Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Uje tena shangazi, shangazi shangazi enhe! Mchana utasikia wimbo ule hivi sasa ni lunch time... Na mwisho wa mwezi kulikuwa na wimbo wake wa kasim kama hana pesa nyumbani hatoki......!
Umenikumbusha mbali sana. Nilipenda sana kusikiliza huo wimbo wa Lunch Time uliotungwa na kuimbwa na mwanamuziki wa Kenya aitwae Gabriel Omolo Aginga (Mr. Lunch Time). Ni bahati mbaya sana kwamba huyu mzee alifariki mwanzoni mwa mwaka huu. Huo wa Kassim ni wa Orchestra Mlimani Park. Ni kupitia vipindi kama hivyo vya RTD tuliweza kupata nafasi ya kusikiliza kwa wingi nyimbo za wanamuziki wa Tanzania na majirani zetu hususani Kenya na wale wa Zaire (kwa sasa DRC).
 
Pwagu na Pwaguzi.
 
Hiki niwe mkweli sikuwahi kukisikia ila majina nilikuwa nayasikia
Hivi kipindi cha Mahoka na Pwagu na Pwaguzi vilikuwa ni vipindi viwili tofauti au Mahoka ndiyo lilikuwa jina la kipindi huku Pwagu na Pwaguzi wakiwa ndiyo waigizaji wake?
 

Mimi hunitoi hapo kipindi cha BP chini yake marehemu Uncle J.Nyaisanga.Huyuhuyu aliendesha Bwana chai kama sikosei.Kumbuka, vipindi vingi vilikuwa na break, mnakula ngoma moja hivi mnaendelea.

Usisahau Malenga wetu.Unakula mistari na vina toka kwa wazee wa Kilwa na Rufiji.Nimemsahau yule aliyekuwa akighani mashairi. Usisahau vipindi kama NASACO! SUKITA, T.E.S

Hiyo T.E.S(shirika la ugavi wa vifaa vya elimu) basi tangazo lao lilikuwa kitu kama hivi:

A:Aaah!una kalamu nzuri, umeipata wapi?

B: T.E.S

A: Na wino?

B: T.E.S

Yani ilikuwa burdaaaaaaaaaani.

Usisahau tulikuwa na idhaa mbili, taifa na biashara

Asante
 
Hivi kipindi cha Mahoka na Pwagu na Pwaguzi vilikuwa ni vipindi viwili tofauti au Mahoka ndiyo lilikuwa jina la kipindi huku Pwagu na Pwaguzi wakiwa ndiyo waigizaji wake?
Sijui boss sijawahi kuwasikia hao pwagu na pwaguzi wakiigiza pengine wakati huo mzee alikuwa hajanunua redio
 
Hivi kipindi cha Mahoka na Pwagu na Pwaguzi vilikuwa ni vipindi viwili tofauti au Mahoka ndiyo lilikuwa jina la kipindi huku Pwagu na Pwaguzi wakiwa ndiyo waigizaji wake?


Vipindi viwili tofauti.Ila baadhi ya waigizaji ni walewale.
 
ATC hewani kale kawimbo kalikua kananivutia sana...Kipindi kingine ni Majira hasa Ben Kiko Tabora aki report...Richard Leo....Ukweli mambo ya RTD ilikua imeivaa kila Idara
 
ATC hewani kale kawimbo kalikua kananivutia sana...Kipindi kingine ni Majira hasa Ben Kiko Tabora aki report...Richard Leo....Ukweli mambo ya RTD ilikua imeivaa kila Idara
Haha Ben Kiko alikuwa anaripoti matukio ya ajabu ajabu ndio huyo eti,?
 
Ooh kumbe...kuna kingine kile kilikuwa kinaitwa pole kwa kazi nadhani kilikuwa kinaanza saa sita
Kulikua na kipindi kinaitwa wakati wa kazi. Kilikua kinaanza saa tano kamili hadi saa sita kamili mchana, na walikua wanatembelea wafanyakazi mbalimbali katika maeneo yao ya kazi na kuzungumza nao kuhusu shughuli wanazofanya na kisha wanapewa fursa ya kutuma salamu kwa ndugu na jamaa halafu wanachugua muziki wautakao wanachezewa

Saa sita kamili hadi saa saba mchana kulikua na hicho kipindi cha mchana mwema ambacho nacho kilikua ni cha salamu na muziki

Pole kwa kazi ilikua ni jioni na pia kulikua na jioni njema
 
Shikamoo Muhenga Ses. πŸ™ˆπŸ™ˆπŸ™ˆπŸ™ˆ

Japo sivijui hivyo vipindi huku na mie ni Muhenga pia Ses kwa hili naomba nikazie tu maana sina jinsi.πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒ
 
Kipindi cha Sitasahau-RFA kila jumapili

Kipindi cha Wosia wa Baba wa Taifa-Radio Tz(TBC FM) kila baada ya taarifa ya habari saa 2 usiku

Kipindi cha Matagazo ya Vifo-Radio Tz(TBC FM) saa kumi jioni

Kipindi cha Darubini ya leo-RFA siku kuanzia saa 4(sina uhakika, nishasahau)
 
Haha uko sawa kabisa boss kwa kweli umekwiva
 
Nakumbuka baada ya kuacha kusikiliza TBC na kuhamia RFA nilikuwa napenda kusikiliza hiki kipindi cha Sitasahau kilikuwa kinarushwa saa mbili asubuhi siku ya jumapili kikifuatiwa na kile cha vitu vilivyovunja record sijui kiliitwaje baada ya hapo kilifuatiwa na Je huu ni uungwana???? Nlikuwa shabiki sana wa hilki kipindi wakati huo mtangazaji alikuwa Fredua ( sijui ndio inaandikwa hivi? ) baadae akaja mwingine anaitwa nani sijui mtani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…