Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Hapana hii inategemea. Madrasa zetu nyingi hazitilii mkazo katika kujifunza lugha ya Kiarabu. Zile ambazo zinafundisha Kiarabu hazifundishi kwa undani sana.

Ila ukitaka uijue Dini ya Kiislamu vizuri lazima usome Kiarabu na ukijue. Hii inataka muda na juhudi kubwa.

Qur'an ni muujiza ndio maana mtu yoyote ambaye hakijui Kiarabu anaweza kuihifadhi Qur'an na akaisoma kwa ufasaha, hata akiwa hajui maana yake. Kwa vitabu vingine hili ni muhali.

Jee hamuoni haja ya kubadili mfumo mzima wa dini ya kiislamu uwape watu uhuru wa kuabudu kwa lugha yao? Badala ya kung'ang'ania ibada lazima ifanyike kwa lugha ya kiarabu.
 
Bado sijaelewa unatofautisha vipi Kiarabu na lugha iliyoandikwa quran,
Yoda,
Kiarabu kinazungumzwa sehemu nyingi sana katika bara la Arabia, na kila sehemu huwa wana lafdhi zao, na pengine huwa na maana tofauti katika utumiaji wa maneno fulani. Kiarabu cha Qurani ni fasaha(fus-ha). Ni kama kiswahili kinavyozungumzwa na watu tofauti ambacho kina lahaja zisiopungua 15.
 
Bro kama naleta siasa. Jifanye jeuri au jitoe ufahamu kwa kuswali swala 5 kwa lugha yako ya kiswahili au ya kabila lako.
si ndo siasa zenyewe hizo mkuu, kwa msingi huu unaosema wewe mtu yeyote akitukana kwa lugha tofauti na kiarabu hakuna tatizo maana haeleweki kama katukana
 
Quran imeandikwa kiarabu ila kiarabu si Quran maandishi ya kiarabu yanatofautiana na ya kwenye Quran kwa kuwa huwa hayana irabu(aeiou) kwa hyo anaesoma Quran tupu hawez kusoma kiarabu unless amesoma kiarabu ama kwa lugha nyingine kiarabu kinasomwa kwa kujua maana na muundo wa maneno.
Kwa hiyo kwenye kirani kuna mixer ya lugha?!
 
Rudien kusoma post za Abdulrahman Said nadhan mjadala kaufunga.
Hajaufunga mjadala, hapa tena inasemwa kuna waumini wengi tu wanajua surat au aya za quran lakini ukiwambiaa wakuelezee maana yake hawajui! Mimi siku zote nimekuwa nafikiri wale wanaohifadhi Quran wanaelewa kila wanachonukuu kumbe sivyo.
 
Kiarabu ni lugha yetu sisi Waislamu na tunajivunia sana.

Sababu kama unataka kuijua dini ya Kiislamu vizuri ni lazima ujifunze lugha ya Kiarabu.

Lakini, kingine hakuna lugha ambayo imehudumiwa na kuhifadhiwa vizuri sana kuzidi lugha ya Kiarabu. Hapa tuweke mapenzi pembeni.

Nimecheka kwa sauti
😛 😛😛
Yaani wewe mmatengo wa mbinga ujivunie kiarabu. Je waarabu watasemajee?

Kweli kabisa waarabu wamefanikiwa kuwateka watu na kuwafanya watumwa wao.
Sasa nimeamini kabisa ya kwamba uislam ni chombo au mjango malidhawa kabisa wa kueneza tamaduni, mila na desturi za kiarabu.
 
Majibu yashatolewa kote unless tu hujasoma, Mkuu mngoni ametoa Majibu mazuri tu.

Quran inatokana na Fus'ha classical Arabic ya wakati huo, kama huyo sheikh alivyokwambia ila kuifanya iwe rahisi kusomeka na hata wasio kuwa waarabu yakatumika maandishi rahisi kuyasoma yakawekwa irabu na viashiria vingine kMa hapa uvute, hapa ukaze etc.

So ni rahisi kusoma Quran hata kama sio mwarabu, binafsi naweza kusoma Quran ila Kiarabu mpaka nikaze sana na maneno mengi yatanishinda.

Hili ni shairi la kiswahili ambalo lime tumia Lugha ya kiarabu cha kwenye Quran kuandika

View attachment 3168671
Unaona hivyo mistari vimepita juu na chini? Hizo ni irabu na alama nyengine kukusaidia kusoma,

Ila kiarabu chenyewe kinakua kama hivi
View attachment 3168673

So kiarabu cha Quran hata wewe ukipigwa msasa wiki tu unaweza kuanza kusoma, ila kiarabu chenyewe inabidi ukae darasani kujifunza.
Kwa maana nyingine kiarabu cha kwenye Quran sio kiarabu cha mawasiliano kama lugha rasmi katika enzi hizi? Yani mfano watu wawili wakisoma Quran tu vizuri wakailewa bila kujifunza kiarabu cha nje ya Quran hawawezi kuzungumza kiarabu katika mazungumzo ya kawaida hata broken??
 
Kuna elimu ya lugha ya kiarabu ambayo wanafunzi huwa wanapatiwa sasa ni juhudi za mtu mwenyewe kujiendeleza ndani zaidi lugha ya kiarabu ni lugha tajiri na ni lugha kubwa mnoo inahitaji muda miaka na miaka ili kufikia kujiita gwiji wa lugha ya kiarabu , ambacho hamkijui tu hata waarabu wenyewe kiarabu kinawashinda.

Kingine kama mtu hakusoma kabisa kiarabu ila akasoma tu quran pamoja na kujiendeleza labda hadith , fiqih n.k anakuwa kiarabu chake kwanza ni kigumu kwa sababu maneno ambayo ameyakariri mengi ni ya kwenye quran ( kumbuka quran kiarabu chake ndiyo original haswaa na ni cha kale kweli kweli) hivyo kuzungumza na waarabu kidogo itamletea shida.
 
Kiarabu ni lugha pana sana kuliko lugha zote duniani. Wanaweza na pia hawawezi.

Mfano mzuri ni Kiswahili, cha Zanzibar na cha Tanganyika kuna tofauti zake za matamdshi na hata maneno. Kiarabu ni vivyo hivyo kwa kila kinapotumika.

Hapo juu kwenye wino mzito. Tunaomba uthibitisho au cite authority.
 
Hakuna tatizo kukariri Qur'an bila kuielewa
Ila ni mbora ambaye ameikariri Qur'an na kuielewa na kuifanyia kazi na kuifundisha
Kiarabu kama mtu anapojifunza lugha nyingine yoyote uelewa wa watu uko tofauti wengine wanazungumza kiufasaha zaidi wengine wanajitahidi
Mkuu unaona ni sawa kukariri tu bila kuelewa kilichoandikiwa ni nini??
 
Unapoenda madrasa hauendi kujifunza lugha ya kiarabu unaenda kujifunza quruwani iliyoandikwa kwa lugha ya kiarabu cha asili ya wakureshi.

Maustadhi wengi wanachokifanya ni kuwakaririsha sura mbalimbali za quruwani hao vijana wanaoenda madrasa kujifunza quruwani sambamba na kuwakaririsha tafsiri ya baadhi ya aya zinazopatikana kwenye hizo sura walizofunzwa na maustadhi wao.

Kuhusu lugha ya kiarabu maustadhi hawafundishi lugha kwa maana ya muundo bali wanafundisha kwa kuwakaririsha wanafunzi wao baadhi ya maana ya maneno ya kiarabu mfano gari,nyumba,mti n.k, namba zinavyotamkwa na kuandikwa kiarabu, namna ya kujitambulisha kwa kiarabu, n.k.

JE UKISOMA MADRASA UTAWEZA KUONGEA KWA UFASA LUGHA YA KIARABU?

JIBU NI HAPANA HAUTAWEZA KUONGEA KWA UFASAHA LUGHA YA KIARABU MPAKA UJIFUNZE LUGHA YA KIARABU.

KWA KUWA UTAKUWA FAMILIA NA BAADHI YA MANENO YA KIARABU NAMNA YANAVYOTAMKWA NA KUANDIKWA UNAWEZA KUANDIKA MANENO KADHAA KWA KIARABU MFANO: MAMA,BABA,MJOMBA N.K ILA KUUNDA SENTENSI KAMILI HAUTAWEZA MILELE.
 
Kwa maana nyingine kiarabu cha kwenye Quran sio kiarabu cha mawasiliano kama lugha rasmi katika enzi hizi? Yani mfano watu wawili wakisoma Quran tu vizuri wakailewa bila kujifunza kiarabu cha nje ya Quran hawawezi kuzungumza kiarabu katika mazungumzo ya kawaida hata broken??
Ndio, japo kama wengine walivyo sema ukitaka kujua Quran/uisilamu in deep ni lazima kujua Kiarabu.
 
Unachotakiwa kufahamu! Lugha ya kiarabu ina lahaja nyingi kama Maghreb, hasaniyya, egyptian, syrian, na kadha wa kadha. MSA ni standardized version ya kiarabu hata natives wengi (isipokuwa wasomi) pia hawaongei ijapokuwa kwa kiasi flani mnaweza kuelewana, na ukienda nchi zinazozungumza kiarabu only wale educated ndo unakuta wanazungumza MSA.
Kuna classical arabic, msa na colloquial (hii sasa ndo inayozungumzwa na iko tofauti kulingana na eneo hapa ndo unakutana na hizo hassaniyya, maghrebi, egyptian etc).
Pale madrasa wengi hufundisha MSA (Modern Standard Arabic) ijapokuwa kwa namna flani ni rahisi kuelewa classical Arabic baada ya kusoma MSA and vice versa. Kusoma MSA haimaanishi kwamba wewe utakuwa rahisi kwako kuwasiliana na native Arabic speaker, kwasababu utkuwa na misamiati anatumia huijuwi na halikadhalika kuna misamiati unatumia yeye haijuwi
Ninachofahamu mtu anayefahamu lugha classical inakuwa rahisi zaidi kuelewa version ya lugha ya kisasa/modern, kwa hiyo kama Quran inafundishwa katika classical Arabic ilipaswa kujua Modern Standard Arabic(MSA) iwe jambo rahisi zaidi kwa walioilewa quran.
 
Ndio, japo kama wengine walivyo sema ukitaka kujua Quran/uisilamu in deep ni lazima kujua Kiarabu.
Kama ndivyo ilivyo basi wewe ndio utakuwa umeufunga huu uzi.
 
Back
Top Bottom