Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Nakumbuka kupindi kilichokuwa kinarushwa siku za jumapili kipindi ambacho mgonjwa anahojiwa mwishowe anapewa nafasi ya kutuma salamu,
Vichekesho ilikuwasiku wakihojiwa vichaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Khaa walikuwa wanaenda hadi wodi ya vichaa? Hiki nilikuwa sikisikilizi saana maana kilikuwa kinarushwa muda wa kujiandaa kwenda kanisani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
akuuu labda unitajie ndo nimjue
Sasa unasemaje simtendei haki mtu ambae hata humjui? Kwa kukusaidia huyo dada anaitwa Moon Chae Won, Korean actress born November 13,1986..kwa hiyo ni muhenga mwenzangu upo ziwa?[emoji108] kama ulikuwa unasononeka kwa kumweka mtoto mwenzio you can now relax

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumbuizo Asilia - Michael Katembo , Khalid Ponera baadae Malima Ndelema

Starehe na BP - Julius Nyaisangah

Misakato - Julius Nyaisangah

Ugua pole - Walikuwa wanazunguka hospitali mbalimbali nchini kupitia wawakilishi wa mikoani na wale wa Dar

Nipe Habari - Siwatu Luanda

Mama na Mwana - Deborah Mwenda

Club Raha Leo Show - Julius Nyaisangah, Enock Ngombale na Geofrey Erneo

Kijaruba - Abdallah Mlawa

Mchana Mwema/Pokea Salamu - Christine Chokunegela na wenzake wengi

Chaguo la msikilizaji - Malima Ndelema

Mkoa kwa Mkoa - Michael Katembo, Nadhir Mayoka, Malima Ndelema

Disco Show - Julius Nyaisangah

General tyre na gari lako - Samadu Hassan

Ngano za Muziki - Salama Mfamao, Siwatu Luanda na wengine

Majira ya asubuhi na saa 3 usiku...

Watoto wetu - Watangazaji wa kike..

Mikingano - Salum Seif Nkamba 'SS Nkamba'

Mkulima wa Kisasa - Malima Ndelema

Michezo/Matangazo ya Mpira - Mshindo Mkenyenge, Omary Jongo, Ahmed Jongo 'Father', Dominick Chilambo, Mikidah Mahmoud, Charles Hillary, Juma Nkamia, Salim Mbonde, Abdallah Idrissa Majura na wengine..

Taarifa ya Habari - Julisu Nyaisangah, Charles Hillary, Betty Mkwasa, Sarh Dumba, Halima Kihemba, Jacob Tesha, Sekione Kitojo, Tido Mhando, Mikidad Mahmoud, Christine Chokunegela, Abdallah Mlawa, Abdul Ngalawa, Eddah Sanga, Aboubakary Liongo, Iddi Rashid Mchatta na wengine...

Mazungumzo baada ya Habari - Abdul Ngalawa, Mikidad Mahmoud

Pia walikuwepo wawakilishi wa Kanda/mikoa

Nyanda za Juu Kusini - Idrissa Sadallah, Martha Ngwila

Kanda ya Mashariki - Halima Kihemba , Penzi Nyamungumi, Monica Lyampawe..

Kanda ya Magharibi - Titus Philipo

Kigoma - Chisunga Stephen

Songea - Abisai Stephen

Lindi - Angalieni Mpendu

Ziwa Victoria - Dominick Chilambo, Nathan Rwehabura

Kanda ya Kati - Ben Kiko, Ahmed Kipozi, Sangi Kipozi, Hendrick Michael Libuda, Daniel Msangya, Wilson Malosha, Hellen Masele na wengine

Mtwara - Cassim Mikongoro

Kanda ya Kaskazini - Ahmed Jongo

Zanzibar - Yusuph Omary Chunda na Makame Abdallah

Hawa ni kwa uchache tu....
David wakati mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom