Waganga wa jadi 10 wapelekwa Kigoma kupambana na Wachawi, DC aweka ngumu

Waganga wa jadi 10 wapelekwa Kigoma kupambana na Wachawi, DC aweka ngumu

Nimesoma nimeishia hapo, nimegundua huna unalolijua kuhusu mkoa wa Kigoma. Kupiga picha Ukiwa kibirizi haikufanyi ukaijua Kigoma vizuri.

Wewe ukipita Kigoma nitakua mwenyeji wako ubishi utaisha. Why tubishane na uhalisia upo.

Tatizo lenu mnadhani nyie tu ndo mnaijua Kigoma kama kawaida ya waamini ushirikina hamna logical reasoning whatsoever. Kigoma kuanzia mjini, Kasulu, Uvinza, Manyovu, Mnanila hadi Burundi nimefika countless times FYI. Nakufahamu kama kiganja changu cha mkono. Hamna ushirikana zaidi ya ujinga na umaskini na kuaminishana story za kusadikika, mazwazwa wanaamini moja kwa moja kama nyumbu.

Msaidie mwenzako kutaja jina la diwani aliyetoka kishirikina. Nilitaja hadi dau ila mwaka wapili sasa jina tu sijapata.
 
Unaamini kuna mamba hugeuka watu?
Ndio naamini, kama fimbo ya musa iligeuka nyoka na ikameza nyoka wote wa waganga wafarao kwanini nisiamini kuwa mamba anaweza kugeuka kuwa mtu?

Uchawi ulisha kuwepo kabla hata ya ujio wa yesu ukisha lijua hilo basi huna hata haja ya kutilia shaka uwepo wa ushirikina katika ulimwengu wa leo
 
Uchawi upo wa kutosha katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika ukianzia hapo Ilagala,Sunuka nakuendelea mbele......Hao makamchape ni waganga ambao wanafanya madawa yao kuwapokonya uchawi watu wanaoutumia kudhuru watu...endapo atakapo nyanganywa akarudia kuushika tu anakufa.

Kama wewe sio mchawi hao waganga Makamchape hawawezi kukudhuru kwa chochote.

Mkuu wa Wilaya ni mgeni wa hayo mambo sasa anataka kuleta hisia za kiserikali kwenye mambo ya kienyeji sasa ni bora angekaa faragha na viongozi wa kijiji ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo sasa kama watu wanavyodai kuna mamba za kichawi zinapoteza watu.....hali hii ikiendelea atalaumiwa yeye kwa kutoa amri ya kuwafukuza hao wafichua uchawi.
 
Wamuloge kwanza huyo DC ili tu prove Kama wanachodai ni kweli.kama DC hajalogwa Basi ni uongo!!
Unahisi huyo Dc kurogwa inashindikana kijana....kuna mambo ya kienyeji yapo sana na yanafanya Kazi.

Kuna trafki mmoja hapo KG alikuwa mtata alipigwa Ugonjwa na hedhi Mwaka mzima...unaambiwa sasa hivi kapoa.....kuna Hakimu alivimbishwa tumbo kama mimba mwishowe akafa.

Hatutakiwi kuamini ushirikina ila upo mzee,hapo Kigoma ni mambo yapo toka Kitambo.
 
Ukimsikia mtu anapinga kuwepo kwa wachawi, mwangalie Mara mbilimbili, utakuta anafuga bundi ili kuwinda panya!, anamiliki fisi usiku ili kulinda mifugo! Wachawi wanataka "maggles" kwa mujibu Harry Potter wasijue kinachoendelea duniani
Umenikumbush Prof. McGonagall.
 
Ila wewe ujue ni comedian🤣
😂😂ni hatari boss. Ndio maana inatakiwa viongozi tuombewe mara kwa mara.
tapatalk_1580568781107.jpeg
 
Sasa unachobisha ni kipi haswaa? Njoo Kibondo au Kahama ndio ubishe sio umekaa Dar kwenye kiyoyozi unaleta ujuaji.

Hizo risasi sio kama zinapenya Bali Zina deflect kwenye mwili.... na majambazi wengi tu waliostaafu watakueleza hayo mambo yanavyofanya kazi Wala haihitaji ujuaji.

Na sio Tanzania tu hata nimewahi weka thread ya Reuters kuripoti kuhusu Polisi wa Mexico kulalamikia wauza madawa kutumia uchawi unaozuia risasi.

Tupunguze ujuaji tuzunguke mikoa tujifunze.
Dar ndiyo inaongoza kwa kuwa na waganga wa kienyeji wengi
 
Tatizo lenu mnadhani nyie tu ndo mnaijua Kigoma kama kawaida ya waamini ushirikina hamna logical reasoning whatsoever. Kigoma kuanzia mjini, Kasulu, Uvinza, Manyovu, Mnanila hadi Burundi nimefika countless times FYI. Nakufahamu kama kiganja changu cha mkono. Hamna ushirikana zaidi ya ujinga na umaskini na kuaminishana story za kusadikika, mazwazwa wanaamini moja kwa moja kama nyumbu.

Msaidie mwenzako kutaja jina la diwani aliyetoka kishirikina. Nilitaja hadi dau ila mwaka wapili sasa jina tu sijapata.
Aliyepotea najua alikua Diwani anaitwa Kanguye ila alipotea kipindi hicho 2018-20 huko Kakonko. So not sure huyo anamuongelea nani maana yule hata mwili haukuonekana mpaka Leo.
 
Hakuna uchawi wa kuzuia risasi. Hayo ni matokeo ya ujinga. Yalianza huko kwa Kinjekitile. Na si Kinjekitile tu, Wahindi wekundu walikuwaga nao na mganga aliyewadanganya kuwa ana dawa wakipigwa risasi na wazungu hazitawadhuru. Na zaidi ni kuwa jeshi hupingq vikali imani za kishirikina. Maana nirahisi sana kudemoralize jeshi linaloamini uchawi.
We kweli mtupu sana!

BADO sana mkuu!

Mungu mwenyewe anajua upo na anasema "usimuache mchawi akaishi"akimuagiza Musa,wewe unakata SASA sijui unataka proof gani we jamaa!!
 
Aliyepotea najua alikua Diwani anaitwa Kanguye ila alipotea kipindi hicho 2018-20 huko Kakonko. So not sure huyo anamuongelea nani maana yule hata mwili haukuonekana mpaka Leo.

Sasa wenzako wanasema kuna diwani alipotea na bdae akarudi kishirikina. Uzi huo hapo. Story zote za ushirikina ni story za hearsay zilizokosa logic wala proof, kuaminishana ujinga ujinga tu ndo maana story hizi hutamalaki sana kwenye jamii ya watu wajinga na maskini.
 
Wakimaliza hiyo kazi ya kutafuta wachawi waje tuwape tenda ya kusaka mafisadi na wala rushwa serikalini labda watatusaidia kupunguza huo ugonjwa

Ajabu watasema hawawezi. Wanasema wanaweza Kila kitu kupaa angani, kupenya ukutani, kuzuia risasi ila kufanya jambo lolote la maana lionekane mbele ya jamii kama uthibitisho hawawezi. Inabidi uwe zwazwa pro max kuamini hizi story 🤣🤣🤣
 
Naona DC yupo upande wa wachawi,wanapata vyeo toka kwa wachawi japo wanapinga uchawi
 
Back
Top Bottom