DOKEZO Wagonjwa wanapewa magonjwa ambayo hawana ili Zahanati ziuze dawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
unaangalia cost au afya bora ? na hii ndo asili ya mtu mweusi hataki kusimama na kitu kimoja , wenzetu ukiwahudumia hadi raha , twende zahanati za gov km hatujiamini kipesa
Mkuu Huu Ni.mwaka wangu wa 26 nikiwa nafanya kazi idara ya Afya kutoka Daktari wa kawaida mpaka sasa Ni Specialist..

Ninamiliki kituo cha afya Pia..
Najua kila kitu ila Nimezuia kufanya polypharmacy na hata kuandika dawa yenye Bei kubwa na wakati dawa za bei ndogo zipo..
Ukishindwa kuwa Cost effectivesness hiyo inadhihisha Jinsi gani Ulivyo unethical na pia hata Mtu lazma uwe unproffesional kufanya hicho kitu..

Unazungumzia kuhusu Wazungu wa wapi?
Nimefanya kazi kwenye Hospitali za Nje nyingi sana na hakuna huo upuuzi unaoutetea Tena wao wako Very strict kwenye Bei za Dawa na hazitofautiani
 
Duhhhhhh.... Hatarizzzzz
 
unasubir mpk watangaze ITV ndo ujue ipo ? mtu mweusi mvivu kufanya utafit , China mpk leo bado wanapambana na Malaria ww ni nan uiondoe kwa 99%
Wewe ngedere tuanzie hapo kwenye familia yako, mara ya mwisho kukutwa na malaria ni lini?
 
kwann usijipime na kujitibu ? umeenda kwa daktaru ukampangie matibabu ?
Daktari sio Mungu Mtu wala sio kwamba hakosei..
Tena Kizazi cha Sasa hivi cha madaktari cha shule za kata hiki..

Wana very Poor Pt Managements..
Unakuta Mtu kuanzia Dx anafanya Misdiagnosis kibao na wrong dx nyingi..

Wrong au Investigation Chaka.. Hata dawa ni Fikra zake tu ,offbook yaani Tafarani..

Wengi wanaishia Kwenye Magonjwa ambayo huwa nayaita mwisho wa kufikiri kama PID,UTI,URTI..
Magonjwa ya watambuzi wasiofikiri na kufanya uchunguzi wa kina..

Nimewahi kufanya Supervision Hospitali kadhaa za mikoa Ni shida kwakweli na ni AIBU mambo mengine hata kuyasema mbele za layman
 
Haya mambo ni ya kitaalamu..Unatakiwa uanze kwa Daktari, yeye ndo akuandikie ukape hiki na hiki na hiki. Sasa wewe unanyanyuka kwenda moja kwa moja Maabara halafu unafika unawaambia nipime taifodi, nipime malaria. Jilaumu mwenyewe kwanza kabla ya kurudha tuhuma kwa watu.
 
Usinikumbushe kaka!
😀😀
Miaka kadhaa nyuma alikuja Jamaa fulani sjui alikuwa Ni mwalimu wa sayansi shuleni kwake?

Kafika Namuuliza ili anielezee anachoumwa analeta ujuaji mwingi mara ooh nachoumwa nakujua..

We niandikie nikapime Mkojo, Choo,Malaria na Typhod nikajaribu kumuelewesha aniambie shida yake kakazia..
Sasa kipindi hicho nilikuwa kijana wa makamo yeye alikuwa kidogo umri umesonga ikabidi nimkubalie..

Sasa majibu yanakuja Kila kitu hana..
Akaniuliza "Sasa Doctor tunafanyaje.."
Nikamwambia "Kwakweli Sjui labda uniambie nini niandike tena.."
Akaniambia "sasa nitakuwa naumwa nini"
Nikamwambia kwakwli Mimi Sifahamu unachoumwa labda nikuulize wewe?
Yule mzee akaniangalia akaniambia Dr samahani sana..
Nikamwambie enhee sasa kwakuwa umelijua kosa lako.nieleze unasumbuliwa na nini..😀😀
 
Wrong quote bro. Mbona mimi sijazungumzia malaria wala uric acid?
 
kuna siku umeenda kupima ukiwa mzima ? tusipende tu kulalamika wazee , tamaduni zetu tunapima tukiona hatupo vzr kiafya Je unategemea uambiwe mzm
Ndio kuna dispensary ukienda huko si UTI au mkojo mchafu
 
kuna siku umeenda kupima ukiwa mzima ? tusipende tu kulalamika wazee , tamaduni zetu tunapima tukiona hatupo vzr kiafya Je unategemea uambiwe mzm
Unacoment kinegative sana mkuu, nakupongeza kama wewe huwa unafuata utaratibu kuhudumia wagonjwa na hubambikii ili wanunue ni jambo jema ,

Sasa na wewe usione hilo tatizo la wahudumu kufanya hayo halipo jaribu kwenda vituo viwili au tatu vidogo(dispensary) binafsi uone ni kweli au watu wanasingizia
 
Mimi kitu ambacho sina taaluma nacho mfano afya huwa sina pingamizi , namsikiliza mtoa huduma otherwise labda anioneshe. Signs ambazo si sahihi . Ujuaji sehemu ambayo hujui kitu unaweza Kutana na mtu anakisirani 🤣 upewe dawa hazieleweki
 
Typhoid na UTI ni magonjwa ambayo most of health laboratory attendant wanayakuza sana kuonesha ukubwa wa tatizo wakati ukweli ni kwamba wanakuwa wameelekeza nguvu kwenye uuzaji wa dawa
 
Haya mambo ya Kila nikienda hospital Nina U.T.I ndo yalifanyaga nisiende kwenye "hospital za mama" mpaka pale watakapobadilika....
 
💯 True huu Ni ukweli Mchungu
Shida kubwa kwenye kipimo kilichozoeleka cha urine dipstick ni mpimaji mwenyewe huenda ni colour blind hivyo anashindwa ku compare colours anaishia kusema mtu ana UTI.

Shida ya pili huenda mgonjwa kipindi analeta sample alikuwa hajala muda mrefu hivyo ukipima unakuta ketones zimepanda japo leucocyte zipo normal anaandikiwa madawa.


Kingine sample imekaa muda mrefu kwa hiyo rangi kwenye zile strips zinachange mwisho wa siku anaambiwa ana UTI.

Kwa hiyo hapa shida sio kwa daktari shida ipo kwa lab technician kutokuwa competent anapelekea daktari kupata wrong ddx.
 
Safi Sana mkuu kusema ukweli, ambao wengi tunauficha!

Kuongezea hata wanaotumia machine za urine analyser machine hazioshwi kwa kila sample na mda mwingi inapelekea majibu kufanana..
Na hata kwa microspy Vile vile kwa wanaopima sediments....

Japo ukiniuliza Mimi kati ya kipimo cha mkojo nachokubali Accuracy kati ya dipstics na Urine sediments nitakujibu Bora sediments..

Handling ya Dipsticks Iko poor Hata upimaji wake poor wengi wanaopima Ni Untrained Personell..

Utunzaji wa Dipsticks hata sample zinavyokuwa collected mpaka Kupimwa Obvious lazma ukute Leococytes na makorokoro mengine..

Kimbembe kipo kwenye utambuzi wa Majibu (Interpretation) hapa ndo unaweza kucheka..
Madaktari wa sasa sijui wanasoma wapi au wanajifunza wapi?

Unakuwa Urobirinojen zimesoma nyingi ila vipimo vingine viko normal Mtu anaambiwa ana UTI anaandikiwa Dawa..
Ketones Ziko nyingi anapigwa antibiotics..

Yaani sijui kama walisoma hata Micro na clinical Lab.. Ni tabu kwaweli ni Aibu ukienda kukagua na kufanya Supervision unaweza ukatamani kumtandika vibao Mtoto wa Mtu lakini ukaona bora umuache tu..

Kamuandikia Mgonjwa Dawa za kutosha Cefotaxine 1g BD kwa siku 7 kisa ketones kupitia Faili la mgonjwa ni DM cases unasema sasa huyu Alipita Hata Internship kweli?

NA alipataje kuwa daktari..

Asiyejua hata Alitakiwa afanye nini baada ya kuona Ketone kwa mtu aliye na DM na akamuacha anaenda nyumbani huu si uuaji kabisa?

VItu vingine kwa Layman huwa ni normal ila kwa mtu unayejua huea vinatia hasira sana kuvitazama
 
Vituo vya afya ubabaishaji mwingi,tumeshuhudia wengi wakipoteza maisha kwa kukosa huduma muda muafaka,madaktari wako bize na miradi yao ya afya,pia unaandikiwa dawa za kwenda kununua duka la dawa tena kwa kulengeshewa duka fulani.
Vituo vya afya unaishia kupewa dawa ambazo ni common ambazo hata majumbani mwetu akiba tunazo. Unamshawishije mgonjwa aende vituo vya matibabu vya serikali hapo?
 
Kuhusu Dawa na Level za Dawa nimeshaandika Ufafanuzi soma Comment #18
 
Kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…