Wahadhiri kuomba kuongezewa muda wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 70

Wahadhiri kuomba kuongezewa muda wa kustaafu kutoka miaka 60 hadi 70

Nimemsoma mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania, OUT akimuomba makamu wa Rais, Mh Mpango awaongezee wahadhiri wa vyuo vikuu muda wa kustaafu Kutoka miaka 60 ya sasa hadi miaka 70.

Kwa kuwa umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, kuna faida yoyote kuwaongezea umri wa kustaafu wahadhiri hao?

Ni yapi madhara ya kuwaongezea umri wa kustaafu na upatikanaji wa ajira za kada hiyo katika vyuo vya Serikali?

Je, mhadhiri wa chuo ufanisi wake kikazi hauna kikomo?

Kuna madhara gani ya kuwaongezea muda wa kustaafu na kuwaacha kada nyingine wakistaafu at 60?
TAFSIRI YA VIJANA TAIFA LA KESHO HAITATIMIA KAMA MTU ANA MIAKA 60 BADO ANAOMBA MINGINE 10
 
Back
Top Bottom