Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Naweza nikakipata wapi
 
Mkuu uko sawa. Uebert Angel nimemfuatilia tangu 2018. mara ya kwanza kumwona mtandaoni nilijua mhuuni fulan wa kiinjili,nilijaji kitabu kwa kuangalia cover. Baada ya kumsikiliza deeply alisababisha nishindwe kuwasikiliza wahuburi wengine mitandaoni mpka nilipomsikia akisema Pastor Chris ni baba yake,kumfuatilia naye wa moto pia. Lakini yote kwa yote uebert Angel bado ndio nilishaganda. Wakati anakuja Dar June mwishoni,nilisafiri kutoka Geita just kuhudhuria live,sijuti kumfahamu huyu mtumishi.
 
Benny Hinn mzee wa Roho Mtakatifu,hiki ni chuma
Mkuu, fahamu kuwa imeandikwa, USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA.

Kama Bonnke aliamini kuwa Benny Hinn ni mtumishi wa Mungu, si vizuri wewe kumwita tapeli.

Angalia video Bonnke akimwombea Benny Hinn na mkewe.
 
Benny Hinn mzee wa Roho Mtakatifu,hiki ni chuma
Like the father like the son. Mlezi wake wa kiroho alikuwa Kathryn Kuhlman, mhubiri aliyekuwa "akitembea" na Roho Mtakatifu.
 
Mwanzoni nilitaka kumtilia mashaka kutokana na kilichoonekana kama miujiza iliyozidi kiasi kwenye huduma yake. Lakini kadiri nilivyomfuatulia, ndivyo nilivyozidi kugundua kuwa hayupo kinyume na Maandiko. Nilisikiliza mahubiri yake kadhaa na kusoma vitabu vyake kadhaa, vikiwemo GENETICS OF WORDS, PRAYING FOR THE IMPOSSIBLE, PRAYER BANKS, SPIRITUAL WARFARE, etc.

Nilipofahamu kuwa mentor wake ni Pastor Chris, na kwamba anawakubali akina Benny Hinn,David Oyedepo, Kenneth Hagin, T. L. Osborn, n.k., mashaka yote yaliniisha.
 
Naweza nikakipata wapi
Mwandishi wake ni Dr. Charles Sokile. Mimi nilikinunua Dodoma mjini mwaka 2010. Nafikiri, kinaweza kupatikana kwenye maduka ya vitabu, hasa Dar Es Salaam. Ukikikosa, wasiliana na huduma ya New Life Band. Mkurugenzi wa hiyo huduma ni Hondo ambaye ni mtoto wa Mabondo. Kwa vyo vyote, wanajua kinapopatikana.
 
Mzee wa Neema Pastor Ceasar Masisi

Anahuburi kweli ya Kristo
 
huyo Uebert Angel, umepotea. mwalimu wenu pia ni mhubiri mzuri ila huwa hajui hata anachohubiri kwasababu hajawahi kuexperience wokovu wa kweli. the same kwa kimaro. mwenye kuelewa ameelewa.
Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…