Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Haha, sasa sijui lengo la kuzima lilikuwa wafanyakazi wa kalale?

Mimi hadi leo ninayo kanda ya Jangalason nimetape baadhi ya vipindi.

Na tulishapigana na kaka yangu sababu ya kutape kanda zake hadi nikamchoma Kisu cha mguu.
Japo nilikuwa Mdogo lakin nakumbuka yote nimecheka sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani
Pale [HASHTAG]#Mambo[/HASHTAG] yote tisa 10 zinduka
Nilikuwa sipitwi
 
"Tuache kazi ya miradi tutakula kwako" ene ujangili magendo na rushwa dini" MZEE Mwinamila akiburudisha katikati ya kipindi cha Mikingamo

Kuna mwaka Mei Mosi ilifanyika Shinyanga basi Kulikuwa na kibwagizo kinaimbwa kuelekea siku hiyo. Wasukuma sahihisheni nilipokosea....

"Utakwilima....Bana ba Shinyanga mwaka ugu ba shile kabisa. Ukulima gwa kisasa gwaleni gwangazile gwange kuyupa ni mbolela mala ku ga beche,
 
Huyu mzee namkumbuka sana,nakumbuka mzee julius alimjengea nyumba pale dodoma, kuna nyimbo alikuwa anaimba zilitumika redioni wakati huo kama huu
"msukosuko wa wimbi maji yanapoingia.......huko mbele nimesahau
Mwingine ni huu
"kuleni kuku mayai na kuujenga mwili pakulala pawe bora....mbele nimesahau malizia mkongwe,kuna mwengine anasema "dereva kalewa gongo aah hiyo si sawa dereva acha vituko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwa RSA siyo Moses Mkandawile bali ni Duncan Kandawile na wenzake Francis Chandiona, William Joranji na Boston Caleja Kaunda.
 
Kuna mtangazaji Lenard Mtawa nasikia alifariki. Bujaga Izengo Kadago nikasikia ni afisa uhusiano na masoko pale SUA. Wengine kama Mohammed Kisengo na Nyambona Masamba sijui wako wapi hao siku hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…