Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
- Thread starter
- #141
Jina la Tanzania limeanza 1964 sio Tanzania imeanza 1964…siku hizi shule huwa mnajifunza nini ?
kwa hiyo mimi nikisema nimezaliwa Dar es salaam nakuwa Muongo kwa kuwa nimezaliwa kabla ya huu mji kupewa jina la Dar es salaam?
kwa hiyo tukisema wageni walivamia Pwani ya Tanganyika tangu 1490 tunakuwa waongo kwa kuwa wakati huo hili eneo lilikuwa haliitwi Tanganyika?
Na hapo ndipo shida ilipo, nchi yetu kama tuijuavyo leo hii kwa mipaka ya Kijiografia ilihusisha Rwanda na Burundi ya leo yote iliitwa German East Afrika, hivyo unatumia kigezo gani kusema familia ya Nyerere au Magufuli hawana asili ya Tanzania kama Rwanda na Burundi zote tulikuwa nchi moja?