Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

“Jifunzeni Kiarabu na wafundisheni watu kwa sababu ni sehemu ya dini yenu.”

Kiarabu siyo sehemu tu ya dini yako, bali ni nguzo ya uislam. Kwa ufupi No kiarabu No uislam.
 
Naam wapo wengi sana. Na wapo ambao hawajui Kiarabu lakini wanasioma Qur'an vizuri mno.

Suala zuri sana. Wanasoma na kwa ufasaha. Lakini je wanasoma na kuelewa?
 

Jee hamuoni haja ya kubadili mfumo mzima wa dini ya kiislamu uwape watu uhuru wa kuabudu kwa lugha yao? Badala ya kung'ang'ania ibada lazima ifanyike kwa lugha ya kiarabu.
 
Bado sijaelewa unatofautisha vipi Kiarabu na lugha iliyoandikwa quran,
Yoda,
Kiarabu kinazungumzwa sehemu nyingi sana katika bara la Arabia, na kila sehemu huwa wana lafdhi zao, na pengine huwa na maana tofauti katika utumiaji wa maneno fulani. Kiarabu cha Qurani ni fasaha(fus-ha). Ni kama kiswahili kinavyozungumzwa na watu tofauti ambacho kina lahaja zisiopungua 15.
 
Bro kama naleta siasa. Jifanye jeuri au jitoe ufahamu kwa kuswali swala 5 kwa lugha yako ya kiswahili au ya kabila lako.
si ndo siasa zenyewe hizo mkuu, kwa msingi huu unaosema wewe mtu yeyote akitukana kwa lugha tofauti na kiarabu hakuna tatizo maana haeleweki kama katukana
 
Kwa hiyo kwenye kirani kuna mixer ya lugha?!
 
Rudien kusoma post za Abdulrahman Said nadhan mjadala kaufunga.
Hajaufunga mjadala, hapa tena inasemwa kuna waumini wengi tu wanajua surat au aya za quran lakini ukiwambiaa wakuelezee maana yake hawajui! Mimi siku zote nimekuwa nafikiri wale wanaohifadhi Quran wanaelewa kila wanachonukuu kumbe sivyo.
 

Nimecheka kwa sauti
😛 😛😛
Yaani wewe mmatengo wa mbinga ujivunie kiarabu. Je waarabu watasemajee?

Kweli kabisa waarabu wamefanikiwa kuwateka watu na kuwafanya watumwa wao.
Sasa nimeamini kabisa ya kwamba uislam ni chombo au mjango malidhawa kabisa wa kueneza tamaduni, mila na desturi za kiarabu.
 
Kwa maana nyingine kiarabu cha kwenye Quran sio kiarabu cha mawasiliano kama lugha rasmi katika enzi hizi? Yani mfano watu wawili wakisoma Quran tu vizuri wakailewa bila kujifunza kiarabu cha nje ya Quran hawawezi kuzungumza kiarabu katika mazungumzo ya kawaida hata broken??
 
Kuna elimu ya lugha ya kiarabu ambayo wanafunzi huwa wanapatiwa sasa ni juhudi za mtu mwenyewe kujiendeleza ndani zaidi lugha ya kiarabu ni lugha tajiri na ni lugha kubwa mnoo inahitaji muda miaka na miaka ili kufikia kujiita gwiji wa lugha ya kiarabu , ambacho hamkijui tu hata waarabu wenyewe kiarabu kinawashinda.

Kingine kama mtu hakusoma kabisa kiarabu ila akasoma tu quran pamoja na kujiendeleza labda hadith , fiqih n.k anakuwa kiarabu chake kwanza ni kigumu kwa sababu maneno ambayo ameyakariri mengi ni ya kwenye quran ( kumbuka quran kiarabu chake ndiyo original haswaa na ni cha kale kweli kweli) hivyo kuzungumza na waarabu kidogo itamletea shida.
 
Kiarabu ni lugha pana sana kuliko lugha zote duniani. Wanaweza na pia hawawezi.

Mfano mzuri ni Kiswahili, cha Zanzibar na cha Tanganyika kuna tofauti zake za matamdshi na hata maneno. Kiarabu ni vivyo hivyo kwa kila kinapotumika.

Hapo juu kwenye wino mzito. Tunaomba uthibitisho au cite authority.
 
Mkuu unaona ni sawa kukariri tu bila kuelewa kilichoandikiwa ni nini??
 
Unapoenda madrasa hauendi kujifunza lugha ya kiarabu unaenda kujifunza quruwani iliyoandikwa kwa lugha ya kiarabu cha asili ya wakureshi.

Maustadhi wengi wanachokifanya ni kuwakaririsha sura mbalimbali za quruwani hao vijana wanaoenda madrasa kujifunza quruwani sambamba na kuwakaririsha tafsiri ya baadhi ya aya zinazopatikana kwenye hizo sura walizofunzwa na maustadhi wao.

Kuhusu lugha ya kiarabu maustadhi hawafundishi lugha kwa maana ya muundo bali wanafundisha kwa kuwakaririsha wanafunzi wao baadhi ya maana ya maneno ya kiarabu mfano gari,nyumba,mti n.k, namba zinavyotamkwa na kuandikwa kiarabu, namna ya kujitambulisha kwa kiarabu, n.k.

JE UKISOMA MADRASA UTAWEZA KUONGEA KWA UFASA LUGHA YA KIARABU?

JIBU NI HAPANA HAUTAWEZA KUONGEA KWA UFASAHA LUGHA YA KIARABU MPAKA UJIFUNZE LUGHA YA KIARABU.

KWA KUWA UTAKUWA FAMILIA NA BAADHI YA MANENO YA KIARABU NAMNA YANAVYOTAMKWA NA KUANDIKWA UNAWEZA KUANDIKA MANENO KADHAA KWA KIARABU MFANO: MAMA,BABA,MJOMBA N.K ILA KUUNDA SENTENSI KAMILI HAUTAWEZA MILELE.
 
Ndio, japo kama wengine walivyo sema ukitaka kujua Quran/uisilamu in deep ni lazima kujua Kiarabu.
 
Ninachofahamu mtu anayefahamu lugha classical inakuwa rahisi zaidi kuelewa version ya lugha ya kisasa/modern, kwa hiyo kama Quran inafundishwa katika classical Arabic ilipaswa kujua Modern Standard Arabic(MSA) iwe jambo rahisi zaidi kwa walioilewa quran.
 
Ndio, japo kama wengine walivyo sema ukitaka kujua Quran/uisilamu in deep ni lazima kujua Kiarabu.
Kama ndivyo ilivyo basi wewe ndio utakuwa umeufunga huu uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…