Wahariri wa magazeti wapigwa na kitu kizito vichwani kuhusu DP World

Wahariri wa magazeti wapigwa na kitu kizito vichwani kuhusu DP World

Sasa kauli yake haieleweki imesimama wapi kiasi kwamba Chawa wote wamejipa kazi ya kumsaidia Madam President kujibu waraka huku wengine wakianza mpaka kuchambana
Ni kweli Kauli ya Rais haionesho yuko upande gani.

Inaonekana na Yeye yuko Dilemma
 
La Badari limeisha ndugu zangu.

Rais alijipa muda wa kutosha kupokea maoni na kayapokea kweli kweli maoni yetu kwa hisia na style tofauti

sasa hivi tumpe muda wa kuyachakata na hatimae kufanya maamuzi kwa maslahi ya Nchi yetu
"La Bandari limeisha..."?

Utakuwa unaishi dunia ya kipekee wewe, siyo hapa Tanzania.
Au pengine unajipa moyo tu na matumaini yasiyokuwepo.

Huyo Samia hana uamzi zaidi ya kufuata amri tu sasa. Hiyo DP World haiendi popote ndani ya nchi hii.
 
The end will justify the means...acha tuone!
1. Binafsi sitakaa kuamini kuna mkataba toka nje utainufaisha nchi hii mingi ina negotiations trap ambazo wameweka wenyewe inakuwa ngumu kutengua bila fidia kubwa pindi wakivurunda, bahati mbaya sana hatupendi mikataba yenye partnership tunapenda aje achume atumegee anachopata kiwe kidogo au cha kati sisi hewala tu vinono wanakula wao, sehemu kubwa ya mikataba iliyopita ina matatizo mengi sana reason behind kuna rushwa nyuma watu walilamba bora liende, mingi ni mikataba ya mfano wa kina Chief Mangungo & Mangi Meri & Marealle ina ulaghai nyuma yake...nchi inalipa madeni tele pindi wakiitengua lakini waliokuwa kwenye panel husika iliyoingia mkataba wapo wanadunda tu wameshajilia ganji kuona 10%
Hivi huu mkataba sijasikia expire date yake au ni Indefinite contracts, kwani wa Ticts walisema hata nyongeza waliyowapa waliitangaza?

2. Ishu ya usimamizi wa bandari kuwa sio mzuri kiutendaji it means serikali yenyewe imeshindwa kuwawajibisha utawala/uongozi ambao wao ndio wameuweka/teua na kuubariki pale, how comes sehemu ambayo ina watu wa idara ya usalama wa taifa wakiitazama 24/7 inakuwaje chini kiutendaji na ujanja ujanja chini ya uangalizi wa watu ambao wanaripoti moja kwa moja kwa Boss lady haiingii akilini?!

3. Kama shida maadili wange reform sheria wateue mgeni awe mkurugenzi iwe mzungu au mhindi apewe target tu huku akiongoza management pale, just for three years waone impact yake, kwasababu wazigua wenzetu si wanavurunda kila wakiteuliwa miyeyusho daily. Nmb hiyo hapo ili yumbayumba mwanamama yule mzungu kaiweka relini leo hii imerudi kwa mswahili trust me ni swala la muda tu itarudi kulekule siombei iwe hivyo, wenzetu wana maadili sana sisi sijui tunakwama wapi kusimamia ni wachache sana wenye kusimamia taasisi zikawa imara, leo hii Boss lady analalamika mashirika & taasisi za serikali zinakula tu ruzuku hazizalishi cha ajabu viongozi wake ni wateuliwa wanaotokana na vetting ya usalama wakijiridhisha wanapeleka jina sasa kama wanavurunda ina maana vetting yao sio nzuri kuna haja ya kujitathimini kisha warekebishe ili wapatikane watu sahihi na makini kuendesha taasisi husika otherwise yatakuwa yaleyale unamtoa Abdallah unamteua dullah.

Mwisho: Na ikawe kheri kwenye mkataba huu uwe wa mfano wa kuigwa na wa haki pasipo kuwa na ganji kuona nyuma yake kwasababu mkataba ukiwa na ganji kuona nyuma yake hautakosa matatizo mbeleni bahati mbaya sana matatizo yakianza wahusika wanakuwa hawapo tena madarakani blunder zilizofanyika anabeba mtawala mwingine.
 
La Badari limeisha ndugu zangu.

Rais alijipa muda wa kutosha kupokea maoni na kayapokea kweli kweli maoni yetu kwa hisia na style tofauti

sasa hivi tumpe muda wa kuyachakata na hatimae kufanya maamuzi kwa maslahi ya Nchi yetu
Limeisha hapo Lumumba,kwa Wananchi halijaisha.
 
Kuna watu wanatafuta kwenda kuishi uhamishoni kwa nguvu.

Pengine hawajali kwani walishajiwekea ukwasi (visenti)wa ajabu huko ughaibuni.

Lakini kama wamesahau niwakumbushe. Marehemu Sani Abacha alijilimbikizia mihela lakini kwa sheria za kidunia za sasa pesa zote alizokwiba au kupata kijanja zilirudishwa na akafa kwa kihoro!

"USIMUAMSHE ALIYELALA, AKIAMKA"
Kila ubaya utalipwa
 
Hivi petro magoti kazi yake ni nini ikulu? Nimeanza kumuona toka enzi za shujaa! Anayejua tafadhali

Huyo ndio mshauri wa rais kwenye masuala ya siasa na chama,ukisika mkeka umetoka huyo ndio approval,ndio link ya wanaccm na serikali. Ukiachana na hoja za poison master[emoji28]
 
Ndugu zangu,

Sasa ni dhahiri kuwa sakata la 'Port Selling" inachukua mkondo mpya. Kauli ya kibabe na kiburi ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu ubavu na misuli imeanza kutafsiriwa na "ofisi nyeti" kwa vitendo.

Kutoka kuwa mjadala Sasa sakata hili linaanza kuelekezwa kwenye mkono wa chuma. Ni kama utawala wa Mwendazake unaanza kufanyiwa majaribio tena. Toka sasa tegemeeni mabaya zaidi ya Magufuli maana mmeshanywea.

Leo tarehe 25/8/2023 hakuna gazeti la main stream lolote lililoandika habari ya Bandari na DP World. Lililojaribu basi habari hiyo nzito ya nchi imepewa uzito mdogo, tena kurasa za ndani.

Taarifa kutoka ndani ya vyombo hivyo vinadai kwamba Wahariri wametishwa na kusmbiwa, "achaneni na habari za Bandari imetosha". Wapo waandishi wengi waliopeleka habari za Bandari lakini Cha ajabu zote na kote hazikutoka leo.

Inaelezwa kwamba sliyesimamia hiyo show ni Nape Nnauye akipewa maelekezo kutoka kwa mtu mmoja wa karibu sana na Samia (mtu mfupi sana aliyeoa mwanamke mrefu na harusi yake ikatrendi sana).

My take: Kimbilio pekee ni JamiiForums. Kwa niaba ya wanajamii wote humu naomba mmiliki wa JF simama na wananchi maana hata redio za kijamii zimetishwa. Tulipofikia Sasa ni ubavu na misuli ya "muuzaji" wa nchi.

Yesu akiteswa alisema, "msinililie mimi, jililieni ninyi na watoto wenu", tumekwisha. Mex Mello Mungu akulinde unapotulinda. Never give up!
a failed mission
 
Limeisha hapo Lumumba,kwa Wananchi halijaisha.
Limeisha kwa Rais kuanza mchakato wa kuamua

kujadili haina deadline kwani hadi sasa tunajadili royal tour kwa kupanda wakati juzi Askofu Bagonza kwa mara ya kwanza Amekiri hadharan Matunda ya royal tour kwa jinsi watalii wanavyomwagika

hata JPM alipondwa kwa kukataa kupiga lockdown Nchi lakini baadae tukajifaharisha kwa ujasiri ule

nakukumbusha hata Mzee Mkapa alipoanzisha mchakato wa kuanzisha NHIF alipingwa sana wazo hilo lakini leo hii tunamkumbuka kwa hilo

hata ukiwaambia masikini na mafukara pangeni foleni mje niwape sehemu ya mshahara wangu usidhani wote watafanana. mawazo kwa uamuzi wako huo

Hakuna mabadiliko chanya yasiyopingwa Duniani

kasome historia ya China wakati wa Chairman Mao alivyokumbana na Upinzani wakati wa Reforms za kuipata china ya sasa

Waliomshambulia JPM kwa kukataa Wawekezaji wa nje ndio hao hao wanamshambulia Samia kwa kukaribisha Wawekezaji wa nje
 
Wazuie tu, Kuna waandishi wengi tu kwenye mitandaoya jamii kama jf, huko hawahitaji wahariri, watajiandikia tu ili mradi ujumbe ufike kwa walengwa..
 
Nape yupo sahihi!!

Walikula Dola 100,000 za Mwarabu kila mhariri. Sasa wanataka tena kukiuka makubaliano?
Au wanadhani Mwarabu atatoa zingine tena? Watulie
Dah!.
 
Ndugu zangu,

Sasa ni dhahiri kuwa sakata la 'Port Selling" inachukua mkondo mpya. Kauli ya kibabe na kiburi ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu ubavu na misuli imeanza kutafsiriwa na "ofisi nyeti" kwa vitendo.

Kutoka kuwa mjadala Sasa sakata hili linaanza kuelekezwa kwenye mkono wa chuma. Ni kama utawala wa Mwendazake unaanza kufanyiwa majaribio tena. Toka sasa tegemeeni mabaya zaidi ya Magufuli maana mmeshanywea.

Leo tarehe 25/8/2023 hakuna gazeti la main stream lolote lililoandika habari ya Bandari na DP World. Lililojaribu basi habari hiyo nzito ya nchi imepewa uzito mdogo, tena kurasa za ndani.

Taarifa kutoka ndani ya vyombo hivyo vinadai kwamba Wahariri wametishwa na kusmbiwa, "achaneni na habari za Bandari imetosha". Wapo waandishi wengi waliopeleka habari za Bandari lakini Cha ajabu zote na kote hazikutoka leo.

Inaelezwa kwamba sliyesimamia hiyo show ni Nape Nnauye akipewa maelekezo kutoka kwa mtu mmoja wa karibu sana na Samia (mtu mfupi sana aliyeoa mwanamke mrefu na harusi yake ikatrendi sana).

My take: Kimbilio pekee ni JamiiForums. Kwa niaba ya wanajamii wote humu naomba mmiliki wa JF simama na wananchi maana hata redio za kijamii zimetishwa. Tulipofikia Sasa ni ubavu na misuli ya "muuzaji" wa nchi.

Yesu akiteswa alisema, "msinililie mimi, jililieni ninyi na watoto wenu", tumekwisha. Mex Mello Mungu akulinde unapotulinda. Never give up!
Hiyo tabia ya kuifanya nchi ni mali ya familia mwisho wake upo karibu sana. Watanzania hawarudia kuchagua watu wa aina hiyo kuwa viongozi wao.
 
Back
Top Bottom