Waganga wa jadi 10 wapelekwa Kigoma kupambana na Wachawi, DC aweka ngumu

Waganga wa jadi 10 wapelekwa Kigoma kupambana na Wachawi, DC aweka ngumu

Yapo majambazi mengi huku Kigoma yame survive risasi sababu ya hizo chale. Ushirikina unatumika ndugu hata kikosi kilichokua kinawasaka kilikua kimeiva kwenye "dark arts".

Njoo huku Kigoma upate shuhuda za live live sio za kusimuliwa. Mimi napinga ushirikiana ila nakubali uchawi upo, in fact ukiwa mtu wa maombi huku huwezi kulala maana wanakuja "kukupima" usiku usiku.
Hakuna kitu kama hicho. Upigwe zile wanaita 50mm ya kichwa ubongo utawanyike harafu upone sababu ya chale!? Hizi ni habari za waganga matapeli wanaotafuta pesa ya kula.
 
Huu ujinga huwa mnasomea wapi? Watu kama nyie ndo walikua wahanga wa maji maji war
Karibu kigoma ndugu maana nina uhakika tokea umezaliwa hujawahi sikia mlio wa SMG. Huku zilikua zikiwaka huko Burundi tunazisikia mpaka huku mind you majambazi yalikua mengi sana huku kipande cha Biharu, Kibondo, Kakonko n.k.

So we know better
 
twende kigoma this week nauli na malazi juu yako then kuna mtu namjua akupe hyo dawa endapo itakuwa uongo nakurudishia gharama zako zote za usafiri na malazi.

baada ya kufanyiwa utajaribiwa kwa kila silaha unayotaka wewe kuanzia wembe,pange,visu,shoka,risasi nk

dawa hiyo inaitwa kidono tembea ndugu dunia ina mengi mno usiyoyajua
Huu ni utapeli wa kizamani sana. Bahati mbaya kuna wajinga wanauamini hadi leo.
 
ULaya na Marekani uchawi umepungua sana baada ya wachawi wengi kuuliwa.

Huku Afrika ni watu viazi kama wewe ndio mnasababisha hawa wachawi waendelee kutusumbua kwa kuwatetea kuwa uchawi hakuna.

Pia Kama mtu anaeamini uchawi ni mjinga au uchawi haupo kwanini nchi hii kuna sheria ya kudhibiti uchawi -Witchcraft Act?

Wewe kama hujawahi shuhudia uchawi piga kimya tu sababu sisi wengine tuna shuhuda nyingi tu za uchawi.
Ulaya na Marekani uchawi umepungua sababu ujinga umepungua sana. Fuatilia vizuri utaona kuwa wajingawajinga ndiyo wanaamini hizi habari za uchawi.
 
Pole sana ndugu yangu,kama wewe ni mpagani hakuna asiyejua kama uchawi upo,kama wewe ni muumini wa dini zote,vitabu vyote vinaelezea kuhusu uchawi,lakini wengi wa wachawi huwa wanakataa kukubali uchawi upo,yawezekana ukawa mchawi
Fisi, Bundi, Paka weusi nk, ni viumbe wazuri wenye manufaa. Hawahusiki na "Uchawi."
 
Hakuna kitu kama hicho. Upigwe zile wanaita 50mm ya kichwa ubongo utawanyike harafu upone sababu ya chale!? Hizi ni habari za waganga matapeli wanaotafuta pesa ya kula.
I'm not here to debate Mimi nakupa fact nayoifahamu huku Kigoma so ukikubali or kukataa ni maamuzi Yako binafsi.
 
Karibu kigoma ndugu maana nina uhakika tokea umezaliwa hujawahi sikia mlio wa SMG. Huku zilikua zikiwaka huko Burundi tunazisikia mpaka huku mind you majambazi yalikua mengi sana huku kipande cha Biharu, Kibondo, Kakonko n.k.

So we know better

You're preaching to the choir. Kigoma naijua vizuri sana, nimefika kote huko hadi Burundi kabisa, naweza tuma file zima la picha hapa nikiwa Kigoma, mwisho wa siku ushirikina ni story tu zinazoaminiwa na watu mazwazwa. Zote ni hearsay na kuaminishana ujinga tu. Inabidi uwe zwazwa pro max kuziamaini.

Mwenzako huyu alisema diwani Kigoma kapotea kishirikina, kama kawaida ya watu mazwazwa wakaamini tu kama nyumbu, mimi nilimwambia nipe jina tu la huyo diwani hadi leo sijapata jina tu:

 
Yapo majambazi mengi huku Kigoma yame survive risasi sababu ya hizo chale. Ushirikina unatumika ndugu hata kikosi kilichokua kinawasaka kilikua kimeiva kwenye "dark arts".

Njoo huku Kigoma upate shuhuda za live live sio za kusimuliwa. Mimi napinga ushirikiana ila nakubali uchawi upo, in fact ukiwa mtu wa maombi huku huwezi kulala maana wanakuja "kukupima" usiku usiku.

Huu utopolo huwa unasomea wapi?
 

Wananchi wa Kijiji cha Sunuka, Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wameshirikiana na Serikali ya Kijiji kuchukua Waganga wa Jadi zaidi ya 10 kutoka Sumbawanga ili kukagua wachawi waliomo ndani ya kijiji chao wakidai ndicho chanzo cha utitiri wa vifo vya vijana katika mazingira ya kutatanisha.

Baadhi wa Wananchi walikusanyika na kuandama barabarani wakiimba “Tumechoka na uchawi” huku wakisapoti kile kinachofanywa na Viongozi wao.

Hata hivyo operesheni hiyo imepingwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani ambaye amezuiwa kuingia kijijini hapo ikiwa yupo kinyume cha mpango huo.

DC Dinah Mathamani amesema “Tumejadili na viongozi kuhusu suala hili, wale wanaojiita Waganda wanatakiwa kuondoka katika wilaya yetu, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na viongozi wanaoshirikiana nao.

Chanzo: UFM
DC mwenyewe anatamani apate kinga awe na uhakika na nafasi yake
 
Hakuna uchawi wa kuzuia risasi. Hayo ni matokeo ya ujinga. Yalianza huko kwa Kinjekitile. Na si Kinjekitile tu, Wahindi wekundu walikuwaga nao na mganga aliyewadanganya kuwa ana dawa wakipigwa risasi na wazungu hazitawadhuru. Na zaidi ni kuwa jeshi hupingq vikali imani za kishirikina. Maana nirahisi sana kudemoralize jeshi linaloamini uchawi.
Home boy haya mambo ni kweli,kuprove inakuwa na utata ila binafsi nimeshuhudia mwizi akichomwa tena kwa mafuta lakini ajabu hakuwa akiungua
 
Naunga mkono uamuzi wa wanakijiji. Kwa kuwa Serikali yenu inajifanya kutoamini uchawi japo wanakesha kwa Sangoma kutafuta vyeo. Basi wananzengo acha wawasake wachawi wenyewe. Na huyo DC aoneshwe advertise kidogo. Ajikute uchi ofisini.
Aheshimu imani za watu
 
Eti hata upige risasi ngapi humuui? Mtu asipokufa ni mipango ya Mungu tu na siyo nguvu za uchawi vinginevyo hao Wachawi wenyewe wasingekuwa wanakufa.
Sasa unachobisha ni kipi haswaa? Njoo Kibondo au Kahama ndio ubishe sio umekaa Dar kwenye kiyoyozi unaleta ujuaji.

Hizo risasi sio kama zinapenya Bali Zina deflect kwenye mwili.... na majambazi wengi tu waliostaafu watakueleza hayo mambo yanavyofanya kazi Wala haihitaji ujuaji.

Na sio Tanzania tu hata nimewahi weka thread ya Reuters kuripoti kuhusu Polisi wa Mexico kulalamikia wauza madawa kutumia uchawi unaozuia risasi.

Tupunguze ujuaji tuzunguke mikoa tujifunze.
 
Uchawi upo ndugu ndio maana hata jeshini wanafundishwa dark arts. Hata askari waliokua wanapambana na majambazi ya Kahama na Kibondo walikua wanatumia dark arts Ili kuwamaliza bila hivyo hata ungerusha risasi ngapi humuuwi.
Ni ya kweli ya jeshi kuendeshwa kishirikina Mkuu?
 
Ni ya kweli ya jeshi kuendeshwa kishirikina Mkuu?
Ndio mkuu ingia mtandaoni tafuta declassified missions za MK Ultra ama Dr Mulholland wa CIA. Kazi yake ilikua ni kuwapika majasusi wa USA kwenye eneo la kutumia "dark arts" kupambana na maadui zake.


 
Dark arts,hebu nipe a,b,c

 
Kigoma, mwisho wa siku ushirikina ni story tu zinazoaminiwa na watu mazwazwa. Zote ni hearsay na kuaminishana ujinga tu. Inabidi uwe zwazwa pro max kuziamaini
Nimesoma nimeishia hapo, nimegundua huna unalolijua kuhusu mkoa wa Kigoma. Kupiga picha Ukiwa kibirizi haikufanyi ukaijua Kigoma vizuri.

Wewe ukipita Kigoma nitakua mwenyeji wako ubishi utaisha. Why tubishane na uhalisia upo.
 
Back
Top Bottom