Unasema hivyo kwakuwa una uhakika wa kula na kunywa,kuna wakati unasema bora ufe ukipambana kuliko kufa kibudu.
Mercenaries = Askari Mamluki = askari Wauaji kwa kulipwa =Mwajiriwa kuua kwa malipo.
Ikumbukwe kwamba Hao π π π wanafanya kazi ya kuua Binadamu wenzao kwa maelekezo ya Boss aliyewaajiri. Mercenaries wanawaua walengwa askari au raia au kuharibu miundombinu mahalia kadri watakavyoelekezwa na Mwajiri wao.
Hawa wauaji hawana ugomvi(Bifu) na hawana Maslahi yoyote kwa matokeo ya uharibifu utakaojitokeza. Askari Mamluki Wao wanaangalia MALIPO/MSHAHARA na marupurupu mengine watakayopewa kwa kazi yao. Suala la ni kwa nini unaua haliwahusu.
Matokeo ya kazi hiyo:-
1. Mamluki akiwahiwa (e.g vitani)anaweza uawa au kujeruhiwa; mamluki akiugua huonekana kama
Bidhaa inayo anza kuoza (
ku-expire) na hathaminiwi sana.
2.Mamluki aghalabu mzoga wake (
maiti)unaweza kutupwa tu porini kwani hana thamani akiwa amekufa (
useless dead horse)
3.Usipopewa Haki zako kutoka kwa Boss wako, huna mahali pa kuzidai hizo haki (huna pa kushitaki).
Mwisho:
Ningewashauri vijana waTZ kwamba licha na pamoja kwamba kuna ahadi za malipo kedekede HIYO KAMWE sio kazi njema hata kidogo. Inakuwaje kijana unakubali kwenda kumuUa mtu ambaye hata haumjui na wala huna ugomvi naye na hata Ukoo wako, Jamii yako, Nchi yako au Taifa lako halina ugomvi naye? Ni kwa sababu tu eti utalipwa pesa
ndefu ndo ukubali kwa hiari yako kufanya uovu wote huo????
Kama una uhakika wa Kula, Makazi ya kudumu (hilo kunywa ni
luxury) ni mwanzo mzuri; ridhika navyo kuliko kujihatarisha na kujiingiza kazini kusikostahili- ni kazi OVU haina baraka hata siku moja.
Si ni bora ukaingia mashambani au kujianzishia shughuli
Halali nyingine?