Abtali Mwerevu
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 796
- 707
Wasukuma ni watu wanaopenda sana utamaduni wao hasa katika suala la nyimbo. Ni kabila pekee hapa nchini Tanzania lenye waimbaji wengi pengine idadi yao ni kubwa hata kulingana na waimbaji wa bongofleva. Kama unabisha, nenda youtube andika nyimbo za kisukuma, utaona waimbaji wasio na idadi. Unaweza kushangazwa na idadi ya view huko youtube, jamaa wanawazidi baadhi ya wasanii wa bongofleva kwa mbali sana, wapo waimbaji wanapata mpaka view milioni nne ndani ya muda mfupi tu!
Hata hivyo, waimbaji wengi wanaimba kwa mtindo wa kufanana usiokuwa na utamu wa kusikiza, wapo wachache wanaoimba vizuri na kupenda nyimbo zao na huenda zikawa na mvuto kuliko hata waimbaji wa Bongofleva. Siyo rahisi kuwapata waimbaji hawa, lakini nimekusogezea watatu pamoja na kazi zao.
Namba Moja ni Nkenyenge, huyu jamaa siyo rahisi kupata kazi zake, nimeambulia kupata kazi moja tu, lakini siyo mchezo, ni mziki mtamu sana:
View: https://youtu.be/_Bd0gQnZUD0?si=imjib7VSAppQDIMP
Namba mbili na Tatu ni Limbu Luchagula na Mayiku Sai: Jamaa wanaimba vizuri sana kwa kuja na melodies mpya tofauti na mazoea ya waimbaji wengine wa Kisukuma, hapa wapo pamoja katika wimbo:
View: https://youtu.be/1nlP-zg80l4?si=AGFCA1fi4RnQuMMX
Ongeza idadi zaidi...