hii mizimu ya ukoo ni kitu common sana kukisikia, utaambiwa mizimu ya ukoo inataka hiki au kile
tunaepukaje? tukiacha kufanya vile inataka hatupati madhara?
(Mathayo 10:36)
Adui wa mtu ni yule wa nyumbani mwake, na YESU asema, sikuja kuleta Amani duniani, Bali UPANGA, kati ya baba na mtoto, Binti na mamaye nk nk
Ukiokoka, ukaamua kuachana na Ibada ya Mizimu, ujue unaanzisha vita ya kiroho,
Na adui zako watakuwa hao wa ukoo na familia Yako ya Damu na nyama, Kwa nje wanasali, ila ukimwambia Mimi sitafanya Mila au maelekezo ya Mizimu ya ukoo au family unakuwa adui nao,
Na ukiogopa kujitenga nao na kubeba msalaba wako kumfuata Yesu , sahau kuhusu mbingu, ni ya Wachache,
Ndiyo maana walokole huitwa wamechanganyikiwa, Ukiwa upande wa Mungu Kweli Kweli, lazima uwe adui wa Dunia.
Maisha ya wokovu ni vita Si lelemama, ukiona mtu anafanya Mila na Kanisani anaenda, analewa na Kanisani anaenda, huyo Bado Hana Ile ALAMA kwenye paji la uso.
Ubarikiwe.