Wahudumu na Uongozi wa Fish Market mnaishiriki dhambi mbaya ya ubaguzi pasipo kujua malipo ni hapa hapa

Mkuu - Huo ubaguzi umeanza lini hapo Fish Market? Mimi huwa napitapita hapo mara kwa mara kupata moja moto moja baridi, na kusikiliza Muziki wa huyo Mwarabu kila Ijumaa - sijawahi kuona huo Ubaguzi.
Labda ni wale wanaokaa masaa kibao wakisubiri wapate muthungu huku wakiwa na soda masaa mengi huku wakizuia viti

Nimeona video clip wanawaongelea wazungu tu
Nilikuwa nasubiri wanaume waje waseme pia
Mbona wanawake tu ?

Shukran kwa kutufungua hapa
Naona wanaenda kudanga tu
 
Nasubiri kuona video yenye malalamiko ya wanaume wakilalamika kubaguliwa katika mgahawa huo kabla sijatoa comment fulani hivi.
Hakuna

Hao wanununuzi wa soda tu mpaka wachukuliwe na mteja

English sasa [emoji1] [emoji1787] ya kudanganyia wazungu

Ila wanajitahidi siku hizi maana miaka ya nyuma walikuwa wanalalamika wanachukuliwa wanaume na wakenya kwa kuzidiwa kimombo
 
Tatizo wanaoharibu hizo sehemu ni wale wadangaji wanaoenda saa 11 jioni wanajinunulisha bia moja inafyonzwa hadi usiku huku macho hayatulii kama fundi saa alopoteza nati.

Na sio CTFM tu hata Wavuvi Kempu wapo wengi, sasa wanawaponza wengine wanaoenda kwa lengo hasa la kula raha kwa pesa zao.

Kingine kuna utaratibu wa ku book meza naona hii wengi wameshindwa kuielewa na kuhisi wanabaguliwa pale wanapokaa kwenye meza baada ya muda wanaambiwa wanyanyuke kwa maana meza ina wenyewe.
 
Bora umelielezea kwa uhakika kabisa
Mimi nilienda hotel moja kubwa hao wadada wanajipitisha zaidi ya mara 10 hadi kero
Garden imekuwa ukumbi wa kupitapita na visimu vyao mara wajipige mara wavue viatu

Hawana hata hela ya kununua bia masikini ila wanakera sana
 
Daah mi niko kwenye hii hii huduma inaniumiza sana nkiona mswahili au mytu mwengine hasa muhindi anabagaliwa na wahudumu wengi huwakimbia waswahili wenzao sababu ya kuhudumiwa vizuri uwa awaachi tip nzuri na wahindi sababu ni wasumbufu ila sio kitu kizuri nyie wafanyakazi wa migahawa na mahotel kumbukeni kipindi cha corona wateja wa ndani ndio walikuwa muhimu sana tuthamini kila mteja.naamimi uongozi wa Fish market mtarekebisha jambo hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…