UJENZI WA KUKURUPUKA
CCM waanche kuingilia mambo wasiyoweza, mfano michuano ya Afcon kule Arusha porini Olmothi maeneo yanayozunguka uwanja huo au stendi mpya Bondeni City ungelenga kuwa na mji mpya wa mfano uliopangika badala ya kugawa viwanja kimoja kimoja uwekezaji wa mfano wa aina ya kina Hamidu City Park ndio ungetiwa mkazo watu wanunue majengo na nyumba zilizojengwa kwa mpango na mipangilio siyo vurugu za ujenzi holela
View: https://m.youtube.com/watch?v=aiJCrekUkW0
BILIONI 2.5 KULIPA FIDIA WATAKAOPISHA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA ARUSHA...
Posted On: December 18th, 2023
Na Elinipa Lupembe.
Kufuatia mkakati wa Serikali ya awamu ya sita, wa kujenga uwanja wa mpira wa miguu, ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yanayotarajiwa kufanyika mapema mwaka 2027, Halmasahuri ya Jiji la Arusha, imetenga Shilingi Bilioni 2.5 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi watakayotoa maeneo yao.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo, kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Damian Ndumbaro ( MB), Mkurugenzi Mtendaji, Jiji la Arusha, Mhandisi Jumaa Hamsini, amesema kuwa Serikali ilitoa maagizo ya kupatikana Eka 83 na mpaka sasa tayari zimepatikana Eka 39, zikiwa zimeandaliwa Hati Miliki, huku Jiji la hilo likitenga shilingi Bilioni 2.5, kwa ajili ya kulipa fidia wananchi watakaopisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo wa mpira.
Amesema kuwa, tayari hatua zote zimeshafanyika, na Jiji limetenga kiasi hicho cha fedha, ambacho kitatumika kulipa fidia kwa wananchi ili kupata eneo la Eka 44 zitakazokwenda kukamilisha Eka 83 zinazotakiwa na Serikali ili kutekeleza ujenzi huo.
"Sisi kama Jiji la Arusha, tumeshajipanga vema, kuhakikisha adhma ya Serikali ya awamu ya sita, inafikiwa kwa kiwa na uwanja wa mashindano, viwanja vya mazoezi pamoja na miundombinu yote inayohitajika inajengwa hapa Mtaa wa Murongoine kata ya Olmoth na tutahakikisha mashindano hayo yatafanyika kama yalivyopangwa".Ameweka wazi Mhandisi Hamsini.
Awali, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, ametembelea na kukagua eneo linaloandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira na viwanja vya mazoezi, na hatimaye Jiji la Arusha kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella Hati Miliki ya Eka 39 na Kumkabidhi Waziri huyo mwenye dhamana.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa kimataifa mkoani Arusha, licha ya kuwa ni kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya AFCON lakini zaidi ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi unaokwenda kuwekeza kwenye utalii wa michezo katika mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla wake.
#arushafursalukuki
Source : arusha.go.tz
Waziri Mkuu akagua ujenzi Mji wa Serikali Mtumba
Imewekwa Tarehe: July 3rd, 2023
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Julai 03, 2023 amekagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu, majengo hayo yawe yamekamilika na kuwekwa samani, ili azma ya Serikali ya watumishi kuhamia kwenye majengo hayo ifikapo Januari Mosi, 2024 itimie.
“Dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutaka kuona watumishi wote waliohamia Dodoma wanafanya kazi kwenye majengo rasmi fedha imetengwa, imetolewa na itaendelea kutolewa”
“Tafuteni mbinu za kiufundi za kukamilisha majengo haya kwa wakati bila kuathiri viwango”Moja ya mbinu ni kusimamia ujenzi huu usiku na mchana, tunataka tumalize majengo haya, Watanzania wanataka kuona majengo yanakamilika na kutumika.”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wasimamizi wa ujenzi wa majengo kwenye mji wa Serikali watumie bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo nchini“. Rais Dkt. Samia amesisitiza kuhusu uwekezaji na amekuwa akialika wawekezaji wa nje na wa ndani kujenga viwanda vya bidhaa mbalimbali hapa nchini ikiwemo marumaru (tiles). Tutumie bidhaa zao badala ya kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.”
Source : dodoma.go.tz