Wahadhiri kuomba kuongezewa muda wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 70

Wahadhiri kuomba kuongezewa muda wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 70

Magu aliwaongezea hadi 65, lakini bado wanaona hiyo haitoshi.

Kuongezewa muda hadi 70 wengi watakufa kabla ya kufikia umri huo. Na hii itakuwa na madhara kwa familia zao, na hasa kuhusu mafao yao
Mimi nawashauri wastaafu na miaka 60 ili walambe mafao yao, baada ya hapo waombe mkataba wa miaka miwili miwili ambao utaamuliwa na tathmini ya uhitaji wa huyo mhadhiri ikiwa hajapatikana mtu wa kujaza nafasi yake au mchango wake kwenye eneo la taaluma na utafiti bado unahitajika, vinginevyo unaweza kujikuta umejaza wahadhiri wanaochapa tu usingizi maofisini kutokana na kuelemewa na uzee........maana kazi ya kufundisha na kufanya tafiti inahitaji energy kubwa sana ya mwili na akili.​
 
Mtaani kugumu wanaogopa kuja kunywa sungura?
hahaha kuna mmoja alistaafu pale UDOM hata nyumba hana akaishia kukaa hotelini huku anajenga mpunga ukakata akahamia guest za 50, 30, 20, 10,,,, mpaka akashindwa kulipa akapewa kauchochoro alale hapo
ALIJIFIA NI KINGEREZA CHAKE
Acha masikhara kwenye Mambo serious
 
Waongezewe angalau wafike miaka 65, miaka 60 ni chini sana kwa Tanzania ya sasa. Nasikia majaji ni miaka 65 kwanini isiwe kwa waalimu wa vyuo vikuu na.....
Hata wahadhiri Kuanzia ngazi ya waandamizi(Senior Lecturer) wao ku-retire ni 65years
 
Watakuja wengi kujitetea maana akili za utu zinawajia wakiwa 60 yrs wakianza kutepeta, wenye elimu wamejaa sana, ni upuuzi tu kuwafanya viwete wasioweza kazi zingine, watoke wakaishi taaluma zao kwa vitendo huko nje.

Watu muhimu ni hao medical doctors hao wengine wakafanye kazi zingine.
Hata medical doctors nao wapishe nafasi,wakapambanie maujuzi yao nje ya mfumo wa ajira.Kuna vijana wengi wamemaliza vyuo hawana ajira,watumikie taaluma zao wapate uzoefu.
Miaka 60 iwe ukomo wa ajira zote serikalini.
 
Je, mhadhiri wa chuo ufanisi wake kikazi hauna kikomo?
Tofauti iliyopo kati ya ELIMU na vitu vingine vyote hapa duniani ni kwamba kadri unavyozidi kuitumia elimu, ndiyo kadri inavyozidi kuongezeka. Tofauti na elimu, kadri unavyozidi kuvitumia vitu vingine vyote, ndiyo kadri vinavyozidi kupungua, au kupunguza thamani, assuming siyo perishables

Mimi nina imani kubwa sana kwamba wahadhiri makini zaidi ni pamoja na hawa walio kwenye umri wa miaka 60-70; na ndiyo wanaoweza kuwa na impact kubwa zaidi kwenye UFUNDISHAJI wa watoto darasani, na possibly, kwenye UTAFITI japo kwenye hili la UTAFITI siwezi kuwa na uhakika zaidi kwa sababu ya umri wao

The fact is, mtu akishavuka umri wa miaka 60, hafanyi tena kazi za kutafuta mali , na hivyo anakuwa ANAFANYA KAZI KWA MOYO kwa sababu malengo yake alishatimiza tayari. Kama hakufanikiwa kuwa tajiri, basi hawezi tena kuwa tajiri, na kama alibahatika kuwa tajri, basi tayari ni tajiri na hatakuwa na haja ya kuanza kuhangaika kuongeza utajiri mwingine tena

Sema tu nchi yetu watu tulio wengi mawazo yetu yamepinda tunafikiria vitu ambavyo viko kinyume na malengo ya nchi, ila assuming mpango huu unafanikiwa na ukaangukia kwenye mikono ya watu sahihi, ni mpango mmoja wa maana sana

Hiki kitu mimi nilishawahi kukiongelea kwa mara ya kwanza, mwaka 2006 nilipokuwa ofisini kwa Prof. Mgaya, kipindi alipokuwa bado ni DVC Administration pale UDSM
 
Hata medical doctors nao wapishe nafasi,wakapambanie maujuzi yao nje ya mfumo wa ajira.Kuna vijana wengi wamemaliza vyuo hawana ajira,watumikie taaluma zao wapate uzoefu.
Miaka 60 iwe ukomo wa ajira zote serikalini.
Dhana yangu ni panapo uhitaji tuweke priority halisia, doctors na watalamu wa molecular science, na sisi wachumi na watu wa masoko taifa bado changa tupewe umuhimu.
 
huku ni kuwazuia vijana nafasi za kuajiriwa.

nashauri umri wa kustaafu urekebishwe uwe miaka 50 HIARI na Miaka 55 lazima, hii itasaidia sana vijana nguvu mpya kuingia kazini.

unakuta mtu kazeeka kibabu hata nguvu ya kupambana hana lakini bado wamekalia nafasi.
 
Dhana yangu ni panapo uhitaji tuweke priority halisia, doctors na watalamu wa molecular science, na sisi wachumi na watu wa masoko taifa bado changa tupewe umuhimu.
Nakubaliana na wewe,ila kwa umuhimu wao/wenu baada ya miaka 60, wangekuwa kama consultant ingesaidia zaidi vijana kukuza uzoefu wao,kuliko wazee kubakia kwenye ajira.
Ni mtazamo wangu
 
Nakubaliana na wewe,ila kwa umihimu wao/wenu baada ya miaka 60,wangukuwa kama consultant ingesaidia zaidi vijana kukuza uzoefu wao,kuliko wazee kubakia kwenye ajira.
Ni mtazamo wangu
Mimi ni mjasiliamali tu nimewasemea walimu wangu wa uchumi na masoko ni muhimu sana maana nafanya nao kazi hawa watu, I have had cases where a I normally bring in cases of merging or bridging the public band private sector initiative with the aim of simultaneous growth and development in all dimensions.
 
Ujue Unapo ajiliwa huwa Mwajili ana nunua muda wako, na si vinginevyo, wala sio ujuzi wako hapana bali ni muda,
Acha kuwa unaongea mambo kama hujaenda shule. Kilichokufanya wewe ukaenda shule ni nini? Kuna mtu ambaye huwa yupo halafu hana muda? Wangapi wapo wanao muda na wanautumia kutembea mtaani hawana kazi, wakati wangependa kuwa mahali fulani wanafanya kazi? Msiwe mnavamina hoja ambazo haujui utachangia nini!
 
Dhana yangu ni panapo uhitaji tuweke priority halisia, doctors na watalamu wa molecular science, na sisi wachumi na watu wa masoko taifa bado changa tupewe umuhimu.
Huo uchumi wenu wa kutoza tozo juu ya tozo umuhimu wake ni upi? Nyie ndiyo mnatakiwa mstaafu na miaka 50 mkaanzishe biashara na nyie mjue madhara ya tozo na kodi holela
 
Mimi nashauri umri ushushwe mpaka 50 kama hawawezi kukuza vijana wengi wa kushika nafasi zao basi hawatufai ni bora kabisa kama wasingeajiriwa
 
Ufaransa, watu waliandamana, kupinga serikali, kuongeza muda wa kustaafu kutoka 60 kwenda 62! Raia wakasema hawataki huo ujinga, wamejiandaa kustaafu at 60, waendelee na maisha yao! Huku kwetu, watu wanaogopa kustaafu, wanaona bora waongezewe muda! Sababu zipo wazi, kwa wenzetu huduma na mifuko ya hifadhi ya jamii inafanya kazi. Ukiwa senior citizen umestaafu, kiinua mgongo chako kipo wazi, unakipata bila rongorongo. Pensheni ndio taaamu kabisa, unarudi zako huko na unaanzisha kashughuli au unaenda vacation mbugani, pesa inaingia!! Hapo lazima hutahofu kustaafu. Huku kwetu kwanza umekuwa unalipwa mshahara mbuzi, kiinua mgongo. Serikali imeishakikata panga, pensheni ni ya kuunga unga!

Unapostaafu, bado kuna juniors wapo first year, mkopo hakuna, lazima udate! Hata genge la kuingiza shilingi mia halipo! Hutafurahia kustaafu! Wanaostaafu kwa raha, chukulia mawaziri wakuu wastaafu, analipwa 80%, anavuta mkwanja mrefu.
 
Nimemsoma mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania, OUT akimuomba makamu wa Rais, Mh Mpango awaongezee wahadhiri wa vyuo vikuu muda wa kustaafu Kutoka miaka 60 ya sasa hadi miaka 70.

Kwa kuwa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kuna faida yoyote kuwaongezea umri wa kustaafu wahadhiri hao?

Ni yapi madhara ya kuwaongezea umri wa kustaafu na upatikanaji wa ajira za kada hiyo katika vyuo vya Serikali?

Je, mhadhiri wa chuo ufanisi wake kikazi hauna kikomo?

Kuna madhara gani ya kuwaongezea muda wa kustaafu na kuwaacha kada nyingine wakistaafu at 60?
Hawa wapumbavu kila siku wanasema vijana wajiajiri lakini wao hawataki kustaafu na mitaji wanayo, kwanini asiombe umri wa kustaafu upungue mpk miaka 50?
 
Kama ana nguvu kiafya mhadhiri aendelee na kazi tu hata miaka 80

Hii kazi inataka sana uzoefu na experience za muda mrefu kwenye kusoma research nk
 
Back
Top Bottom