KUMBE NDIO UJINGA MNAOJAZWA MSIKITINI MASIKINI.
DINI NI NENO LA KIARABU LENYE MAANA YA NJIA.
Naomba nikuthibitishie kuwa UKRISTO SIO DINI ni MATENDO MEMA ya Kumfuata Yesu kristo,mwana WA MUNGU ALIYE hai aliyekuja kufanya upatanishi kati yetu na Mungu Baba yake. ( UKRISTO NI Ufuasi kuwa mfuasi wa Yesu kristo)
Katika kutenda sawa sawa na Yoote aliyoagiza
Kwa mujibu wa tafsiri wewe DINI YAKO NI YESU?
KRISTO NI JINA LA YESU. Kwa mujibu wa bibilia.
YOHANA 4:25-26.
25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
UKRISTO NI KUJISALIMISHA NA KUNYENYEKEA MBELE ZA MUNGU KWA KUFUATA MAFUNDISHO YOTE ALIYOMTUMA YESU KRISTO.
Huu ndio huwo ukafiri, maana ktk bibilia yenyewe hata hilo nene tu
UKRISTO halipo.
Kama lipo lete hilo andiko linalitaja tu
ukristo, hadi wewe utoe hio masna ya kuwa ukristo ni kunyenyekea mbele za Mungu.
YOHANA 14: 6
Mimi ndimi njia na kweli na Uzima mtu haji kwa Baba ila mimi.
Kama kweli Yesu ndie njia ya kweli na Uzima basi Lazima ni mfuate kwa sababu alifia dhambi ya Ulimwengu.
LAANA ya Adamu pale edeni.
Dhambi AMBAYO Ulimwengu mzima tulilaaniwa kupitia Adamu.
Sema wewe ulilaaniwa, sisi wailamu hatujalaaniwa.
KUMBU² LA TORAT. 24:16
16 Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.
Kama hiyo haitoshi:-
EZEKIELI. 18:20.
20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
Litambue hilo, wailamu kila mmoja kwa nafsi yake.
WARUMI 8:9.
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wa kristo.
MANABII WALIKUWA NA ROHO WA KRISTO.
1PETRO 1:10.
Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
HAPA NDIPO WALIOKUBALI KUMFUATA MAFUNZO YA YESU WANAITWA WAKRISTO.
hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
Matendo ya Mitume 11:26
NINYI WAISLAMU HAMNA ROHO WA MUNGU.
HAMNA ROHO WA YESU KRISTO.
Ni kweli, sisi waislamu tuna roho ya mundu bali tuna roho/nafsi na mwili aliotupa Mungu ili kusudi tumuabudu na kumsujudia yeye. Yesu ana nafsi yake na mwili wake.
Quran INASEMA WAISLAMU HAMJUI mambo ya Roho.
Na wakikkuuliza mambo ya Roho sema hatuujui mambo ya Roho.
Ni kweli. Wewe ujuwae mambo ya roho, unaijua kesho yako itakuaje?
Na kwa 7bu Yesu ni Muislamu ndio maana nayeye pia hajui kila kitu.
24:36. MATHAYO.
36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Waislamu kama Yesu tu, sio kila kitu wanajua.
QURAN INATUAMBIA WALE WALIO AMINI NI WA KRISTO.
Wewe ni kafiri kama ulivyosema mwenyewe kwa mujibu wa bibilia na andiko ukatoa. Tazama unavyopotosha manene ya Allah kwa faida yako binasfi.
Quran 2:62 - Hakika Walio amini, ni Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
Sura ya 2 aya ya 62 iko hivi.
QUR-AN. 2:62.
62. Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
Huyu kafiri alichokifanya ni kuondoa na ktk aya ya Qur-an akabadili akaweka ni. Kwa ukafiri wake, akiwa anajua ya kuwa ukiwa mkristo, myahudi au msabani ukijua haqi na kuifuata hiyo haki wewe ndio unakuwa muislamu/mnyenyekevu.
Hakuna kafiri awezae kuibadilisha Qur-an. Hiyo ni ahadi ya Mungu kwa kafiri yeyeote.
UKRISTO SIO KIBOKSI NI MATENDO MEMA SAWASAWA NA YESU KRISTO WA NAZARETH.
3:13. WAGALATI.
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Ni Kristo huyu huyu au yupi?
Alie laaniwa na Mungu anaenda wapi?