tafsiri iko sahihi, mtu anaweza kupigana na nafsi yake maana inaamrisha mambo machafu na mabaya, pia huweza kufanya jihad kwa mali yake akachangia dini iende mbele na pia huweza kufanya jihad ya vita sasa na hii ina masharti mengi na kuhitajia kusoma sana bali ina hatua zake na ni hatua ya mwisho kabisa na inahitaji amri ya kiongozi, sio huo upumbavu wa hao vijana wa alshabaab, boko haram, ISIS, alqaedah na wengineo hawa ni wahuni tu na ukichunguza kuna mkono wa US kuvitumia vikundi hivyo kuvuruga amani ya maeneo husika na kuutukanisha uislamu.
Jiulize silaha wanapata wapi? mwisho kwenye uislamu hairuhusiwi kujitoa uhai, na vigezo vya vita vikitimia hairuhusiwi kuua wanawake, watoto wala kukata miti na kuharibu visivyohusika na vita.