Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Mbona Mimi niliyesikiliza na kuona kichoonyeshwa au kuzungumzwa na Magoti sijaona alipo idhihaki na kuitusi dini yeyote Bali katumia upole na busara ya hali ya juu?

Naomba nikuulize maswali machache tu'
Hivi unaonaje watoto wako wanaokwenda shule uwaachishe shule wakasome hicho unachokitetea?

Mimi naona Africa tunachangamoto sana,
Walioleta dini Wana wanapambana na tunayoiita elimu Dunia ili wajikomboe wao na vizazi vyao...

Tafuta nchi ilizoshika dini nje ya Africa wananchi wao Wana maendeleo kiasi gani?

Dini inanafasi yake katika kumtafuta Mungu na kumjua vyema lakini sidhani kama kuna sehemu katika vitabu vya Imani kapiga marufuku elimu dunia....

MSHIKE SANA ELIMU NA USIMUACHE AENDE ZAKE
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Muislam atakayezua taharuki hapo hana akili mkuu, Mimi Muislam lakini sikubaliani na ule ujinga.
Someni dini muijuwe dini sio kusupport kipuuzi puuzi kisa tu aliyefanya ni Muislam
 
Huwa hamtaki kuambiwa ukweli na hamuachi kulialia.

DC yeye ameplay part yale, amesimama kwenye jukumu lake...haiwezekani aone watoto wa miaka mitatu kwa mitano wanaopaswa kuwepo nyumbani kwa wazazi wao wakisoma shuleni eti wanalala nje ya manyumbani kwao na kujipikilisha huko

Haiwezekani Asilani

Cry more !!!
Kwa nini aende usiku!?..tukimsema aseme tunamnyanyapaa
 
Dah sijui kwann nmecheka sana 😂 kuna mambo ht kama huna uhakika nayo ila ukiyasikia unabaki kucheka tuu
Kuna Ka historia wamekatengeneza siku hizi wanakazungusha mitandaoni kuhusiana na Ikulu na Ocean road hospital wakiaminishana vilikuwa ni vya Waislam na vilijengwa na wai, wakati lile jengo pale lilikuwa disigned na John Sinclair, na ndiye aliyesimamia ujenzi wake na ujenzi huo ulifanywa Waingereza mwaka 1922 baada ya jengo la awali lilikuwa limejengwa na wajerumani kuharibiwa na majeshi ya Uingereza.
German ndiyo walianza kuijenga Ikulu baada ya kuamua kuhamisha makao kutoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam, walichofanya ni kununua ardhi kutoka kwa Sultan basi na si majengo
 
Watangulizi wa Petro Magoti mbona hawakuleta taharuki hizi.

Wamepita ma DC, Mh Jokate mwegelo na Nikki wa pili wameishi vizuri tu na wana kisarawe ila yeye toka aje kisarawe amekuwa ni mtu wa kuzua taharuki.

Kwanza kaanza kwa kutoa matamko kuwa mabinti wa kizaramo wasichezwe, pikipiki zisitumike kubeba mkaa pikipiki ikikamatwa anaitaifisha , hajakaa vizuri kaja na haya
Acheni kulialia. Fuateni sheria.

Pili, achaneni na utumwa wa dini za wageni. Kuweni huru na utanzania wenu.
 
Kuna Ka historia wamekatengeneza siku hizi wanakazungusha mitandaoni kuhusiana na Ikulu na Ocean road hospital wakiaminishana vilikuwa ni vya Waislam na vilijengwa na wai, wakati lile jengo pale lilikuwa disigned na John Sinclair, na ndiye aliyesimamia ujenzi wake na ujenzi huo ulifanywa Waingereza mwaka 1922 baada ya jengo la awali lilikuwa limejengwa na wajerumani kuharibiwa na majeshi ya Uingereza.
German ndiyo walianza kuijenga Ikulu baada ya kuamua kuhamisha makao kutoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam, walichofanya ni kununua ardhi kutoka kwa Sultan basi na si majengo
Bwana wewe..
Ukipita viambaza vya buguruni, tandale,mbagala, magimeni na uswazi kote.
Huwaambii kitu kuhusu hizo stori watakuwekea cd za kina mazinge na wenzake
 
Brother ukiwa unatoa maandiko punguza mhemko wako kwanza, maja ya maandkiko unasema shekhe wa msikikiti alisema hao watoto wanaishi dharura hapo wakat wao wanajiandaa kujenga mabwen, kwel unaweza kuweka watoto wa watu wa dharura?? Sasa hapo mkuu wa Wilaya kosa lake nn?? Amajeli kwanza maisha ya hao vijana, cha msingi jengeni hayo mabwen then muone kama kutakuwa na changamoto tenaa
 
Angeenda mchana angejuaje watoto wanalazwa kama mafungu ya nyanya.hivyo ndio sawa ili aone ukubwa wa tatizo.
Mkuu wa wilaya ni mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani,ana vyombo vya kumpa taarifa,hakuota Bali vyombo vilimpa taarifa ndiyo akavamia usiku,yaani kiki kupitia dini ya watu,ajirekebishe
 
Watangulizi wa Petro Magoti mbona hawakuleta taharuki hizi.

Wamepita ma DC, Mh Jokate mwegelo na Nikki wa pili wameishi vizuri tu na wana kisarawe ila yeye toka aje kisarawe amekuwa ni mtu wa kuzua taharuki.

Kwanza kaanza kwa kutoa matamko kuwa mabinti wa kizaramo wasichezwe, pikipiki zisitumike kubeba mkaa pikipiki ikikamatwa anaitaifisha , hajakaa vizuri kaja na haya
STIKI KATIKA POINT MOJA, TUKUELEWE. Acheni kukusanya watoto wadogo na kuwafungia muda wote ili kuwafunza misimamo yenu, acheni akili zao zipevuke, acheni wafaidi malezi ya wazazi wao (hata kama maisha magumu ipo siku hayo maisha magumu yanakuwa trigger ya wao kutafuta zaidi).
 
Petro anashida na waislam pamoja na tamaduni za watu wa pwani. Atakipata kile anachokitafuta
Ukiwa mtetezi wa watoto una nafasi kubwa sana ya kubarikiwa na Mungu. Tenda wema kwa watoto na ulinzi wa Mungu utakuwa nawe siku zote.
 
Back
Top Bottom