Shida kubwa kwenye kipimo kilichozoeleka cha urine dipstick ni mpimaji mwenyewe huenda ni colour blind hivyo anashindwa ku compare colours anaishia kusema mtu ana UTI.
Shida ya pili huenda mgonjwa kipindi analeta sample alikuwa hajala muda mrefu hivyo ukipima unakuta ketones zimepanda japo leucocyte zipo normal anaandikiwa madawa.
Kingine sample imekaa muda mrefu kwa hiyo rangi kwenye zile strips zinachange mwisho wa siku anaambiwa ana UTI.
Kwa hiyo hapa shida sio kwa daktari shida ipo kwa lab technician kutokuwa competent anapelekea daktari kupata wrong ddx.
Safi Sana mkuu kusema ukweli, ambao wengi tunauficha!
Kuongezea hata wanaotumia machine za urine analyser machine hazioshwi kwa kila sample na mda mwingi inapelekea majibu kufanana..
Na hata kwa microspy Vile vile kwa wanaopima sediments....
Japo ukiniuliza Mimi kati ya kipimo cha mkojo nachokubali Accuracy kati ya dipstics na Urine sediments nitakujibu Bora sediments..
Handling ya Dipsticks Iko poor Hata upimaji wake poor wengi wanaopima Ni Untrained Personell..
Utunzaji wa Dipsticks hata sample zinavyokuwa collected mpaka Kupimwa Obvious lazma ukute Leococytes na makorokoro mengine..
Kimbembe kipo kwenye utambuzi wa Majibu (Interpretation) hapa ndo unaweza kucheka..
Madaktari wa sasa sijui wanasoma wapi au wanajifunza wapi?
Unakuwa Urobirinojen zimesoma nyingi ila vipimo vingine viko normal Mtu anaambiwa ana UTI anaandikiwa Dawa..
Ketones Ziko nyingi anapigwa antibiotics..
Yaani sijui kama walisoma hata Micro na clinical Lab.. Ni tabu kwaweli ni Aibu ukienda kukagua na kufanya Supervision unaweza ukatamani kumtandika vibao Mtoto wa Mtu lakini ukaona bora umuache tu..
Kamuandikia Mgonjwa Dawa za kutosha Cefotaxine 1g BD kwa siku 7 kisa ketones kupitia Faili la mgonjwa ni DM cases unasema sasa huyu Alipita Hata Internship kweli?
NA alipataje kuwa daktari..
Asiyejua hata Alitakiwa afanye nini baada ya kuona Ketone kwa mtu aliye na DM na akamuacha anaenda nyumbani huu si uuaji kabisa?
VItu vingine kwa Layman huwa ni normal ila kwa mtu unayejua huea vinatia hasira sana kuvitazama