DOKEZO Wagonjwa wanapewa magonjwa ambayo hawana ili Zahanati ziuze dawa

DOKEZO Wagonjwa wanapewa magonjwa ambayo hawana ili Zahanati ziuze dawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hili jambo lipo kweli Watz sijui kwanini hawapo HONEST

Ukitaka kupima hospital binafsi unabidi kutafuta kituo ambacho kina ufanisi Sana .
 
Siku nilipoacha kupima Typhoid ndipo nilipopona na sijaumwa tena mpaka leo, hawa jamaa wakitaka tukosane basi waniletee habari za kupima Typhoid!
 
Kwa nchi yetu ilivyo Hilo mbona swala la kawaida sana.

Yaani hii nchi kila sekta Kuna uhuni na upigaji sana
 
Hosptal ni moja tu muhimbili mloganzila.wanapima vizuri wale.hupewi dawa ovyo.na vipimo vyao viko vizuri.
 
Ukitaka uhakika wa vipimo nenda hospitali za mashirika ama serikali,hivi vya watu binafs utatoka na magonjwa kibao na rundo la madawa,kwa mtindo huu AMR ni tishio.
 
Kisa cha pili

Usiku mmoja niliumwa tumbo, asubuhi kulivyokucha tu nikaibukia kwenye kituo cha Afya.

Nikaandikishwa dirishani nikapewa maelekezo kuwa nikamuone daktari chumba fulani.

Daktari akaniuliza kinachonisumbua nikamjibu kuwa ni tumbo pale pale akaniambia hiyo ni Typhoid.

Nikambishia nikamuambia Typhoid haiwezi kuwa kwasababu nina miaka mingi nakunywa treated water na hata vyakula vibicho kama chumbari huwa sili.

Akaniambia hata kama unaepuka njia hizo bado njia za kuweza kupata Typhoid ni nyingi kwa mfano ukawa unakula migahawani.

Nikashangaa kusikia hoja ya aina hiyo kutoka kwa Doctor ikabidi nimuulize hao wadudu wanapenya vipi mpaka wakweza ku survive kwenye chakula ambacho kishakuwa boiled?

Maana yake hata ule ushauri wa kiafya kuwa tunywe maji yaliyo chemshwa basi hauwezi kuwa na impact yeyote kwenye kuzuia wadudu enezi wa Typhoid.

Doctor akaniambia Typhoid unaweza kuipata kwa njia nyingi hata kupitia maji ya chooni unayotumia kutawaza.

Hapo ndio nikabaki mdomo wazi. Akaniambia nenda maabara chumba kinachofuata ukapime.

Nikapima damu, majibu niliyosomewa na Doctor ni kuwa nina vidonda vya tumbo pamoja na Typhoid.

Wakanitajia gharama za dawa kuwa ni 25,000 nikawaambia sawa ila mi kwa saizi sina hiyo hela ila naombeni mnipe hiyo tipoti ya vipimo niondoke nayo ili nikipata hela niende duka la dawa niwaoneshe hiyo report wanipe dawa.

Wakakataa wakaniambia hawatoi ripoti ya vipimo na kama sina hela basi nirudi tu nyumbani nijipange, siku nikapata nitarrjea hapo wanipe hizo dawa.

Sikuridhika na majibu yao ya vipimo hususani ya kuniambia nina Typhoid. Nilipotoka hapo nikaenda kwenye kituo cha Afya Cha Arafa.

Sababu ya kwenda kwenye hicho kituo ni kutokana na kushawishiwa na rafiki yangu kuwa hicho ndio kituo kinachotoa huduma bora kwasababu mke wake alihudiwa hapo.

Kufupisha stori

Niliandikiwa vipimo viwili hapo Arafa

Kipimo cha kwanza kilisema nifanyiwe checkup ya Ultra Sound kuangalia damage ya tumboni

Kipimo cha pili kilikuwa ni damu. Vipimo vyote kwa ujumla niliambiwa nilipie 25,000.

Lakini nilipimwa kipimo kimoja tu ambacho ni cha damu. Hakukuwa na Ultra Sound na wala pesa yangu niliyolipia kwa ajili ya kipimo hicho haikurudishwa.

Nilipofika kwa daktari akaniambia vipimo vimeonesha nina vidonda vya tumbo akaniambia nenda dirisha la dawa

Nilipoenda kwenye dirisha la dawa niliambiwa nilipie 99,000.

Nikasema hiyo hela sina kwa sasa ila naombeni ripoti ya vipimo wakaninyima

Kwa bahati nzuri niliwahi kupiga picha ripoti ya maabara ila ile ya kwa Doctor sikuweza kuipata.

Almost Miezi minne now nimeweza kutibu vidonda vya tumbo kupitia maoni ya wana JF bila kutumia midawa yao ya kausha damu.
Hela walikuàndikia ndefu mno,us
 
je mnaisha mazingira free from malaria exposure ? muda mwingine mnakuwa wajuaji wa vitu vya kitoto , watz wengine wanalala bila neti na mazingira ya nje ni rafiki kwa malaria vectorborn , sisi ni wachafu hatujui kusafisha mifereji jiran inayounda maji yaliyotuama , hatujui kusafisha vichaka vya jiran yetu , tunapenda kurundisha uchafu ndan ya mazingira jiran yetu na bado tunashangaa ddx za malaria , uti na typhoid kuwa nyingi ,TUPENDE KUFANYA RESEARCH KABLA YA KUHUKUMU
Kwahiyo ndio aandike kila mtu ana malaria 1 au 2 ah 3? ,mimi ni lab scientist huwezi kunipanga kizembe hivyo,huo ni unaa na ujuha wa kipuuzi
 
Wee unafikiri zinajiendeshaje wasipofanya hivyo..
Tena unaandikiwa na sindano 5 na kila sindano ni 5000
Mkuu tafuta hela buku 25 sio pesa yakulia ni kubwa, hiyo sindano unachoma buku 5 mnazi mmoja ni 10k,tafuta hela uepukane na fedhea za bei chee
 
T
MKuu naomba niseme wazi kuwa watu kama nyinyi huwa mnanipa hasira sana na ndio mnaipaka Matope Taaluma ya Afya na Udaktari..

Niseme wazi tu Udaktari ni kazi ya Wito isiyo Na faida ni Bora muondoke mkatafute kazi zenye Faida na mtupishe...

Ikiwa kuna Dawa mbadala yenye Uwezo sawa na mgonjwa ana uwezo wa kupata Dawa yenye pesa kidogo kwanini usianze na dawa yenye pesa kidogo??

Mlipokuwa mnafundishwa Kuhusu Cost effectvness mlikuwa wapi? Vyuoni..

Kuwa daktari au kuwa kwenye sector ya afya Haikufanyi wewe kuwa Mungu wa kuamua maisha ya watu..
Ila kunakupa nafasi ya kutatua matatizo ya watu kwa kadri uwezavyo na sio kuyongeza
Tafuta hela hutakuwa na muda wakuhoji gharama za vitu, hakuna kitu aghari duniani, tafuta pesa uzimiliki utanielewa
 
Ujumbe huu ufike Serikalini hasa kwa Wizara ya Afya, sasa hivi baadhi ya vituo vya maabara vinafanya kitu kimoja, ukienda kupima hata kama huna Typhod majibu yao ni una-typhod, unajikuta unatumia dawa huponi.

Ukienda kupima tena bado majibu ni unatyphod, sasa hii ni hatari sana, watu wanakunywa dawa za typhod kumbe hawana changamoto hiyo.

Mimi ilinikuta mpaka nikaenda Mount Meru kupima ndio wakanambia sina typhode nina ‘uric acid’ nyingi sana kwenye mwili.

Nilipofuatilia kwa ndugu na watu wangu wa karibu nimegundua kuwa changamoto za aina hiyo zipo nyingi, zahanati zinafanya vipimo kama biashara ili wahusika waweze kuuza dawa, tena wagonjwa wengi wanauziwa anti biotic ili mradi tu biashara ifanyike, Serikali iangalie hicho kinachoendelea.


Wala wizara haitakusaidia, hii. Nchi pambana mwenyewe, tafuta pesa sana, kuwa makini, usimwamini hata mtume na nabii wala mkeo/mumeo, fanya sala kwa bidii, tafuta tumaini kwa kuweka tegemeo lao kwa Mungu peke yake.
 
Unafikiri serikali na wizara ya afya hawajui, na kwamba unaleta taarifa mpya?
 
Mkuu!
Daktari Bora haangalii Only Efficacy ya Dawa..
Lazma uchague dawa Yenye low side effects plus Cost Effecveness..
Unless utakuwa mfanyabiashara tu..
Lazma ujue unatibu kina nani na wana Uwezo kiasi gani kabla ya kuchagua dawa ya kuwapa
Kama hawana hela wabaki Home, au waende wanakodhani wanafanya charity
 
Back
Top Bottom