DOKEZO Wagonjwa wanapewa magonjwa ambayo hawana ili Zahanati ziuze dawa

DOKEZO Wagonjwa wanapewa magonjwa ambayo hawana ili Zahanati ziuze dawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii mkuu Hilo sikatai nilishafanya Sana kazi kwenye Hospitali za binafsi na Nilifanya hivyo pia..
Ila nilipokuwa Private tulifamya hivi ili kuongeza pesa..
Kwa mfano Mgonjwa atahitaji Amoxyciline..
Bhasi utampa antibiotic ambayo ni kubwa kuliko hiyo na inafanna kazi na hiyi kwa mfano Amoxicine Plus Clavulanic Amoclav...
NA ni kweli wanao ongoza ni Private..
Kwa hiki nakusuport sana na hata kwenye Bima tulikuwa tunachezesha sana
je EFFICACY zinafanana ?
 
swala la afya ukilichanganya na umaskini wako basi utaona hivyo ila swala la afya haliitaji kutizama pesa
Mimi ninayekuambia nimewahi kufanya kazi kwenye Hospitali za Private si chini ya 5 kwahyo nina uzoefu kwa ninachokisema
 
Kwa ushahidi ambao nimeshuhudia mwenyewe kwa matukio mawili.

1. Miezi ya katikati mwaka jana Kaka yangu aliumwa sana akawa anataka kununua mseto ameze. Mimi nikamshauri kuwa akaoime kwasababu kunywa dawa bila kupima unaweza kujikuta kwenye hatari ya kunywa dawa ambazo hazihusiani na ugonjwa.

Kweli nikamchukua mpaka kwenye maabara iliyopo jirani na mtaa wetu. Kufika pale akapimwa damu na majibu yakaja kuwa ana Typhoid

Palepale nikawa namkumbusha ndugu yangu kuwa jinsi ambavyo alitaka kunywa dawa za mseto kwenye ugonjwa ambao haumsumbui.

Wakati tunatoka maabara yule doctor akamshika mkono bro akamuanbia dawa tunazo hapa hapa tena unapona baada ya siku mbili tu.

Bro akamjibu kuwa mimi kuna sehemu ambayo huwa dawa nachukua bure.

Tulipotoka tukaenda pharmacy tukamuambia mhudumu atupe dawa ambayo inaoonesha haraka akatupatia.

Bro kameza zile dawa mpaka kamaliza dozi lakini hakuna mabadiliko, zaidi tukaona anazidi kudhoofika na kuwa katika hali ya hatari.

Hapo ndio ikabidi nimpigie rafiki yangu ambaye ni Doctor kumuomba ushauri akaniambia nenda kituo fulani ukapime hiyo itakuwa ni Maleria.

Tumepima majibu yamekuja ni Maleria madaktari wakawa wanamlazimisha kumchoma sindano na kumpa kitanda eti hali yake sio nzuri.

Dozi ya sindano ni 6 halafu kila sindano gharama ni 6,000, tukakataa.

Tukaenda kununua mseto akanywa na siku inayofuata tu akawa amepata nafuu. Dozi ilivyoisha tayari alikuwa yupo fresh kila kitu.
usilete ujuaji kwa daktari siku nyingine utamuua ndugu yako , yupo mtu x alienda kituo x hapa dar akakutwa na ugonjwa x wa macho akashauriwa operation tena ilikuwa anafanyiwa bure ila analipia kitanda na huduma ya chakula jumla 100k kwa siku 2 akampigia rafiki yake daktari akampoteza akamwambia akanunue dawa x bila kumuona , asee kaamka siku ya 2 jicho limeanza haribika kajifanya kuvimba akaamka next day jicho limeanza ozaa , kaenda mhimbili wanamwambia ni la kutoa tu , jamaa ss hv ni chongo , TUHESHIMU MADAKTARI , UKIPIMA CHUKUA DAWA HAPO HAPO MAANA KUNA SWALA LA QUANTITY NA DURATION VITAKUZINGUA TU
 
  • Thanks
Reactions: apk
Ni mtihani sana hasa vituo vya afya vile vya binafsi huwezi kupima ukaambiwa mzima either usingiziwe malaria, UTI au typhoid , hili ni tatizo sana kucheza na afya za watu
kuna siku umeenda kupima ukiwa mzima ? tusipende tu kulalamika wazee , tamaduni zetu tunapima tukiona hatupo vzr kiafya Je unategemea uambiwe mzm
 
Kisa cha pili

Usiku mmoja niliumwa tumbo, asubuhi kulivyokucha tu nikaibukia kwenye kituo cha Afya.

Nikaandikishwa dirishani nikapewa maelekezo kuwa nikamuone daktari chumba fulani.

Daktari akaniuliza kinachonisumbua nikamjibu kuwa ni tumbo pale pale akaniambia hiyo ni Typhoid.

Nikambishia nikamuambia Typhoid haiwezi kuwa kwasababu nina miaka mingi nakunywa treated water na hata vyakula vibicho kama chumbari huwa sili.

Akaniambia hata kama unaepuka njia hizo bado njia za kuweza kupata Typhoid ni nyingi kwa mfano ukawa unakula migahawani.

Nikashangaa kusikia hoja ya aina hiyo kutoka kwa Doctor ikabidi nimuulize hao wadudu wanapenya vipi mpaka wakweza ku survive kwenye chakula ambacho kishakuwa boiled?

Maana yake hata ule ushauri wa kiafya kuwa tunywe maji yaliyo chemshwa basi hauwezi kuwa na impact yeyote kwenye kuzuia wadudu enezi wa Typhoid.

Doctor akaniambia Typhoid unaweza kuipata kwa njia nyingi hata kupitia maji ya chooni unayotumia kutawaza.

Hapo ndio nikabaki mdomo wazi. Akaniambia nenda maabara chumba kinachofuata ukapime.

Nikapima damu, majibu niliyosomewa na Doctor ni kuwa nina vidonda vya tumbo pamoja na Typhoid.

Wakanitajia gharama za dawa kuwa ni 25,000 nikawaambia sawa ila mi kwa saizi sina hiyo hela ila naombeni mnipe hiyo tipoti ya vipimo niondoke nayo ili nikipata hela niende duka la dawa niwaoneshe hiyo report wanipe dawa.

Wakakataa wakaniambia hawatoi ripoti ya vipimo na kama sina hela basi nirudi tu nyumbani nijipange, siku nikapata nitarrjea hapo wanipe hizo dawa.

Sikuridhika na majibu yao ya vipimo hususani ya kuniambia nina Typhoid. Nilipotoka hapo nikaenda kwenye kituo cha Afya Cha Arafa.

Sababu ya kwenda kwenye hicho kituo ni kutokana na kushawishiwa na rafiki yangu kuwa hicho ndio kituo kinachotoa huduma bora kwasababu mke wake alihudiwa hapo.

Kufupisha stori

Niliandikiwa vipimo viwili hapo Arafa

Kipimo cha kwanza kilisema nifanyiwe checkup ya Ultra Sound kuangalia damage ya tumboni

Kipimo cha pili kilikuwa ni damu. Vipimo vyote kwa ujumla niliambiwa nilipie 25,000.

Lakini nilipimwa kipimo kimoja tu ambacho ni cha damu. Hakukuwa na Ultra Sound na wala pesa yangu niliyolipia kwa ajili ya kipimo hicho haikurudishwa.

Nilipofika kwa daktari akaniambia vipimo vimeonesha nina vidonda vya tumbo akaniambia nenda dirisha la dawa

Nilipoenda kwenye dirisha la dawa niliambiwa nilipie 99,000.

Nikasema hiyo hela sina kwa sasa ila naombeni ripoti ya vipimo wakaninyima

Kwa bahati nzuri niliwahi kupiga picha ripoti ya maabara ila ile ya kwa Doctor sikuweza kuipata.

Almost Miezi minne now nimeweza kutibu vidonda vya tumbo kupitia maoni ya wana JF bila kutumia midawa yao ya kausha damu.
ubishi sio ujanja , ipo siku kitaumana , angekuwa mchina hata dawa ya laki 1 utatoa
 
Siyo ngazi za chini tu mkuu hata huko ngazi ya juu kuna mauza uza ya aina yake ambayo yakiandikwa hapa watu watachukia wataalam wetu
tatizo ni wewe umaskin wako umekuwa ttzo ila naamin mganga wa kienyej utamuamin
 
Uende Masana, Rabininsia, Bochi ukoswe na ugonjwa wataka wao waishi vipi?
 
usilete ujuaji kwa daktari siku nyingine utamuua ndugu yako , yupo mtu x alienda kituo x hapa dar akakutwa na ugonjwa x wa macho akashauriwa operation tena ilikuwa anafanyiwa bure ila analipia kitanda na huduma ya chakula jumla 100k kwa siku 2 akampigia rafiki yake daktari akampoteza akamwambia akanunue dawa x bila kumuona , asee kaamka siku ya 2 jicho limeanza haribika kajifanya kuvimba akaamka next day jicho limeanza ozaa , kaenda mhimbili wanamwambia ni la kutoa tu , jamaa ss hv ni chongo , TUHESHIMU MADAKTARI , UKIPIMA CHUKUA DAWA HAPO HAPO MAANA KUNA SWALA LA QUANTITY NA DURATION VITAKUZINGUA TU
Nyie ni madaktari njaa

Hamumuangalii mtu kama mgonjwa, mnamuangalia kama mteja na opportunity ya kumpiga kwenye bei kubwa za dawa ambazo hazihusiani na magonjwa yake.

Hata kama kuna option ya dawa ambazo ni nafuu hamuwezi kumtajia hizo dawa kwasababu zina maslahi madogo kwenu.

Mna Roho mbaya sana
 
Ngazi ya hospital angalau lakini zipo hospital zinafanya hiyo,, ila hali ya namna hii pia ipo ngazi za chini, mimi nimeshuhudua na kupata case za namna hiyo mara kadhaa ,kuna sehemu asilimia 90 ya wanaoenda anawaambia wana malaria parasite 1,2 au 3,anaandikia mpaka sindano, lakini hakuna mabadiriko
je mnaisha mazingira free from malaria exposure ? muda mwingine mnakuwa wajuaji wa vitu vya kitoto , watz wengine wanalala bila neti na mazingira ya nje ni rafiki kwa malaria vectorborn , sisi ni wachafu hatujui kusafisha mifereji jiran inayounda maji yaliyotuama , hatujui kusafisha vichaka vya jiran yetu , tunapenda kurundisha uchafu ndan ya mazingira jiran yetu na bado tunashangaa ddx za malaria , uti na typhoid kuwa nyingi ,TUPENDE KUFANYA RESEARCH KABLA YA KUHUKUMU
 
Wakati mwingine dispensary uchwara wakiwa na dawa zinakaribia kuisha muda wake kila mgonjwa ataambiwa anaumwa ugonjwa wa dawa hizo ili dawa ziishe.
 
Hakuna Ubaya lakini si unajua Amoxyclav iko limited kwa baadhi ya magonjwa ya Mfumo wa Mkojo japo ni nzuri sana kwa mfumo wa Magonjwa ya Mfumo wa hewa..

Il lengo ni kumaximise profit mkuu..
Mteja angweza kupewa Amxy ya Tsh 2500 mpaka 3000..
Ila unaamua kumpa amoxyclav Ya 20k mpka 25k..
Lengo ni Biashara na sio Cost effectvness
kwann usijipime na kujitibu ? umeenda kwa daktaru ukampangie matibabu ?
 
Mimi ninayekuambia nimewahi kufanya kazi kwenye Hospitali za Private si chini ya 5 kwahyo nina uzoefu kwa ninachokisema
kwenye afya ukianza fikiria ela , utaona unaonewa , ili kituo kiendelee kuhumia wengine lzm daktari atoe huduma bora ila pia kituo kiingize kipato wahudumu walipwe , sasa ni wajibu wako wewe mgonjwa unataka huduma ya bei nafuu isiyo na waranty ya usalama wako au unataka huduma ghali yenye waranty ya usalama wako
 
Mkuu!
Daktari Bora haangalii Only Efficacy ya Dawa..
Lazma uchague dawa Yenye low side effects plus Cost Effecveness..
Unless utakuwa mfanyabiashara tu..
Lazma ujue unatibu kina nani na wana Uwezo kiasi gani kabla ya kuchagua dawa ya kuwapa
unaangalia cost au afya bora ? na hii ndo asili ya mtu mweusi hataki kusimama na kitu kimoja , wenzetu ukiwahudumia hadi raha , twende zahanati za gov km hatujiamini kipesa
 
Nyie ni madaktari njaa

Hamumuangalii mtu kama mgonjwa, mnamuangalia kama mteja na opportunity ya kumpiga kwenye bei kubwa za dawa ambazo hazihusiani na magonjwa yake.

Hata kama kuna option ya dawa ambazo ni nafuu hamuwezi kumtajia hizo dawa kwasababu zina maslahi madogo kwenu.

Mna Roho mbaya sana
dawa nafuu nyingi zina side effects nyingi na slow sana kuleta mabadiliko , kwann msigoogle kwann bei zinatofautiana
 
kwenye afya ukianza fikiria ela , utaona unaonewa , ili kituo kiendelee kuhumia wengine lzm daktari atoe huduma bora ila pia kituo kiingize kipato wahudumu walipwe , sasa ni wajibu wako wewe mgonjwa unataka huduma ya bei nafuu isiyo na waranty ya usalama wako au unataka huduma ghali yenye waranty ya usalama wako
MKuu naomba niseme wazi kuwa watu kama nyinyi huwa mnanipa hasira sana na ndio mnaipaka Matope Taaluma ya Afya na Udaktari..

Niseme wazi tu Udaktari ni kazi ya Wito isiyo Na faida ni Bora muondoke mkatafute kazi zenye Faida na mtupishe...

Ikiwa kuna Dawa mbadala yenye Uwezo sawa na mgonjwa ana uwezo wa kupata Dawa yenye pesa kidogo kwanini usianze na dawa yenye pesa kidogo??

Mlipokuwa mnafundishwa Kuhusu Cost effectvness mlikuwa wapi? Vyuoni..

Kuwa daktari au kuwa kwenye sector ya afya Haikufanyi wewe kuwa Mungu wa kuamua maisha ya watu..
Ila kunakupa nafasi ya kutatua matatizo ya watu kwa kadri uwezavyo na sio kuyongeza
 
Ujumbe huu ufike Serikalini hasa kwa Wizara ya Afya, sasa hivi baadhi ya vituo vya maabara vinafanya kitu kimoja, ukienda kupima hata kama huna Typhod majibu yao ni una-typhod, unajikuta unatumia dawa huponi.

Ukienda kupima tena bado majibu ni unatyphod, sasa hii ni hatari sana, watu wanakunywa dawa za typhod kumbe hawana changamoto hiyo.

Mimi ilinikuta mpaka nikaenda Mount Meru kupima ndio wakanambia sina typhode nina ‘uric acid’ nyingi sana kwenye mwili.

Nilipofuatilia kwa ndugu na watu wangu wa karibu nimegundua kuwa changamoto za aina hiyo zipo nyingi, zahanati zinafanya vipimo kama biashara ili wahusika waweze kuuza dawa, tena wagonjwa wengi wanauziwa anti biotic ili mradi tu biashara ifanyike, Serikali iangalie hicho kinachoendelea.
Wee unafikiri zinajiendeshaje wasipofanya hivyo..
Tena unaandikiwa na sindano 5 na kila sindano ni 5000
 
Back
Top Bottom