Takwimu haziwezi hata siku moja kuwa sahihi kwa 100% na pia ni vigumu kuwa si sahihi kwa 100%, hivyo kama zimepotoshwa sana basi zitakuwa katikati!
Utafiti wangu BINAFSI nimeufanyia kwetu Dar, pia Mikoani kama Shinyanga, Arusha, Mbeya, Iringa, Mtwara na Lindi, na kote huko Uchumi wote kutoka kwenye miji Mikuu ya Mikoa mpaka Miji Mikuu ya Wilaya uko chini ya Wahindi!
Na ukitaka kulijua hilo leo hapa Tanzania jaribu kuanzisha shughuli yoyote ile halafu useme sitaki kuwahusisha Wahindi kwa namna moja ama nyingine uone kama hautakwama, anza hata kuvua samaki tu, lazima uende kitumbini kwa Muhindi akuuzie Nyavu, hata Ukitaka kununua vitenge upeleke nje ya nchi lazima uende kwa Wahindi vinginevyo haufiki mbali, spea za magari, Pembejeo za kilimo, Utalii, Mabenki, n.k na hawa ni watu ambao hawafiki hata asilimia Moja (1%) ya idadi yetu ya watu takribani milioni 40!
Serikali Simamisha kuonyesha Bunge Live Muda wa Kazi ili tufanye kazi kwa bidii na tutoke Hapa tulipo!