Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Ok. Uzee huu memory zinakata [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Mchana masikio kwenye radio mama na mwana. Ila hadithi ilibamba sana hiyo. Ikisimuliwa unasisimka na kuogopa kama unaangalia movie live [emoji23] [emoji23]
 
Jamani kulikuwa na kipindi kinaitwa OMBI LANGU mwakikumbuka? ilikuwa mtu anatuma ombi la muziki aupendao halafu mtangazaji anaurusha hewani!
Dah! Kumbuka kipindi cha ZILIPENDWA!
Ama hakika siku siku zimekwenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikurekebishe kidogo kwa KBC, kipindi cha je huu ni UUNGWANA kilitangazwa na mzee Leonard Mambombotela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kipindi hicho kulikuwa na Idhaa ya Taifa, halafu kulikuwa na External Service na kulikuwa na Idhaa ya Biashara iliyokuwa ikifunguliwa saa kumi jioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa ya habari ya saa moja jioni kutoka radio Tanzania Zanzibar, sijui kama wanajiunga tena siku hizi, nna miaka zaidi ya 15 bila kusikiliza rtd

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama na mwana mtangazaji alikuwa Eda Sanga ukiacha hadithi ya binti chura ilikuwepo hadithi ya Adili na nduguze,nakumbuka kulikuwa na idhaa ya biashara ilikuwa inafunguliwa saa kumi baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku inafuata mazungumzo baada ya habari yalikuwa yanasomwa na Abdul Ngalawa saa mbili na robo kipindi cha vijana Leo mtangazaji alikuwa Julias Nyaisanga ukipenda anko J,nakumbuka mbali sana ilikuwa mida ya jioni unajiunga na radio RSA Hapo utamsikia Moses Mkandawile,UJERUMANI, Hapo utamsikia Umani Heri,mabingwa wa salamu namkumbuka Kondo Ali Kondo,Zakaria Ndefoo mwinda tembo,chivalavala wa chivalavala wa mahuta newala nisimalize utamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenimumbusha Yusuf Omary Chunda nilisha msahau [emoji106] [emoji106] [emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…