Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Kingereza ni lugha ya kufundishia secondary mpaka chuo kikuu, kwa hiyo ni rahisi watu wengi kukijua. Kiarabu sio. Ila wakristo wanatumia biblia za kiswahili na hata za lugha za makabila mbalimbali. Waislamu badala kujikita kufunisha Quran kwa kiswahili wao wanamezeshwa bila kujua maana yake. Mtu kahifadhi Quran nzima bila kujua maana yake, huyo ana tofauti gani na ambaye hajahifadhi?
Quran inatakiwa ifundishwe na watu waielewe lakini hili halifanyiki.

Qur'aan imehifadhiwa na imelindwa, haiwezi kufikiwa na batil au corruption. Hivyo atakayejifunza ni lazima asomeshwe vilevile ilivyo. Atakayeisoma ataisoma vile vile. Atakayeihifadhi ataihifadhi vile vile.

Tarjama za lugha ya Kiswahili, Kiingereza na lugha nyengine sio Qur'aan ni tarjama tu za maana ya Qur'aan.

Halafu una uhakika watu hawasomeshwi kuielewa Qur'aan?

Na wapo watu wengi wamehifadhi Maneno ya Allah na wengine wanaielewa na bado hawawezi kuzungumza kiarabu. Huu ni Muujiza wa Qur'aan. Ni rahisi kuweza kuisoma na kuihifadhi Qur'aan, lakini pia ni rahisi Qur'aan kumponyoka mtu iwapo atakuwa haizingatii katika kuisoma na kuirudia rudia.

Halafu usiseme wanamezeshwa, bali wanahifadhi Maneno ya Mola Mlezi wa kila kitu. Jambo bora lilioje hilo! Kuisikiliza tu Qur'aan kuna fadhila, kuisoma kuna fadhila, sikuambii kuihifadhi kifuani, sikuambii kuielewa, sikuambii kuifanyia kazi na kuiishi. Qur'aan ni Maneno ya Allah, Mola Mlezi wa Viumbe vyote.

Ila kujifunza Lugha ya kiarabu ni muhimu mno katika kujifunza Dini ya Uislam na kuifahamu vizuri.
 
Nao pia watajua cha kusema. Ila sisi tunajivunia Kiarabu.

Hapo hakuna utumwa labda hujui nini maana ya utumwa. Tunajifunza Kiarabu kwa ajili ya kujifunza dini yetu ya Uislamu.

Hujui Uislamu kadhalika Wala Uarabu, tamaduni ngapi za Kiarabu, Uislamu umekuja kuzikemea na kuzikataza ?

Kitu ambacho kinakera humu jf, ni watu kujadili mambo ambayo hawana elimu nayo.

Mchezo huu hauhitaji hasira. Hizo hisia za kwamba uislam si uarabu ni watu wachache sana mlio nazo. Wenzenu wengi wanaona waarabu ni watu wa peponi. Na ndiyo maana ili ukubalike na Mola lazima ujue kiarabu. Hivyo ni ngumu sana kuutenganisha uislam kutoka ndani ya uarabu. Mtakataa nabkuruka ruka huku na kule, lakini ukweli unabaki ule ule, uarabu ndiyo nguzo ya uislam. Ndiyo maana bila kuongea maneno ya kiarabu wakati mnamuomba allahu wenu swala haiswili.
 
Wewe
Kwanza Kiarabu ni lugha kama zilivyo Kiswahili, Kiingereza n.k
Kiarabu sio Kiislam bali ni lugha iliyotumika kushushiwa Quran.

Hivyo basi, wapo wanaokielewa Kiarabu vyema kabisa na binafsi nina ndugu wenye uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na ni kweli walijifunza hukohuko Madrasa na wengine walipata nafasi ya kuongeza maarifa huko Arabuni.

Huyu nae ndio hata hajielewi, eti kiarabu hakihusiani na dini. Nenda basi kapige adhana kwa kiswahili au kingereza. Kuna mungu huko hajui kiswahili wala kingereza.
 
Ukiwaambia hivyo wanabaki kuruka ruka tu. Hawajui ya kuwa uislam ni chombo au mpango wa waarabu wa kueneza tamaduni, mila na desturi zao
 
Qur'aan imehifadhiwa na imelindwa, haiwezi kufikiwa na batil au corruption. Hivyo atakayejifunza ni lazima asomeshwe vilevile ilivyo. Atakayeisoma ataisoma vile vile. Atakayeihifadhi ataihifadhi vile vile.

Tarjama za lugha ya Kiswahili, Kiingereza na lugha nyengine sio Qur'aan ni tarjama tu za maana ya Qur'aan.

Halafu una uhakika watu hawasomeshwi kuielewa Qur'aan?

Na wapo watu wengi wamehifadhi Maneno ya Allah na wengine wanaielewa na bado hawawezi kuzungumza kiarabu. Huu ni Muujiza wa Qur'aan. Ni rahisi kuweza kuisoma na kuihifadhi Qur'aan, lakini pia ni rahisi Qur'aan kumponyoka mtu iwapo atakuwa haizingatii katika kuisoma na kuirudia rudia.

Halafu usiseme wanamezeshwa, bali wanahifadhi Maneno ya Mola Mlezi wa kila kitu. Jambo bora lilioje hilo! Kuisikiliza tu Qur'aan kuna fadhila, kuisoma kuna fadhila, sikuambii kuihifadhi kifuani, sikuambii kuielewa, sikuambii kuifanyia kazi na kuiishi. Qur'aan ni Maneno ya Allah, Mola Mlezi wa Viumbe vyote.

Ila kujifunza Lugha ya kiarabu ni muhimu mno katika kujifunza Dini ya Uislam na kuifahamu vizuri.
Quran haikuletwa ili watu wakariri, bali kuisoma na kuielewa. Wengi waislam wamekariri bila kujua maana. Ni sio lengo la Quran kuhifadhi bila kujua maana.
 
Mchezo huu hauhitaji hasira. Hizo hisia za kwamba uislam si uarabu ni watu wachache sana mlio nazo. Wenzenu wengi wanaona waarabu ni watu wa peponi. Na ndiyo maana ili ukubalike na Mola lazima ujue kiarabu. Hivyo ni ngumu sana kuutenganisha uislam kutoka ndani ya uarabu. Mtakataa nabkuruka ruka huku na kule, lakini ukweli unabaki ule ule, uarabu ndiyo nguzo ya uislam. Ndiyo maana bila kuongea maneno ya kiarabu wakati mnamuomba allahu wenu swala haiswili.
Ni kutozingatia tu Quran. Hakuna sehemu yoyote kwenye Quran imeandikwa watu wa swali kwa kiarabu. Ni utamaduni tu watu wameiga. Mtu anaswali bila kujua anaongea nini na Mungu, swala gani hiyo.
 
Kweli mku, nakuunga mkono tena aibu kubwa kwa waislam wa sasa, hatusomi Kiarabu wengine tunasoma lugha za makafiri badala ya kujifunza lugha yetu. Ijapokuwa kujifunza lugha ya makafiri sio dhambi lkn vijana wengi wa kiislamu wamejikita huko
Lugha zisizo za kiarabu ndio zipi kindengereko kimo?
 
Mbona mnarudia rudia maswali tumeshawajibu mtu anaweza akajua Quran na tafsiri yake ila asielewe kiarabu sio dhambi na haimuondolei chochote kwenye dini ila wale wanaobobea kwenye kiarabu wana X factor kwenye kutafsiri maneno mengi kwenye Quran, Quran imeshushwa kwa kiarabu ila kiarabu si Quran ni lugha pana zaidi.
Ona hii emptied head,imeshushwa kwa kiarabu halafu tena sio kiarabu,ibilisi kweli bingwa wa upotoshaji.
 
Ni kutozingatia tu Quran. Hakuna sehemu yoyote kwenye Quran imeandikwa watu wa swali kwa kiarabu. Ni utamaduni tu watu wameiga. Mtu anaswali bila kujua anaongea nini na Mungu, swala gani hiyo.

Mimi nilifikiri iko kwenye msahafu, kumbe wamejitungia wao.

Na vipi ile ya kutundika ma loudspeakers kwenye mapaa ya misikiti ni aya gani ya kuruwan?

CC: Bwana Utam Kisai Njooni kwa ufafanuzi
 
Mbona mnarudia rudia maswali tumeshawajibu mtu anaweza akajua Quran na tafsiri yake ila asielewe kiarabu sio dhambi na haimuondolei chochote kwenye dini ila wale wanaobobea kwenye kiarabu wana X factor kwenye kutafsiri maneno mengi kwenye Quran, Quran imeshushwa kwa kiarabu ila kiarabu si Quran ni lugha pana zaidi.

Kuna mmoja wenu akawa anasema "ukibobea kuruwan, itakuwa rahisi kwako kuelewa kiarabu". Hapo imekaaje?
 
Wenzenu wengi wanaona waarabu ni watu wa peponi.

Thibitisha hili. Wakina nani hao ? Unafikiri ni kama Ukristo ambao mnaliona taifa ovu la Israeli ni taifa teule na watu wake ?
Na ndiyo maana ili ukubalike na Mola lazima ujue kiarabu.

Hili limesemwa wapi katika Uislamu ? Tuwekee andiko.
Hivyo ni ngumu sana kuutenganisha uislam kutoka ndani ya uarabu.

Kwako wewe ambaye huujui Uislamu na Uarabu kadhalika ni ngumu kwako, ila ni rahisi sana.
Ndiyo maana bila kuongea maneno ya kiarabu wakati mnamuomba allahu wenu swala haiswili.

Kwanini mnayajadili mambo ambayo hamna elimu nayo ? Unaweza pia ukaongea hayo unayosema maneno ya Kiarabu swala yako pia ikawa batili. Sala ya Muislamu ina nguzo zake na masharti kadhalika.
 
Quran ni lugha ya zamani sana kwa hiyo wengi hukariri na ukibahatika kusoma sana utaelewa maana na tafsiri zake lakini huwezi kuongea hiyo lugha ya Qur'an mitaani
Kwa hiyo ni kujifunza tu lugha ya sasa ndio unaweza kuongea na wanaoelewa kiarabu
Mimi naongea vizuri sana kiarabu kwa sababu nimejifunza na ninajua tofauti za lafudhi zao wote ingawa wote wanaongea kiarabu lakini kuna tofauti kubwa baadhi ya maneno
Watu wa gulf kama Saudia, Emirates, hata Kuwait na Bahrain wanashabihiana
Ila ukiwasikiliza Syrians na Lebanon nao tofauti kubwa
Wamisri nao ni tofauti na Sudan ila wanaelewana kwa maneno mengi
Na mimi wote hao naweza kuwaelewa bila tatizo kwa sababu nimeishi nao wote
Kwa hiyo anaejua Quran huenda akashindwa kuongea kiarabu mpaka ajifunze
 
Back
Top Bottom