Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Nakumbuka kupindi kilichokuwa kinarushwa siku za jumapili kipindi ambacho mgonjwa anahojiwa mwishowe anapewa nafasi ya kutuma salamu,
Vichekesho ilikuwasiku wakihojiwa vichaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] hatari

learn to serve
 
Haha, sasa sijui lengo la kuzima lilikuwa wafanyakazi wa kalale?

Mimi hadi leo ninayo kanda ya Jangalason nimetape baadhi ya vipindi.

Na tulishapigana na kaka yangu sababu ya kutape kanda zake hadi nikamchoma Kisu cha mguu.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] ulikuwa mtata wewe.

learn to serve
 
Edda Sanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa anaitwa Edda Sanga. Hivi yupo hai huyu mama? Mazungumzo baada ya habari acha kabisa. Nakumbuka karibu na uchaguzi wa 2000 yule baba mazungumzo yake yalijikita kuponda wapinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee nyie mwaka 2000 bado mlikuwa mnasikiliza RTD?!
 
Pia kulikuwa na vipindi kama zilipendwa na hongera. Enzi hizo kipindi cha michezo ni saa 2 kasorobo usiku, majira saa 3 usiku na taarifa ya habari za kutwa nzima saa 5 usiku. Enzi hizo uwanja wa fisi ndio umebamba jingle za hivyo vipindi zikiwa zimerekodiwa zikawa zinatumika kuwapumbaza walevi. Ikifika saa 3 inawekwa kanda ya kipindi cha michezo, ikifika saa 5 inawekwa ya majira, ikifika saa 7 inawekwa ya ngoma za Mzee Moria Nyunyusa kuonyesha ndio kwanza saa 5. Ilichukua muda mpaka walevi kugundua huo mchezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chei chei shangazi na Betty Mkwasa,Mama na mwana na Deborah Mwenda,jamani those days ilikuwa raha sana.Nimekumbuka hadithi ya Binti Chura.Na ile ya Ua jekundu.
 
chei chei shangazi na Betty Mkwasa,Mama na mwana na Deborah Mwenda,jamani those days ilikuwa raha sana.Nimekumbuka hadithi ya Binti Chura.Na ile ya Ua jekundu.
Hivi ilikuwa ua jekundu au Koti jekundu... Life was good those days.
 
Kumbe ulishazaliwa wakati huo?
 
Ninakumbuka mchezo wa kuigiza Masha aliolewa na Mawazo alikuwa na mawifi Naviwe na Havijawa, walimpelekesha Masha mpaka aliisoma namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…