Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Wewe ni nani kuhukumu..hujui uwepo wa haya makanisa ndio ueneaji mkubwa wa injili.

Au ulitaka waje kusali kwako ndio uone wako sawa.?

#MaendeleoHayanaChama
Sio KILA kanisa ni la MUNGU mengi ni mahekalu ya shetani
 
Sio KILA kanisa ni la MUNGU mengi ni mahekalu ya shetani
Unathibitishaje haya uyasemayo?

Hujui hata maandiko yamesema acheni ngano na magugu yakue pamoja..yatapepetwa wakati wa mavuno.

Chamsingi injili isonge mbele..awajuaye wale wa kweli ni kristo mwenyewe.

As long as injili inahubiriwa kwenye hayo makanisa hiyo ndio furaha yangu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hapa nchini hakuna mwimbaji wa injiri anayefikia viwango vya Rose Mhando, hakuna! hakuna! hakuna!
 
Kupitia maandiko magugu yanaonekana,bora watu waambiwe ukweli waamue wenyewe kutembea na ngano au magugu.
Injili zingine za shetani kupitia maandiko mfano
1.Daudi alicheza hadi akabaki uchi, 2.Mungu anaangalia roho
3.Mafuta, chumvi,maji,upako,hizi ni hirizi toka lini Yesu akachanganywa na visaidizi hivi vya kipepo.Au tangu lini shetani akayaogopa mafuta aliyowapa watumishi wake?
Haya ni mafundisho ya kuzimu kupitia mawakala wao makanisani.
 
Jamani wekeni msaada hapa 😊
 
Kuna nyimbo hizi mbili nazitafuta
1.kuwalaani wana waisreali balaam nani aliimba hiyo nyimbo

2.na yapili sijui nani aliimba wanacheza ofisini wamekaa kwenye meza kubwa jamaa anaimba vizuri sana

Naombeni msaada
Ngoja wataalamu wanakuja.. jaribu kucheki pia youtube.
 
Hiyo List 1-10 wanasali kanisani kwako nini? Itakuwa wote mnasali kanisa moja Nyinyi
Mimi sina kanisa. Kwenye list nzima ninayefahamiana naye ni mmoja tu. Pia hakuna hata mmoja hapo anayesali kanisa moja na mwenzake.
 
Joel Lwaga bado sana.

Alibebwa na wasanii wa kike wa bongo muvi lakini wa kawaida sana
 
Yaani eti unamtoa Bahati Bukuku na Rose Muhando kwenye first list unamweka Paul Clement.

Ua not a serious Christian.
Kwamba Paul Clement sio serious christian? Rose na Bahati wana vipaji, hakuna anayepinga lakini vigezo vilivyotumika vimewaweka kando kwa sasa. Miaka ijayo wanaweza kirudi watakaporejea kwenye misingi walikoanzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…