Waislamu; kwanini Adamu mnamwita Nabii, kwani alitenda unabii gani?

Waislamu; kwanini Adamu mnamwita Nabii, kwani alitenda unabii gani?

Nabii Kwa wakati wa zama zake.na ndio binadamu wa kwanza
 
Ukisoma Quran hususani Surah Al-Baqarah (2), Al-A'raf (7), and Al-Isra (17), habari ya Adamu na maisha yake kwa ujumla zinazungumziwa humo.

Adamu alikuwa na Mke mmoja tu aliyetajwa kwenye Quran, naye ni "Hawwa", na watoto wao waliotajwa ni Wawili tu ambao ni "Habil" wakristo umuita "Abel" na "Qabil" ambaye wakristo umuita "Cain" au Kaini kwa Kiswahili.

Quran imezungumzia maisha yote ya Adam kama Biblia ilivyoelezea. Vilevile Quran ikaelezea kisa cha Adam na Hawwa kula Tunda la mti wa kati lilizaa dhambi za hivi sasa. Japo Biblia anasema aliyeanza kudanganywa ni Hawwa, ila Quran inasema Shetani aliwadanganya wote kwa pamoja.

Tukija kwenye Maana ya UNABII

"Unabii maana yake ni ufunuo wa kimungu unaotolewa na Mungu kwa nabii ili awaongoze watu kwa haki, kuwafundisha maadili mema, na kuwaonya dhidi ya maovu"

Je ni kwenye Surah gani ya Quran, Adam alitenda unabii kwa mujibu wa maana ya unabii?


Mangi Meno soma hapa, unaweza kupata majawabu yako
 
Kama yapi unakusudia? Ikiwa sisi tunaamin ya kuwa issa ( yesu) ni mtume wa allah na alipewa injili ambayo ilikuja kupotoshwa baadae na ndugu paulo na nyinyi munaamin kuwa yesu ni mungu/ mtoto wa mungu ( allah ametakasika na hilo) sasa itakuwaje iwe hakuna tofauti?
Tupeni hyo iliyopotoshwa na km imepotoshwa mbona maifanya rejea kwenye Quran na unabiibwa muhamad?
 
Uislamu haufuati biblia so ustaki kila unacho amin wewe kwenye biblia na waislamu waamin hvyo, na huyo samson ni nani? Katajwa kwenye kitabu gani cha waislamu?
لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ ﴿٦﴾

6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
Huo ni msimamo wako wewe binafsi na si uislam na qurani . QURANI INA AMINI KTK BIBLIA ASILIMIA MIA.

Yunus 10:94 "basi waulize waluopata kitabu(biblia) kabla yako....."


Uislam haumini katika biblia huo uislam umekuaje uislamu????????
 
Mtume ni wale waliopewa vitabu.

Manabii ni wale hawakuwa vitabu.

Nabii Ibrahim, Musa, Yesu Muhamad nk

Manabii hao wengine

Yona
Zakaria
Adam

Mitume na manabii walikuja na ujumbe mmoja.

Unyenyekevu


Halafu wakaja wapotoshaji, wakapandikiza upagani juu ya imani ya Mitume na Manabii kwa mfano Mr Paulo.

Ujumbe ulioletwa na Mitume na Manabii si kwenda mbinguni. Mbingu ni matokeo.

Ujumbe wao ulikuwa Dunia ni koloni la Mungu na mitume na manabii ni magavana wa Mungu. Na kwamba wako hapa duniani si kutupeleka watu mbinguni bali wapo kwa ajili ya kuuondoa utawala wa kibinadamu na kusimika utawala wa Mungu kwa kufata sheria zake.

Mtume Muhamad alifanikiwa ktk hilo, Mtume Yesu alifeli.

Prof Paulo nae alishinda kuwapeleka wafuasi ktk upagani.

Kwahiyo kwa kujibu wa uislamu hata Mimi ni nabii kwenu maana Sina kitabu chochote.
 
Kwahiyo kwa kujibu wa uislamu hata Mimi ni nabii kwenu maana Sina kitabu chochote.
Muhimu:
Kila Mtume ni Nabii. Lkn si kila Nabii ni Mtume.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Quran, Utume na Unabii ulihitimishwa na Nabii na Mtume wa Mwisho Muhamad ﷺ meaning Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe Juu yake.

Quran 33:40 Muhammad si Baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Hivyo yyt atakaejipambanua au kufikiri yeye ni nabii au mtume.

Hao ni kina Vibwetere nani mabomu yanayosubiri kuuwa watu

 
Kuuliza jambo JF sio vibaya ila kwa minajili ya kujifunza dini huwezi kupata majibu hapa JF. Kama uko serous tafuta hata sheikh atakusaidia pale ulipokwama

Ila kwa kukusaidia endelea kusoma hiyo hiyo Quran utapata majibu ya maswali yako yote uliyo nayo. Kama hujapata majibu kwa mara ya kwanza rudia tena kuisoma, nakuhakikishia utapata majibu ya maswali yote uliyo nayo.

Quran ni kitabu cha kipekee sana, kinaeleweka kwa urahisi kabisa.
Quran ndio kitabu cha ovyo nimewahi kukiona hapa duniani

Kwanza kabisa, Qur’an haifati mpangilio wa kihistoria au wa kimantiki kama ilivyo kwa vitabu vingi vya dini au elimu. Kwa mfano, sura ya Al-‘Alaq ambayo inasadikika kuwa ndiyo yenye aya za kwanza kabisa kushushwa kwa Mtume Muhammad haipo mwanzoni mwa Qur’an, bali iko karibu na mwisho wake kama sura ya 96 kati ya 114.

Hili linathibitisha kuwa mpangilio wa Qur’an si wa mfululizo wa kihistoria (chronological order), bali ni wa aina nyingine ambayo si rahisi kufuatilia bila msaada wa vyanzo vya nje kama Hadith au tafsir.

Vilevile, Qur’an haina mtiririko wa kimantiki wa matukio au hoja.

Kwa mfano, unaweza kukutana na aya zinazozungumzia Nabii Musa katika sura moja, kisha zikakatizwa ghafla na maelezo ya mambo mengine yasiyohusiana kabisa, kisha zikarudi tena kwa Musa katika sura nyingine baadaye bila muendelezo wa moja kwa moja.

Hii inaonyesha kutokuwepo kwa muundo wa simulizi wa kawaida ambapo tukio moja hufuata jingine kwa mtiririko wa maana.,Ni wazi Muhammad alikuwa anaokotaokota visa huku na kule,.

Hata masimulizi ya kihistoria ndani ya Qur’an hayaweki matukio kwa mfuatano bali yanaruka ruka sehemu mbalimbali na kurudiwa mara kwa mara, hali inayoashiria kutokuwepo kwa coherent narrative sequence.

Kwa upande mwingine, mpangilio wa sura ndani ya Qur’an hauzingatii hata urefu wala maudhui yanayofanana. Sura ndefu kama Al-Baqarah ziko mwanzo wa Qur’an, lakini sura fupi sana kama Al-Kawthar au Al-Ikhlas ziko mwishoni.

Hakuna mantiki ya kihistoria, kielimu, wala kimaudhui inayoweza kueleza mpangilio huo kwa msomaji wa kawaida.

Kwa mtu anayetarajia utaratibu kama wa vitabu vya dini vya Kiyahudi au Kikristo ambavyo vina historia ya mfululizo Qur’an huonekana kama mkusanyiko wa sehemu mbalimbali zisizopangwa kwa mtiririko unaoeleweka kwa urahisi.

Quran inakosa chronology, logical sequence, na thematic order katika mpangilio wa sura na aya.

Msomaji wa nje ya Uislamu au hata Mwislamu asiye na maarifa ya tafsir, Hadith na historia atalazimika kuomba msaada wa nyongeza kuelewa Qur’an, kwa sababu haitoi mwongozo wa mfululizo wala muktadha kamili wa masimulizi yake ndani ya kitabu chenyewe.
 
Huo ni msimamo wako wewe binafsi na si uislam na qurani . QURANI INA AMINI KTK BIBLIA ASILIMIA MIA.

Yunus 10:94 "basi waulize waluopata kitabu(biblia) kabla yako....."


Uislam haumini katika biblia huo uislam umekuaje uislamu????????
Biblia inayoaminiwa na qur an ni ile iliteremshwa kwa issa sio hii yenu ambayo haijulikani halisi ni ipi? Kwann nyote ni wakristo halafu muna biblia tofauti halisi ni ipi? Iweje uislamu uamin asilimia 100 dini ambayo haina kitabu maalumu kila mtu anajiamulia tu mara yesu mungu wengine mtoto wa mungu tunaamin vpi? We ushawah kusikia et kuna qur an tofaut toka uzaliwe?
 
Tupeni hyo iliyopotoshwa na km imepotoshwa mbona maifanya rejea kwenye Quran na unabiibwa muhamad?
Et rejea? Hebu taja sehemu moja tu kwenye qur an ambayo imerejea iwe kwenye biblia ya wasabato au waroma maan nyiny wenywe kila mtu na biblia yake sijui hata sahihi ni ipi 🤣 ila ukija kwenye uislamu pamoja na tofaut zetu qur an ni moja tu ولله الحمد
 
Ktk maisha nimegunduwa kwamba sometimes kubishana na mtu asiyejuwa kitu, kunampa faida ya kujifunza kupitia mabishano yako.
Ni vyema mtu kama hajui jambo aje straight aelekezwe kuliko kuja Kwa style ya kubishana ili ajifunze kutokana na mabishano yako..

Adam ni Mtume wa MUNGU ,na sio lazima Mtume wa MUNGU kufanya miujiza...
Kwanza jifunze kutofautisha kati ya Mtume na Nabii... Hawa ni watu wawili tofauti, pili jifunze kuelewa kwamba mimi nimezungumzia nabii
 
Back
Top Bottom