Wahitimu wanne wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamefanikiwa kubuni gari inayotumia umeme

Na wewe hujanielewa. Kumbe unadhani niliposema tufungue kiwanda nilimaanisha tuwe tunatengeneza gari kama hilo la wanafunzi wa NIT
Hilo gari lipo hivyo kwa sababu ni project tu ya wanafunzi, na it was meant to be as cheap as possible. Lakini ukifungua kiwanda gari haliwezi kuwa baya hivyo. Hilo gari la wanafunzi wa NIT ni baya kwa sababu imeundwa na team ya watu wanne halafu ni cheap, ukiwekeza hela na watu wengi gari linakuwa zuri zaidi
Mfano angalia hizi picha mbili. Haya ni magari ya umeme ya ITAOUA yanayotengenezwa Burkina Faso, na ni proper cars kabisa. Sio kwamba ukiendesha linadunda hovyo hovyo

ITAOUA, model ya SAHEL. Made in Burkina Faso 👇
 
Kwa sababu wengine wako more advanced, unataka wasitengeneze? acheni vijana wafanye kazi na ugunduzi ndio maendeleo, soko lipo sio kila mtu anahitaji gari la mchina
 
Waelimishe hao inaonekana hawana idea products and manufacturing zinavyofanyika dunia hii, hakuna mtu anatengeneza gari 100% kutumia original parts zake
 
Unaijua kampuni ya Nothing? Imeanza kutengeneza simu juzi tu leo hii ipo successful, simu zake ni nzuri na ina soko kubwa.
Wangekuwa na hii akili yako ya "Tumeshachelewa" hicho kiwanda cha Nothing kisingekuwepo duniani leo hii
 
hujitambui unajibujibu tu.hicho nikitu ambacho hakiwezekani wazungu sio mafala waweke kamera ya sony iingie kwenye iphone

uliona wapi?
Sony ndio anatengeneza camera sensors kwa iPhone enzi na enzi hawajaanza leo

Sony sio tu wanatengenezea iPhone camera sensors, bali wanatengenezea Samsung, Xiaomi, Oppo, Vivo, Tecno na makampuni mengi, kuna mengine hata hujawahi kuyasikia. Hata hiyo simu yako unayotumia, kuna uwezekano asilimia 99% inatumia camera sensors za Sony
Mpaka leo Sony ndio inaongoza kwa kutengenezea iPhone camera sensors. Soma hapa 👇👇

Pia iPhone 17 Pro Max nayo inatumia sensors za Sony. Fungua link hii hapa, nenda kwenye page ya camera usome specifications za kamera ya iPhone 17 Pro Max ambayo ndio simu yao bora zaidi kwa sasa

Hapo nimekuwekea link uone mwenyewe, ukiona uvivu kuifungua, angalia screenshot hii hapa chini. Hizi ndio specifications za kamera ya iPhone 17 Pro Max

Nadhani unaliona jina "SONY" hapo, tena kamera zote tatu plus ya mbele (jumla nne) zinatumia sensors za Sony

Ukitaka ushahidi zaidi niambie
 
Waelimishe hao inaonekana hawana idea products and manufacturing zinavyofanyika dunia hii, hakuna mtu anatengeneza gari 100% kutumia original parts zake
Mi nawashangaa wanawakandia vibaya mno wanafunzi kuassemble gari. Yani hata makampuni makubwa yaliyofanikiwa hayatengenezi kila kitu kwa 100%, vingine wananunua wana assemble
Halafu wao wanataka wanafunzi wa chuo watengeneze kila kitu from scratch na hawana hela za kufanya hivyo. Waafrika sijui nani alituroga
 
My question,

Did they made it or assemble it? If it's assembling then fundi garage can do it better?

For a university project, they need to go beyond assembling, as this has been practises now days, they need to add more features to say they made the electric cars.

They have more lab resources or financial resources plus additional supervisors for the job to look and feel professional.
 
Ndio uwe mgari mbaya hivyo kama mkokoteni
Kwanini wameshindwa kuiga hata muundo wa vitz
Kwanza ni vilaza, unapotengeneza gari kitu ni muhimu ni uzito wa gari vs energy consumption halafu wao wanatengeneza la umeme halafu zito kama gari la dizeli
 
Ndio uwe mgari mbaya hivyo kama mkokoteni
Kwanini wameshindwa kuiga hata muundo wa vitz
Kwanza ni vilaza, unapotengeneza gari kitu ni muhimu ni uzito wa gari vs energy consumption halafu wao wanatengeneza la umeme halafu zito kama gari la dizeli
Hata baskeli huna kelele tuu
 
Vijana wanajaribu, na hiyo inaonekana ni prototype tuu, acheni ujinga
 
Sio kweli, financial resources zipi hizo unasema wanafunzi wanazo? Na pia ni uongo kwamba eti kwa university they have to do beyond assembling. Huu ni uongo, we umesoma university yoyote Tanzania? Unajua ratiba za chuo zinavyobana? Kwamba ulitaka wanafunzi wa chuo kwenye project yao waanze kazi ya manufacturing? Umesikia NIT wana viwanda? Lab resources gani unaongelea we jamaa. Khaa
Halafu kama fundi garage can do it better ni jambo la heri, kwani ulisikia wanafunzi wanashindana na fundi gereji au? Wao wamefanya projecr yao na ndio hiyo hapo
Hayo mambo ya going beyond assembling ni kwamba unaota tu au hujui unachoongelea. Kwamba eti wafanye beyond assembling, ulitaka wafanye nini? Naona unaongea ilimradi tu na wewe uonekane umeponda, chuo ulisoma kozi gani na uliwahi kufanya project gani wewe binafsi?
 
Ndio uwe mgari mbaya hivyo kama mkokoteni
Kwanini wameshindwa kuiga hata muundo wa vitz
Kwanza ni vilaza, unapotengeneza gari kitu ni muhimu ni uzito wa gari vs energy consumption halafu wao wanatengeneza la umeme halafu zito kama gari la dizeli
Ulipokuwa chuo ulifanya project gani, genius?
 
Sawa ni rahisi kuunda, lakini hatuna kiwanda hata kimoja kinachounda magari ya umeme
Sasa hata tukibeza ni rahisi kufanya hivyo itasaidia nini wakati hatuna kiwanda hata kimoja cha kufanya hivyo
Cha ndege tunacho, bado cha magari
Walikuja. Benz wakati fulan wakataka kuweka kiwanda, wakazungushwa hadi wakakata tamaa kiwanda wakapeleka rwanda

Tatizo la hii nhci ji sera, urasimu kila kona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…