PostGE2025 Wahadhiri wa Kiislam: TEC wanapotoa matamko kuhusu utekaji & mauaji awamu ya Samia, kwanini hawakuyatoa wakati wanaongoza marais wasio waislam?

PostGE2025 Wahadhiri wa Kiislam: TEC wanapotoa matamko kuhusu utekaji & mauaji awamu ya Samia, kwanini hawakuyatoa wakati wanaongoza marais wasio waislam?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wamefeli big time tumeoleana na kuzaliana kati ya Islam na Christian.
Waje na spana nyingine icho kichaka hakina maajabu.

Tunataka
Katiba
Tume huru ya uchaguzi
Kuachia wafungwa wote wa kisiasa
Samia atuachie nchi hii ngoma ngumu kwake.
Wanaotaka Kutugawa Kidini wamtafute kazi nyingine
 
Vita ya dini inaenda kuwa kubwa sana kutokana na akili ndogo za wanaotumwa kuwashambulia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Katika matamko yote ya TEC, hawajawahi kuitaja au kushambulia dini yoyote, sasa hawa BAKWATA na wengine hawawezi kuzungumza yao bila kuishambulia TEC.

Nitarudi na ushahidi kuonesha kuwa TEC hata wakati wa viongozi wa Kikatoliki walikuwa wakitoa matamko kulaani mabaya yanayoendelea nchini.

Kuna mpango michafu unasukwa hapa!
 
Rais, wakuu wa hii serikali japo ni dhalimu, viongozi wote wanatakiwa kuwa wa kwanza kukemea vitendo kauli kama hizi za uchochezi na polisi kuwaita watoe ushahidi zaidi na kupewa onto.

Wanalipoteza Taifa japo kwa visenti vichache. Tumezoea kuishi pamoja tukianza kuwindana huku mitaani tutapotea.
 
Hawa jamaa wanatuaibisha sana waislamu. Hao TEC hata wakati wa Magufuli ni mwenzao kabisa ila walimkosoa kila mara hata kuna uzi humu wa waraka wa TEC wakati wa marehemu Magufuli.

Jamaa wanatuaibisha sana basi tu.
Ni wakati wa Magufuli rais wa TEC wa wakati huo Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Ngara (kama sijakosea) alitengenezewa mpaka zengwe la kuambiwa siyo raia wa Tanzania! Na hati yake ya kusafiria ilishikiliwa na uhamiaji.

Sababu ilikuwa ni kutoa matamko ya kuikosoa serikali ya kidikteta! Sasa hao wanazuoni wanavyoamua kujitoa ufahamu, lengo ni kumfurahisha nani?

Au wanataka kusema hakuna utekaji na mauaji ya raia nchini? Hata ningekuwa mimi Muislam ninayejitambua, hakika ningesimama kwenye haki badala ya kumlinda mhalifu kwa sababu tu ya dini yake!
 
Naona hapa tunaenda kuhama kutoka kwenye matukio muhime na agenda za kitaifa kuhamia kwenye Udini, kila mtu atasupport dini yake nomatter its right or wrong.....tatixo ni wakatoliki wanao jifanya kuongoza madamano ya wanaishi TEC kaeni pembeni watu wafanye revolution bila udini.
Mnazingua sana kuwahusisha TEC na madudu ya serikali! Serikali ndiyo inayoteka, kufunga na kuua wakosoaji wake! Serikali ndiyo inayofanya matendo ya ufisadi na dhuluma! Sasa TEC inapokosoa, nyinyi mnaleta nongwa, kisa Rais ni Muislam mwenzenu!

Mbona Magufuli enzi za utawala wake alipingwa na watu wa dini zote, na hatukusikia habari za aina hii? Lissu alishambuliwa kwa sababu ya kuukosoa utawala wake! Je, alikuwa ni muislam?
 
Vita ya dini inaenda kuwa kubwa sana kutokana na akili ndogo za wanaotumwa kuwashambulia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Katika matamko yote ya TEC, hawajawahi kuitaja au kushambulia dini yoyote, sasa hawa BAKWATA na wengine hawawezi kuzungumza yao bila kuishambulia TEC.

Nitarudi na ushahidi kuonesha kuwa TEC hata wakati wa viongozi wa Kikatoliki walikuwa wakitoa matamko kulaani mabaya yanayoendelea nchini.

Sisiem wanachokifanya kwa kujihalalishia kuendelea kutawala tanganyika kitawatafuna siku za some. Waziri wa Mambo ya Nje wa Dubai, UAE 2017 aliwaambia nchi za Magh'aribi kuwa NYINYI MNAJIFANYA MNAUJUA UISLAM KUPITA SISI WA NCHI ZA KIARABU? mnawakaribisha Maislamists ambao sisi tumewapiga marufuku!? Basi mjue iko siku inakuja Magaidi wa Itikadi Kali ya Uislamu ngome zao zitakuwa nchini mwenu. Msichojua ni kuwa Uislamu Umeingiliwa na Maislamists wanaofadhiliwa na Muslim Brotherhood.
Kule Sudan, Serikali ya Elbashir kwa raha zake iliwafadhili Jamii ya Waislam wenye Asili ya Uarabu katika Jimbo la Darfuu ( Janjaweed) ili kuzima harakati za wananchi wa Darfuu za kupinga ukandamizaji wa serikali kwa wananchi hao. Walifanikiwa na baadae wakawajumuisha Janjaweed hao kama sehemu ya Jeshi la Sudan. Ambacho hawakujua ni kuwa Janjaweed hao na itikadi zao kali za kiislam walikuwa na malengo yao. Matokeo yake kukawa na Jeshi ndani ya Jeshi la Sudan-RSF linaloongozwa na Muhammad Hamdan Dagalo Musa. Matokeo yake ni vita inayoendelea sasa ya majeshi mawili.
Kinachokuja tokea Tanzania.
Kweli ccm mtafanikiwa kuwapaka matope TEC na kuwanyamazisha watanganyika waliowengi. Msichojua ni kuwa hao mnaowatumia siyo waislam wa kweli kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE 🇦🇪 bali ni Maislamists waliouvamia Uislamu. Wana Agenda zao ambazo zinatofautiana na Genge la Muslim Brotherhood ndani ya ccm. Islamists huwa hawana ushirika na serikali za kidunia. Pia waulizeni Saudi Arabia ambao baada ya kuona mafanikio ya mapinduzi ya Iran (Shia) na wao wakataka kukumbatia Wahabbi.
Mnatengeneza Boko Haramu na Alshabab nchini mwetu.
 
Aliyepaswa kujibu ule waraka wa TEC ni Serikali, na hakuna mahali TEC wameongelea Bakwata au dini fulani.

Sijui hawa jamaa wamekula maharage ya wapi?

Watu tunapinga vitendo vya utekaji na kuua bila kuangalia imani zetu ni vizuri wangejiridhisha kwanza kabla ya kuja na mambo yao.
 
Back
Top Bottom