

Katiba bora hupatikana baada ya machafuko, au nchi kupinduliwa.

Hilo ni angalizo nakupa ndugu yangu.
Hapana.

Siyo lazima ya kuwepo machafuko ili kupata Katiba iliyo bora.

Suluhisho ni kukataa CCM kuendesha shughuli za hiyo katiba mpya, basi!

Labda useme machafuko kutokea wakati CCM waking'ang'ania kuendesha shughuli hiyo. Hapo machafuko watakuwa wameyaleta CCM wenyewe.
 
CCM wang'ang'anie kuendesha shughuli hiyo mara ngapi?
 
Sijui unataka niseme mara ngapi kabla ya machafuko kuwepo.

Ninachosema hapa, ni leo na kesho, sitazami ya huko nyuma.
 
Kipi kimebadilika sasa?
Mengi sana yamebadilika.
CCM ipo kwenye hali ya umahututi.

CCM yenyewe imepitia katika hali ngumu sana, na bado haijui itatoka vipi.

Kosa litakalofanyika ni kuiruhusu tena ijiimarishe.
 
Yaani waTanzania magumu yakiwafika kama nyongeza ndogo za mshahara, huduma mbovu za afya, matumizi ya anasa na ufahari ya viongozi wateuliwa wa CCM ndiyo huanza kuikumbuka CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI n.k
Hapa umegusa jambo muhimu sana ambalo linahitaji uchambuzi makini sana ili kufahamu sababu zinazopelekea iwe hivyo.
Jibu rahisi ni kualumu wananchi. Hata mimi hulaumu hawa waTanzania kwa nini hawastuki hata mambo yanayorudisha juhudi zao nyuma yanapotokea.

Bila shaka zipo sababu. Kushindwa kwetu kuzielewa hakuwezi kamwe kuhalalisha lawama kwao.

Bila shaka ipo nafasi pia ya kujiangalia sisi tunaolaumu. Je, tumefanya juhudi za kutosha kuondoa mashaka yao juu yetu?
 
28 July 2022
Ukerewe, Mwanza

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA KTK KESI No. 171 OF 2021, YAWAACHIA HURU WANACHAMA WA CHADEMA

Waliokuwa wagombea udiwani kupitia chama cha CHADEMA washinda rufaa yao na kuachiwa huru. Mzizi wa Hii kesi ilitokea wakati wa kurudisha fomu za udiwani, walipigwa risasi mwilini na walibabikiwa kesi.

Makamanda hao ni Mateso Mgeta na Alfred Mabagala ambao mbali ya kushinda kesi hiyo walikuwa tayari wametumikia miaka 2 katika ya mitano kabla ya kushinda rufaa yao.

Makamanda hao wa CHADEMA sasa wataenda kukaguliwa afya zao kwani walipata majeraha na vipigo vilivyopelekea kutembelea magongo na walipokuwa jela, mazingira yale yalikuwa magumu kuweza kupata huduma kamilifu za kutibu majeraha yao.

CHADEMA kanda ya Victoria na taifa inaomba wana CHADEMA na waTanzania kwa ujumla kuwaangalia hawa makamanda ili waweze kupata huduma za kiafya baada ya kutoka gerezani na sasa wapo huru.

Jaji wa mahakama kuu kanda ya Mwanza katika uamuzi wake ulio andikwa katika jumla ya kurasa 17 Alfred Mabagala @ Mugeta & Another vs Republic (Criminal Appeal 171 of 2021) [2022] TZHC 10789 (25 July 2022); | Tanzlii na kusomwa mbele ya Mahakama Kuu, alikubaliana na hoja za upande wa utetezi kupiga hukumu ya mahakama ya wilaya ya Ukerewe.

Source : CHADEMA Media TV

Ila magufuli hapana aisee he was tyrant
 
Mwanakondoo ameshinda
 
Hapa umegusa jambo muhimu sana ambalo linahitaji uchambuzi makini sana ili kufahamu sababu zinazopelekea iwe hivyo.
Jibu rahisi ni kualumu wananchi. Hata mimi hulaumu hawa waTanzania kwa nini hawastuki hata mambo yanayorudisha juhudi zao nyuma yanapotokea.

Bila shaka zipo sababu. Kushindwa kwetu kuzielewa hakuwezi kamwe kuhalalisha lawama kwao.

Bila shaka ipo nafasi pia ya kujiangalia sisi tunaolaumu. Je, tumefanya juhudi za kutosha kuondoa mashaka yao juu yetu?
Mkuu kushindana na mtu aliyeshikilia bunduki huku ameshaikoki wakati wewe una mikono mitupu ni sawa na kumvimbia Simba dume mwenye hasira kali
 
Makamanda si wana mafunzo ya uvumilivu,wavunjwapo wavumilie tu.
Povu ruksa!
 
TOKA MAKTABA :

7 May 2021
Dodoma, Tanzania

Serikali imekanusha kuwa na wafungwa wa kisasa na kwamba Rais Samia Suluhu hajaamuru wafungwa wowote watolewe magerezani kama ilivyotangazwa na kituo cha televisheni cha Citizen cha Kenya. Msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesisitiza kuwa Tanzania haina wafungwa wa kisiasa na wala hakuna wafungwa wa kisiasa Tanzania bali zipo kesi za makosa ya kijinai yanayoendelea kusikilizwa mahakamani ili haki ipatikane .

Tanzania yakanusha, yasema hakuna wafungwa wa kisiasa

Source : Zanzibar Kamili TV

Tanzania hii hii ilisema Mbowe gaidi halafu wakamtoa wenyewe, hivi tokea lini serikali ya ccm ikakubali makosa yake.
 
Sio uvumilivu mkuu, ni uoga. Na watawala wameshajua kuwa wananchi ni waoga, hivyo wanafanya lolote watakalo. Bila uoga kututoka wananchi mambo mabaya zaidi yataendelea kutokea.
Huo uogo umetengenezwa moja ya strategy ni kufunga watu wanyee debe miaka nenda rudi bila losa lolote, extrem ilifika wakaanza kuteka, kuua na kutesa.
 
Back
Top Bottom