Waislam kubalini Wakristo wamewazidi katika maeneo mengi nyeti. Kama haya kisha mjifunze

Waislam kubalini Wakristo wamewazidi katika maeneo mengi nyeti. Kama haya kisha mjifunze

Hamjambo!

1. Waislam ni kama Kaini kwa ndugu yake Habil. Wanaona wivu na kuwa na hasira na maendeleo ya Wakristo.

2. Mimi kwa upande wa Baba ni Waislam. Mara yangu ya Kwanza kuingia msikitini nilishangaa Sana. Waislam wengi hawajaujenga uislam kama taasisi.

3. Unaweza kuingia msikitini Siku ya ijumaa na msikiti usijue hata jina lako.

4. Waislam Dini yao inategemea misaada zaidi ya watu binafsi kuliko wajibu wa mtu mmojammoja kuwajibika kuujenga uislam na maendeleo yake.

5. Bila kupoteza Muda nitaeleza mambo nyeti ambayo Wakristo wanawazidi kwa mbali ndugu zao Waislam;

a) Usimamizi wa Rasilimali watu.
Waislam hawana tools mbalimbali za kusimamia watu tofauti na madhehebu ya Wakristo.

I) Wakristo wanajua idadi kamili ya waumini wao na wanamfumo wa kuhesabu waumini wao Kila Mwaka.
Kila Kanisa, Kila jumuiya, Kila kanda inajua waumini wake. Programu mbalimbali kama Ubatizo, jumuiya, Kaya na familia, komunio ni moja ya mambo yanayotoa idadi ya watu katika ukristo.

ii) Kila jumapili au jumamosi lazima waliohudhuria wahesabiwe na wageni wajulikane.
Wapo mashemasi KAZI Yao ni kupanga watu, kuhesabu watu, kusimamia watu na kuhakikisha Ibada inaenda sawasawa.

Waislam hata uende Leo msikitini hakuna wa kukuuliza umetokea wapi, hawana huo mfumo.

ii) Kujua idadi ya watu ni muhimu katika usimamizi wa mission na malengo ya Kanisa.

b) Mifumo ya Kutoa zaka na Sadaka.
i) Wakristo wote Duniani iwe amesoma au hajasoma. Kutoa sadaka na zaka ni sehemu ya ibada.

ii) Huwezi kwenda kanisani bila sadaka au zaka hiyo tangu tukiwa watoto tunafundishwa.

iii) Watoto wa Kikristo wanafundishwa kutoa wakati waislam hawatilii mkazo kwenye utoaji.

iv) Kila kanisa Lina kanisa la watoto au Ibada ya watoto ambazo zinaendeshwa katika mfumo uleule wa wakubwa.

v) Nilishangaa kumsikia sheikhe mmoja akisema ati msikiti mzima waislam wote sadaka ni ngumu kufika Laki tatu. Hiyo kama sio aibu ni kitu gani.
Wakati laki tatu ukienda pale Kanisa la wasabato Mwenge au Magomeni au Manzese hiyo ni sadaka inayotolewa katika kanisa la watoto.

vi) utoaji ni utamaduni na tabia ambayo MTU anafundishwa tangu akiwa Mdogo. Wakristo kwa Hilo wamefanikiwa.

vii) waislam kama kutoa tuu sadaka elfu kumi au elfu hamsini anashindwa ataweza kumchangia sheikhe Anunue gari walau la million 50?

viii) Waislam wao wanachojua ni kuswali, kufunga Ramadhan, kusikiliza Kaswida, kusoma Quran. Hicho wanajua. Waambie watoe sadaka au zaka. Huo wajibu wengi wao hawautimizi. Na hawautilii maanani.

ix) Masheikhe na maimamu kibao huku mitaani wanadhalilika. Mnashindwa kuwatunza maishekhe wenu, maostadhi wenu, imamu wenu ambao wala sio gharama kubwa. Milioni mojamoja kwa mwezi Kila sheikhe nchi nzima. Mnashindwa. Mtaweza kuchangia mambo ya sijui ujenzi wa hospital, ujenzi WA shule, au mambo mengine?

x) Sio kwamba Waislam hawana pesa au vipi. Hapana ni utamaduni huo ndio hawana. Utoaji.
Kwani waislam wangapi ni waalimu huko serikalini, waislam wangapi ni madaktari, wanasheria, manesi, madereva, wafanyabiashara. Lakini waambie kutoa uone utakavyogombana nao.

c) Wakristo kupitia Zaka wanajua kipato na KAZI ya Kila muumini.
I) Yaani ukishakuwa mkristo ukaenda Kanisani lazima watu uongozi ujue kipato chako.

ii) Zaka ni lazima kwenye dini ya Ukristo. Yaani huwezi kumuabudu Mungu kama hutoi Zaka.

iii) Zaka ni kuonyesha Mungu amekubariki na shukrani hivyo unarudisha fungu la kumi la kipato chako kwa Mungu kupitia Kanisa unaloabudu.

iv) Waalimi, madaktari, manesi, madereva, na wafanyakazi wote kanisani wanajulikana na mishahara yao inajulikana.

v) Mwallimu anayelipwa Laki Saba fikiria anatoa Zaka elfu 70 Kila mwezi. Hiya ni nje ya sadaka na michango mingine.

vi) Kwa waislam hawana mfumo huo. Waislam mnaosoma hapa. Kuna wafanyakazi. Jiulize wewe unalipwa milioni Moja au unafanya biashara kwa mwezi unapata milioni moja je, Kila mwezi unatoa msikitini Laki Moka ya zaka?

vii) Kwa wakristo usipotoa Zaka uongozi utajua tuu. Kwani Kila kitu kinaenda kwa mfumo wa maandishi na ushahidi.
Utatembelewa na lazima uhojiwe.
Waislam wao hiyo hawana. Kwanza hata hawajigusi.

d) Ni wajibu na jukumu la muumini kuchangia miradi ya kanisa.
i) Sadaka zinazotolewa kanisani zina kazi nyingi.

ii) Kuna marekebisho ya kanisa.
iii) Kuna kazi ya utume na kueneza injili.
iv) Kuna kuanzisha na kuboresha miradi ya Kanisa.
v) mambo hayo yote waislam hawana.
Huwezi sikia msikitini waislam wanatoa sadaka ya kujenga mashule au hospitali za kiislam.
vi) Na waislam moja ya maeneo waliyodhaifu ni kwenye mawaidha ya utoaji sadaka na zaka. Ninafuatiliaga mafundisho Yao wakigusia utoaji sadaka na zaka. Wanatia huruma kweli. Sheikhe au mtoa mawaza anazungumza kama anabembeleza waumini.
Kwenye ukristo kutoa sio hiyari. Kutoa ni lazima. Na kuna namna mbalimbali za kushinikiza Jambo Hilo kama kutumia misiba, harusi na mambo kama hayo.


6. Kanisa linasapoti KAZI za Waumini.
I) Ukijua kupiga kinanda na kuimba utasapotiwa na kanisa.

ii) Ukiwa na project inayohusiana na dini utasapotiwa. Mfano uimbaji na muziki.
Lakini ni waimbaji wangapi wa kiislam wanaoimba Kaswida ambao Waislam wanashindwa kuwasapoti? Wangapi?
Huyo Mzee Yusuph ambaye aliamua kuacha nyimbo za kidunia akasema aimbe Qaswida aliishia wapi? Waislam Siku za maulidi, siku za idi siku za sikukuu zenu mnashindwa kuandaa matamasha ya kiislam mkaita waimbaji wa kiislam, waumini wa kiislam wakatoa kiingilio, wasanii wa kaswida wakapata, na misikiti ikapata. Hamtaki! Mnalalamika.

iii) Kanisa linasapoti wenye shule na hospitali.
Wasabato kuna wakati ambao sio Siku ya ibada labda sikukuu ya Makambi wenye shule au miradi wanapewa nafasi kuonyesha miradi yao. Na waumini wanasapoti, wazazi wanapeleka watoto shule za kanisa.

Ni lini ninyi waislam mliwahi kufanya hivyo? Ni waislam wangapi wanamiliki shule mkatumia misikiti yenu kuwasapoti hata kwa wao kuonyesha miradi Yao kama sehemu ya matangazo? Hamfanyi. Leo mnataka muwe Sawa na Wakristo? Kuweni serious

7. Viongozi wa Dini ya Kikristo Siku zote wapo Upande wa Waumini wao.
Kile waumini wanataka ndicho Viongozi wa dini watakisema full stop.

I) Nyie Waislam hamna umoja. Masheikhe wanataka heshima za burebure kisa kusoma Quran. Nani atakupa heshima hiyo?

ii) Kueni upande wa waumini wenu. Muone kama Waislam hawatakuwa upande wenu.

Iii) Unakuta viongozi wengi wa kiislam badala wawe upande wa Waumini wao wenyewe wanakuwa upande wa serikali. Alafu muda huohuo wanataka waumini wa kiislam watoe sadaka na zaka au wawasikilize. Hakuna binadamu mjinga atafanya hivyo.

iv) Wachungaji wengi wakiongea wanaangalia waumini wao wengi msimamo wao na matakwa yao ni yapi. Wanasimamia hapo. Bila kujali matokeo.
Wauumini nao wanajua chakufanya.

v) Wachungaji wengi wanaishi maisha mazuri na wanalipiwa bills karibu zote mpaka kusomesha watoto kwa sababu ya majukumu yao. Na wakristo hilo haliwaumizi.
Wakristo wanaumia pale wanatoa sadaka na zaka alafu mchungaji hatekelezi wajibu wake.

vi) Waislam lazima mbadilike.
Nasikia Masheikhe Kila Siku wanalalamika. Ooh! Ndugu waislam nyie hamsikilize viongozi wenu, sijui hamuwapi hela. Hivi kusoma tuu hiyo Quran unafikiri ndio sababu ya waumini kuwa upande wako au kukupa pesa?

8. Matamasha, programu na media zinazopromoti ukristo na kazi za wakristo.
i) kuna kina Goodluck Gozebeth, Joel Lwaga, Angel Bernad, Clement, Rose Muhando, Bahati Bukuku, Njiro SDA kwaya kishindo cha Wakoma, Zabron Singers Mkono wa Bwana, n.k.
Vijana wa Kikristo mfumo wao unawabeba. Wanatangaza kazi zao, wanapata pesa, Makanisa Yao wanawatumia wote wanapata pesa.
Jamii inaburudika. Vyombo vya habari vinatumika kutangaza kwa namna na mbinu zote.
Waislam hata upite mtaani sasa hivi unaweza ukaa mwezi mzima usisikie wimbo wa kiislam.
Sasa hivi ninauhakika ukimwita muislam akutajie waimba Qaswida watatu tuu anaowajua ili umpe laki Moja hawezi kutaja. Ila huyohuyo muislam mwambie ataje waimbaji wa kikristo atakutajia hata kumi na nyimbo zao ataimba.

ii) Waislam waliopo kwenye vyombo vya habari kama redio au luninga lini utasikia wameweka Qaswida nje ya Siku ya ijumaa?
Lakini njoo kwa Wakristo, Madj, waendesha vipindi redioni au luningani haiwezi pita Siku usisikie nyimbo ya Gospel hiyo haiwezekani.

iii) Wakristo wanauwezo na wanamifumo ya kutrendisha wachungaji na wanamuziki wa Injili na Kila mmoja anamuachia mwenzake nafasi.
Sasa hivi kuna wimbo wa Makombolelo. Chuma kinapaa watu wanapata pesa na ujumbe unafika.

Waislam hawana hiyo mifumo. Uislam umelimit baadhi ya maeneo na hiyo kuufanya ukose sapoti ya vijana na wakati wa sasa.

9. Sikukuu za kikristo zipo Kiroho na kibiashara.
i) watu wanaabudu Mungu na hapohapo wanapata pesa.
Waislam wanaabudu bure na wanatoka bure.
Dini ya kikristo sio Dini ya Bure. Inagharama ya kiroho na kimwili.

ii) Christmas ni sikukuu inayonifaisha jamii na taifa na dunia nzima. Waimbaji, watengeneza filamu, wachungaji, watangazaji, n.k. Wote wananufaika.
Lakini vipi sikukuu za waislam?

Nina mengi ya kuandika lakini ndugu zetu waislam mnamambo mengi ya kujifunza kuhusu Wakristo ili nanyi mfanikiwe.

Mnasema kwamba MOU inapendelea Wakristo, hicho ni kisingizio tuu. Huko Uarabuni kuna MOU? South Africa, Nigeria, na nchi zingine zinaMOU?
Hizo nchi za kiislam tuu kama sio kuweka vikwazo kwa Wakristo unafikiri Ukristo ungekuwaje nchi hizo?

Ndio maana Mission na Missionary.

Kufikia hapa sina la ziada.

Taikonmaster
Kwa Sasa Dar es salaam
Kiongozi umeandika vizuri,shida ya sisi waislamu ni taasisi inayoitwa BAKWATA.....
 
Baadhi ya mifano: Ukienda North Nigeria kuliko jaa waislam wenye kipato cha kawaida; ILA wanapigana vita huku wakiwa na silaha za kisasa ambazo huwezi kuzipata huku Africa na hela nyingi wanayotumia ni dola;
Sijaelewa, mbona sasa hao magaidi wa Nigeria wanaua wakristo? Yaani mzungu anafadhili magaidi kuua wakristo inakuaje tena inadhoofisha uislam? In fact Waislam tayari ni majority Nigeria.

Nadhani hauna facts vizuri, kingine kama wangetaka kudhoofisha uislam mbona wanapokea wakimbizi wa hiyo Syria, Afghanistan n.k huko Ulaya?
 
lutheran husikiag kwenye matangazo yao wanasema jumapili walihudhuria watu kadhaa wanawake 120 wanaume 70 na watoto 50? catholiki sijui sana ila walokole huwezi enda mgeni na wasikutambulishe lazima upewe maiki useme unaitwa nani umetoka wapi na kama unapita tu au utabaki hapo.
Hakuna kabisa linalohesabu watu labda hayo ya kilokole yenye waumini wachache, hata yale type ya mwamposa hawahesabu
 
Hii ndo mbinu yako mpya uliyokuja nayo ya kuchochea utengano wa wakristo na waislamu?

Umefeli pakubwa.
Hapana mkuu, wala hakuna hata Neno moja la uchochezi

Jamaa anatamani Waumini wa Kiislamu wawapende maimamu wao
 
Hapana mkuu, wala hakuna hata Neno moja la uchochezi

Jamaa anatamani Waumini wa Kiislamu wawapende maimamu wao
Uislamu na ukristo ni dini tofauti zenye mafunzo tofauti.

Kipindi hiki focus ni 9D kwanza.

Please msitutoe kwenye reli na mambo yenu ya dini.

Ngoja tumalizane na wauaji na watesi wetu kwanza halafu tutarudi kwenye hayo ya dini.
 
Kiongozi; Jifunze kuandika kwa ufupisho ili watu wengi wasome;
Uandishi wote huo umeandika point moja tu, ya kuhimiza utoaji.
Naona umemalizia kwa kusema, ukristo usingezuiwa ungesambaa sana. Kwa taarifa yako Uislam unapigwa vita vikuu pengine Ingekuwa sio Dini yenye baraka za Mungu ingefutika kabisa Duniani ILA wanaoweza kuelewa ni wenye maarifa tu.... Nikupe mifano michache....

Vita unavyo sikia Duniani kwenyye Nchi/maeneo yenye waislam wengi; karibia zote zinatengenezwa ili kudhoofisha uislam...kama walivyo mtengeneza Osama Bin laden akaja kuwageuka...
Baadhi ya mifano: Ukienda North Nigeria kuliko jaa waislam wenye kipato cha kawaida; ILA wanapigana vita huku wakiwa na silaha za kisasa ambazo huwezi kuzipata huku Africa na hela nyingi wanayotumia ni dola; Isis huko Siria, wana silaha za kisasa kabisa duniani na hela nyingi, juzi kati mamluki kaenda kuishambulia Irani kwa kisingizio eti anataka kutengeneza Nuclear? kwani ni nchi ngapi zenye nuclear Duniani?; Baada ya Libya kufanya vizuri sana kwenye uchumi na kuanza kutaka Nchi za kiafrica zikakope kwao; wakatengenezewa skendo, mara, anatesa watu,, dictator , anasihala za nuclear...wakati kule vijana wasio na ajira walilipwa mshahara, matibabu bure, kusoma ilikuwa bure, petrol sawa na bure, ukioa mahari inalipwa nk nk nk
ILA wakamuua (Call a dog a bad name and kill him.

Naamii ipo siku hata kama ni miaka 100 ijayo ataingia kiongozi katika Taifa kubwa, na kukataa kabisa huo uovu wa kuanzisha na kuwapa pesa na silaha za kivita hayo mashirika ya kijasus wanayotengeneza sijui Isis, Alshabab nk nk na ndipo hapo DUNIA ita tambua dini ya kweli duniani ni ipi?
Huwa sikubaliani na hoja za dini. Mnaudogosha na kuunyongesha uislam. Mnaufanya uonejkane dini ya kuonewa. Jambo la kawaida mtu yoyote anafanyiwa ila akifanyiwa muislamu utaskia kwa sababu ni "muislamu"

Kuhusu vita na vikundi si kweli lengo ni kuupiga Vita uislamu. Hivi vikundi vya vita vipo nchi nyingi kulingana na malengo yao. Congo kuna waasi miaka mingi, kungekua na majority ya Muslim ungesema sababu ni uislam
Uganda kulikua na waasi kwa miaka mingi, ingekua majority ni waislamu napo ungesema uislamu unapigwa Vita
Angola, Liberia , Sierra Leone n.k

Leo hii marekani anajiandaa kuivania Venezuela, kwa hoja zako hizo Venezuela kungekua na waislamu wengi ungesema wanavamiwa sababu ni waislamu.

Mmekua watu wa kuhisi kuonewa kila mara, acheni kujidogosha na kujipa unyonge.
 
Sijaelewa, mbona sasa hao magaidi wa Nigeria wanaua wakristo? Yaani mzungu anafadhili magaidi kuua wakristo inakuaje tena inadhoofisha uislam? In fact Waislam tayari ni majority Nigeria.

Nadhani hauna facts vizuri, kingine kama wangetaka kudhoofisha uislam mbona wanapokea wakimbizi wa hiyo Syria, Afghanistan n.k huko Ulaya?

Ukitaka kumuua paka au mbwa na watu wasikulaumu, cha kwanza ni kumpa jina baya (Call a dog a bad name and kill him...
Kwa kuwa una mtandao fuatilia pole pole yaliyotokea; Sep 11, ile ya Osama; naamini utapata cha kujifunza...
Theory nyingi za physics zinakataa yale majengo yalivyo anguka ndani ya muda mfupi kulingana na ulio kuwa umadhubuti wake, na udongo wa yale majengo sijui kupelekwa wapi ??? nk
 
Ukitaka kumuua paka au mbwa na watu wasikulaumu, cha kwanza ni kumpa jina baya (Call a dog a bad name and killi him) na hii ni hata kama kwa kufanya hivyo itafanya watu wako wachache waadhirike...
Kwa kuwa una mtandao fuatilia polepole Sep 11, ile ya Osama; naamini utapata cha kujifunza...
Nachojua Osama alipewa support kupambana na Urusi enzi hizo imevamia Afghanistan ila baada ya vita akawa tayari ana fedha, silaha na intelijensia ndio akageuka mabosi zake. So kuna interest za geopolitics ila sio UDINI.
Kule upande wa juu (Kaskazini ndipo wapo waislam wengi wenye kipato cha kawaida). Umewahi kujiuliza hayo macontainer ya silaha za kisasa kabisa duniani wanatoka wapi, na hela nyingi za kugawa bure..
Eeh si wana support za kutoka UAE, kama tu RSF mbona wanapewa silaha na UAE? Na hata licha ya hivyo bado wana uwezo wa kununua maana wanateka, wana mabilione wachimba mafuta wa Nigeria wana wa support kwa maslahi yao. If anything ni interest za kiuchumi ila sio DINI.

Tuache mawazo ya kidini Afrika, Congo wanauwana mbona hamsemi ni wakristo wanachafuliwa? Au mauaji ya kimbari mbona hatusemi kanisa lilichafuliwa? Ila yakitokea Nigeria basi ni waislam wanachafuliwa?

Duh tuna safari ndefu sana waafrika kujua adui yetu wa kweli
 
Nani anawafanyia makusudi?
Nikuulize swali dogo, kipi kinawazuia nyie waislam kuchangishana kuwanunulia magari hata ya million 50 masheikhe wenu? Kitu gani hicho?

Kipi kinawazuia kusapoti wasanii wenu wa Qaswida kama kina Mzee Yusuf mpaka wanaamua kurudi kwenye nyimbo za dunia? Kipi hicho huko nako mtasema serikali?

Kipi kinawazuia kuwalipa mishahara masheikhe wenu nchi nzima na maimamu? Kipi hicho?

Kama walokole tuu wanaweza nyie mnashindwa kitu gani?

Twende kwa hoja
Mbona unataka kulazimisha watu waishi maisha unayoyataka wewe?
 
Mimi ni Mkatoliki NAKATAA UDINI. Waislamu & Wakristo wote walipigwa risasi.

Tunaungana kwa pamoja kumpinga Dikteta samia kama ilivyo kwa Magufuli na sio sababu ya DINI
 
Nachojua Osama alipewa support kupambana na Urusi enzi hizo imevamia Afghanistan ila baada ya vita akawa tayari ana fedha, silaha na intelijensia ndio akageuka mabosi zake. So kuna interest za geopolitics ila sio UDINI.

Eeh si wana support za kutoka UAE, kama tu RSF mbona wanapewa silaha na UAE? Na hata licha ya hivyo bado wana uwezo wa kununua maana wanateka, wana mabilione wachimba mafuta wa Nigeria wana wa support kwa maslahi yao. If anything ni interest za kiuchumi ila sio DINI.

Tuache mawazo ya kidini Afrika, Congo wanauwana mbona hamsemi ni wakristo wanachafuliwa? Au mauaji ya kimbari mbona hatusemi kanisa lilichafuliwa? Ila yakitokea Nigeria basi ni waislam wanachafuliwa?

Duh tuna safari ndefu sana waafrika kujua adui yetu wa kweli

Sehemu nyingine za Africa wanapiganishwa kwa sababu za kiuchumi
Wakishaona mahala kuna fursa ya kueleweka (Madini, petrol, gas) mnapiganishwa hadi hao wakoloni waje kujifanya kuwapatanisha na kujichukulia raslimali zenu kizembe....
Mfano: Congo, sUDANI kUSINI, north Mozambique, nk nk nk
 
Nashangaa huyu jamaa naye anaingia huu mtego wa udini. Ni mjuaji sana alafu hakuna anachojua
Ni kweli kabisa mara nyingi sana hasa hizi mada za dini ndio kabisa huwa anazingua sana,hajui halafu hajui kama hajui

Ninatoa mifano michache tu

1. Zaka kwa waislamu ni miongoni mwa nguzo za Uislamu, katika Uislamu kuna nguzo tano,na Zaka ni moja kati ya nguzo hizo,sasa utasemaje kuwa Uislamu haueweki kipaumbele katika zaka?

Na asichojua kingine ni kwamba zaka kwa dini yetu ni mapato ambayo yana kiwango maalumu cha kutoa na baada ya kupita mwaka,yani hela hii iwe imekaa mwaka mzima kisha unatoa asiimia 2.5 ya mali hiyo

Na kama pesa hiyo haijafikia kiwango cha kutoa basi mtu huyu hana wajibu wa kutoa zaka,kiwango cha pesa ambacho mtu anatakiwa awe nacho na kuwa na kigezo cha kutoa zaka ni thamani ya pesa sawa na gramu 85 za dhahabu

Wastani wa haraka haraka wa shilingi milioni 14,na hizi hela zikae mwaka mzima kama ziada kisha anatoa asilimia 2.5 ya pesa hiyo

Ndio maana zaka kwa waislamu imewajibika kwa matajiri

Kuna zaka ya mazao,mfano umevuna gunia kumi basi unatoa gunia moja kama zaka,zaka ya mazao hutolewa mara tu pale unapovuna

Na vile vile kama umetumia kilimo cha umwagiliaji zaka yako ni tofauti na mtu anayetegemea mvua tu

Huo ni mfano mmoja wa zaka nimempa tena nimechokonoa kidogo tu

Sadaka ndio haina kiwango maalumu na unatoa muda wowote ule,na hii imesisitizwa sana hakuna muislamu asiyejua umuhimu wa kutoa sadaka
Kwani kwenye qur'an tunaambiwa mara tu pale mtu anapotolewa roho basi kitu cha kwanza ambacho atakiomba ni kupewa muda walau akatoe sadaka ili awe miongoni mwa watu wema

Sasa kwa uelewa wake mdogo mtoa mada anakuja kuropoka hapa

Anazungumzia sijui kuimba kaswida hajui haya ni mambo ambayo yana hitilafu kubwa kwenye uislamu,kuna ambao wanaamini ni haramu na wengine sio haramu,kwahiyo sio jambo ambalo lina msingi mmkubwa wa dini yetu,kifupi halina umuhimu wowote

Anyway natamani nijibu kila kitu lakini ni wastage of time kwa mada zisizo na mashiko kama hizi,kifupi mtoa mada hakijui alichoandika period
 
Kwanza tunawagawanya kisha tunawatawala, ni formula ya ukoloni na utawala wa kiimla. Kondoo ni wale wale tofauti rangi na mabanda. Chakushangaza wote adui wao ni shetani, ila hawampogi sheatani bali wao kwa wao; ideology moja tofauti ni cover za vitabu , kilichop ndani ni kilekike.
Waafrica tuko gizani sana. Tupeleke hizo fedha Italy, Maryland na kwa wasuka mifumo wengine at least ngwaj boy na wenzake wanatanulia hapa nchini. Mtu unatoa pesa shambani alafu unawapelekea taasisi za wauza maneno alafu ukuombe hii imekaaje kiuchumi huku wao tunawachangia magari n.k
 
Licha kuwa waislam ni wabinafsi na wabaguzi wa kidini hawana moyo wa shukrani na utoaji. Si watoaji kwa maendeleo yao, wanasaidiwa na waarabu wa nje kujenga misikiti. Bila misaada ya uarabuni hawajiwezi kujenga misikiti yenye majengo mazuri. Sadaka zao tu hutoa kidogo sana tofauti na wakristo hutoa sadaka nyingi. Wamisionari wa kizungu siku hizi hawapo sana, hivyo basi wakristo wenyewe huchangishana kufanya maendeleo yao wenyewe bila kutegemea wazungu wa mashirika ya kimisionari
 
Hakuna kabisa linalohesabu watu labda hayo ya kilokole yenye waumini wachache, hata yale type ya mwamposa hawahesabu
Lutheran mimi naabudu huko kila jumapili wanaposoma matangazo lazima wasome na mahudhurio ya ibada iliyopita hiyo ni lazima kama wanavyosoma jumla ya mapato ya wiki
 
Hii ndo mbinu yako mpya uliyokuja nayo ya kukabiliana na 9D kwa kuchochea utengano wa wakristo na waislamu?

Umefeli pakubwa.
Jana alikuja na ujinga wake tukampopoa mawe

Leo kaja kivingine tena
 
Back
Top Bottom