Waganga wa kienyeji na wachawi ni mawakala wa shetani, kwanini wanapingana

Waganga wa kienyeji na wachawi ni mawakala wa shetani, kwanini wanapingana

Kwa stairi hiyo basi hao manabii wa kweli ni wachache mno maana siku hizi watu wanataka huduma ya miujiza na ndio maana makanisa yamekuwa mengi kuliko villinge vya waganga kwa ajiri ya kutoa huduma ya miujiza.
Ni Kweli,

Watumishi wa Mungu wa Kweli ni Wachache kuliko matapeli,

Ni sawa tu na njia ya Mbinguni, ni nyembamba sana, lakini ya kwenda kuzimu ni Pana, na wengi wanaingia humo,

Mfano mdogo, dini kubwa mbili uzijuazo, ni Mali ya Popee, anahakikisha wote wale waliomo anawapeleka chini, lakini Kwa nje wanaamini wanaenda Mbinguni.

Wengine amewambia ukimchinja kafiri utaona Pepo, wengine anawambia kunywa kidogo usilewe, na sasa amewambia mashoga wanafaa kubarikiwa,

Ndo ujue njia ya Mbinguni ni nyembamba sana.

Ubarikiwe.
 
Walokole wahaheshimika sana huko katika medani za Ulimwengu wa Roho.

Kwa nje utawaona wa kawaida, ndani ni giants hatari.
Kuna walokole wazinzi, walevi, majambazi nk
Kuna wapagani sio wazinzi, sio walevi, sio majambazi nk.

Umetumia vigezo gani kusema walokole wanaheshimika sana katika ulimwengu wa Roho?

Nadhani ungesema walolole wanaofata misingi ya kristo, maana ulokole ni sifa tu hata mchawi anaweza kusema ameokoka.
 
Mungu aliumba Malaika kama watumishi wake,

Walipoasi, wakalaaniwa na kubadilishwa title kuwa mapepo, mashetani nknk.

Mizimu, mapepo ni viumbe vilivyolaaniwa na Mungu, kamwe usikubali kudanganywa upate ulinzi wao, ni waongo.

Mungu ndiye mlinzi wa Kweli.
Kwahiyo kumbe hawa majini,mizimu,mashetani n.k ni malaika ila na matendo yao ndio yaliyofanya walaaniwe na kuitwa hayo majini mizimu mashetani n.k?
 
Kuna walokole wazinzi, walevi, majambazi nk
Kuna wapagani sio wazinzi, sio walevi, sio majambazi nk.

Umetumia vigezo gani kusema walokole wanaheshimika sana katika ulimwengu wa Roho?

Nadhani ungesema walolole wanaofata misingi ya kristo, maana ulokole ni sifa tu hata mchawi anaweza kusema ameokoka.
Peaky blinders...mafia family
 
Hao wanaotumia nguvu za Giza madhabahuni ni agents wa kuzimu,

Ni sawa tu na mganga avue kaniki, avae sauti na kufungua Kanisa.

Mungu ameruhusu hayo maana yapo na yalishataniriwa katika maandiko.

Lakini, Manabii wa Kweli wapo, hawauzi miujiza, wamepewa karama Bure, wanatoa bure.

Ukienda Kwa nabii, anayetoza fee kumuona ni WA UONGO, ikiwa ana kashfa za kuzini na waumini, ni WA UONGO huyo. Nk nk

Mungu akusaidie kuwatofautosha.
tusaidie mfano wa nabii wa kweli mkuu
 
Mchawi anaweza kukuroga, ukaenda kwa Mganga, then Mchawi akaenda kwa Mganga ama kumuomba au kumpa Rushwa ili asikutibie, ikiwa Nguvu za Mganga ni kubwa kuliko za Mchawi...!

Source ya Nguvu zao ni Moja...! Ni kama Maigizo ya CCM.
Lakini navyojua wakati mwengine mganga anaweza kukutajia dawa ya tatizo ukaitafuta mwenyewe na ukajitibu tatizo lako pasina kutibiwa na mganga, je hapo source ya nguvu ya hiyo dawa inatoka wapi?
 
Uchawi na ushirikina ni mind of game na ni eneo la ambalo halina nguvu.

Mganga
Mshirikina

Wote hawa ni watu wa kawaida Sana.
Ukielewa haya mambo utajua uchawi unavyofanya kazi.
Kwa maana kwamba mtu unaweza kwenda kwa mganga kwa kutaka kumroga mtu afe na akafa kweli au awe chizi awe chizi na kweli akawa chizi huwa ni mind game tu hatujajua?
 
Kuna walokole wazinzi, walevi, majambazi nk
Kuna wapagani sio wazinzi, sio walevi, sio majambazi nk.

Umetumia vigezo gani kusema walokole wanaheshimika sana katika ulimwengu wa Roho?

Nadhani ungesema walolole wanaofata misingi ya kristo, maana ulokole ni sifa tu hata mchawi anaweza kusema ameokoka.
Waliookoka/ Wana wa Mungu, waliozaliwa mara ya pili, waliojazwa Roho mtakatifu Wana ALAMA/CHAPA/ MUHURI katika mapaji ya nyuso zao.

Ni kama tu wachawi, wana CHAPA na ALAMA zao,

Hawa wengine ambao wako katikati ni wafungwa, Mungu anawasuburi watubu, na shetani anataka aendelee kuwafunga Ili awapeleke kuzimu.

So check ikiwa una alama ya Mungu, ikiwa Jina lako limeandikwa katika KITABU Cha Uzima.

Tofauti na hapo, wewe ni sawa na mpiga debe kwenye basi la waenda Mbinguni, wakiondoka WATAKATIFU wewe unabaki.
 
Asili zao ni kuzimu,

Katika ukoo, ukiambiwa Mizimu ya ukoo inataka hili au lile Ili mfanikiwe katika jambo Fulani, jua ni shetani huyo.

Kwa nje ni kama anawapa ulinzi, lakini anataka aabudiwe, na ndiyo chanzo Cha matatizo, mf magonjwa ya kurithi, vifo vya kijirudia tarehe mwezi, kutolewa, nk nk
hii mizimu ya ukoo ni kitu common sana kukisikia, utaambiwa mizimu ya ukoo inataka hiki au kile
tunaepukaje? tukiacha kufanya vile inataka hatupati madhara?
 
Waliookoka/ Wana wa Mungu, waliozaliwa mara ya pili, waliojazwa Roho mtakatifu Wana ALAMA/CHAPA/ MUHURI katika mapaji ya nyuso zao.

Ni kama tu wachawi, wana CHAPA na ALAMA zao,

Hawa wengine ambao wako katikati ni wafungwa, Mungu anawasuburi watubu, na shetani anataka aendelee kuwafunga Ili awapeleke kuzimu.

So check ikiwa una alama ya Mungu, ikiwa Jina lako limeandikwa katika KITABU Cha Uzima.

Tofauti na hapo, wewe ni sawa na mpiga debe kwenye basi la waenda Mbinguni, wakiondoka WATAKATIFU wewe unabaki.
jambo zuri kuwa na chapa ya Mungu
Tunajuaje mtu ana hiyo chapa
au tunajuaje jina limeandikwa kwenye kitabu cha uzima
 
tusaidie mfano wa nabii wa kweli mkuu
Mwalimu Mwakasege, Mchungaji Amiel Katekela, Jackob Steven wa Huduma ya Kristo, Mwalimu Tengwa wa Tengwa Tv, Boniface Victor wa UNYAKUO TV, Mchungaji Mbarikiwa nk nk

Mungu akusaidie kuwatambua maana ni wengi, hata ulipo wapo, maana pia watu hubadilika, anaweza kuamua kubadilika na akawa wa UONGO.

Mungu atubariki.
 
  • Thanks
Reactions: 511
Kwanza kabisa athibitishe uchawi upo na shetani yupo.

Tusije kubishana sana kuhusu vitu ambavyo havipo.
Hili suala la uthibitisho ni tata maana mfano unakuta inajulikana hakuna dawa ya ugonjwa fulani lakini kuna watu huko wanatumia mitishamba yao kutibu ugonjwa huo huo ila kwa kuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi kwa dawa hiyo basi inaendelea kubaki kuwa huo ugonjwa hauna dawa.
 
Labda mganga ni kama mahakama ya rufaa na mchawi na mahakama za chini.
 
jambo zuri kuwa na chapa ya Mungu
Tunajuaje mtu ana hiyo chapa
au tunajuaje jina limeandikwa kwenye kitabu cha uzima
Lazima kwanza uwe umemkiri Yesu kuwa BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAko.

Lazima uwe na Roho mtakatifu ndani anayekushuhudia kuwa wewe ni mwana wa Mungu.

Na lazima uisikie sauti na maelekezo ya Roho mtakatifu ndani Yako,

Lazima uchukie dhambi na uishi maisha matakatifu,

Lazima uwe mtu wa maombi na kusoma neno lake,

Lazima uwapende wenye dhambi na kuwaombea na kuwahubiri Ili waokoke.

Ubarikiwe.
 
Kwa maana kwamba mtu unaweza kwenda kwa mganga kwa kutaka kumroga mtu afe na akafa kweli au awe chizi awe chizi na kweli akawa chizi huwa ni mind game tu hatujajua?

Uchawi unaishia dimension 03
Sasa ukiona unalogwa ujue tatizo kubwa lipo kwako wewe unayelogwa.

Maana ili ulogwe lazima lango lako liwe wazi.

Kuna innocence na guilty ukiwa innocence- (Mnyongofu) haumdhuru MTU wala kumuazia MTU mabaya ukiishi hivyo hata Kama hauendi msikitini au kanisani huwezi kulogwa.

Ili ulogwe lazima ulogeke , na njia rahisi ya kulogeka ni kuwa guilty kinyume cha innocence ni guilty.

Ukiona MTU anasema uchawi Una nguvu au amelogwa basi ujue yeye ndo Ana matatizo ameruhsu Giza ndani yake.

Unaweza kuona hii michezo yao wachawi huwa wanafanyiana wao kwa wao na sio watu wengine.

Wanawake huwa wanapitia hizi changamoto za kulogana kwa sababu hawapo innocence.

Dimension zipo nadhani hadi 7+ na uchawi huishia dimension 3 tu sasa ili ulogwe unakuwa umekubali mwenyewe kulogeka.

Ndo wajanja huwa wakiiba wanatubu na kujaribu kutakatisha walichokiiba hii yote hufanya ili kupandisha dimension ili wasiwe guilty na wakitubu huwezi kupiga ramli (dogma) ukawapata.

So uchawi MTU anayesema Una nguvu ni muhongo uchawi umekuzwa na mashekh na wachungaji bila sababu za msingi.
 
Waliookoka/ Wana wa Mungu, waliozaliwa mara ya pili, waliojazwa Roho mtakatifu Wana ALAMA/CHAPA/ MUHURI katika mapaji ya nyuso zao.

Ni kama tu wachawi, wana CHAPA na ALAMA zao,

Hawa wengine ambao wako katikati ni wafungwa, Mungu anawasuburi watubu, na shetani anataka aendelee kuwafunga Ili awapeleke kuzimu.

So check ikiwa una alama ya Mungu, ikiwa Jina lako limeandikwa katika KITABU Cha Uzima.

Tofauti na hapo, wewe ni sawa na mpiga debe kwenye basi la waenda Mbinguni, wakiondoka WATAKATIFU wewe unabaki.
Wewe ukimuona mtu tu kwa sura yake unajua kama ana Roho Mtakatifu?
Utamtofautisha vipi mlokole kwa kumwangalia ukajua huyu kazaliwa kweli mara ya pili na huyu anaigiza.?
 
Back
Top Bottom