Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Na hii ndio tofauti ya QURAN NA BIBLIA, Quran imebaki kama ilivyo kwa miaka 1400 na mpaka sasa dunia nzima tuna Quran moja tu. Na ndio maana utaona mashindano ya kusoma Quran yanafanyika Tanzania yanahusisha nchi 40 ambazo hizo nchi zinaongea lugha tofauti. Lakini inapofika kwenye Quran tunayo moja tu dunia nzima.

Lakini kwa wenzetu wakristo wao wana bible zaidi ya 6000 duniani kote, ukiachilia mbali utofauti wa lugha kwa maana kila bible ipo kwenye lugha yake, lakini pia ndani ya lugha moja kuna bible tofauti tofauti kila dhehebu lina bible yao. Hata bible za kiswahili tu zimetofautiana za wasabato zikiwa tofauti na za wakatoliki na walutheri. Na ndio mana kamwe huwezi kuona Wakristo wakifanya mashindano ya kuhifadhi bible kwa sababu kila mtu ana bible yake kwa version yake na kwa lugha yake..

Kwa waislamu hata wakiwa madhehebu tofauti lakini Quran yao ni moja tu popote duniani.
Hii ingesaidia sana kama kungekuwa na juhudi za kufundisha kwa lugha za wenyeji na sio kukariri. Asilimia kubwa ya waislam hawajui content ya Quran sababu wamekaririshwa badala ya kusoma nankuelewa.
 
Kwamba anakuwa amekariri tu surat ila haijui tafsiri au maana yake?!
Ila wengi huwa naona wakinukuu aya ya Quran wanatoa na tafsiri yake kwa Kiswahili.
Mbona mnarudia rudia maswali tumeshawajibu mtu anaweza akajua Quran na tafsiri yake ila asielewe kiarabu sio dhambi na haimuondolei chochote kwenye dini ila wale wanaobobea kwenye kiarabu wana X factor kwenye kutafsiri maneno mengi kwenye Quran, Quran imeshushwa kwa kiarabu ila kiarabu si Quran ni lugha pana zaidi.
 
Na hii ndio tofauti ya QURAN NA BIBLIA, Quran imebaki kama ilivyo kwa miaka 1400 na mpaka sasa dunia nzima tuna Quran moja tu. Na ndio maana utaona mashindano ya kusoma Quran yanafanyika Tanzania yanahusisha nchi 40 ambazo hizo nchi zinaongea lugha tofauti. Lakini inapofika kwenye Quran tunayo moja tu dunia nzima.

Lakini kwa wenzetu wakristo wao wana bible zaidi ya 6000 duniani kote, ukiachilia mbali utofauti wa lugha kwa maana kila bible ipo kwenye lugha yake, lakini pia ndani ya lugha moja kuna bible tofauti tofauti kila dhehebu lina bible yao. Hata bible za kiswahili tu zimetofautiana za wasabato zikiwa tofauti na za wakatoliki na walutheri. Na ndio mana kamwe huwezi kuona Wakristo wakifanya mashindano ya kuhifadhi bible kwa sababu kila mtu ana bible yake kwa version yake na kwa lugha yake..

Kwa waislamu hata wakiwa madhehebu tofauti lakini Quran yao ni moja tu popote duniani.
Vijana waswahili wa Kibongo ambao hushiriki katika mashindano ya kuhifadhi Quran wote huwa wanaelewa tafsiri au maana ya surat na aya za Quran walizohifadhi??
 
Hivi ukiwa muislamu uliyesoma dini madrasa automatically unakuwa na uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na weledi? Unaweza kufika uarabuni mkazungumza na mwarabu mkaelewana vizuri au huwa cha kuzungumza nje ya dini ni cha kuombea maji ya kunywa tu?
Huwa naona wengi wanaweza kunukuu Quran kwa kiarabu na pia hata katika kuswali kinatumika kiarabu.
Ukiukiza inabidi ujibiwe, kwa ueleo wangu
Mkuu, huko Madrasa watoto wanafundishwa kwa mfumo wa lugha kama zilivyo lugha nyingine. Kwa maana ya kwamba a b c d & a e i o u.

Wanafundishwa vyema kabisa, ndio maana mwanafunzi bora anayezingatia mafunzo ana uwezo wa kukifahamu Kiarabu kwa ufasaha.
Hapana ndugu yangu Somo la Quruani linajitegemea ni kiarabu kinajitegemea ingawa maneno yanaingiliana tena yanaingiliana na kiswahili
 
Hii ingesaidia sana kama kungekuwa na juhudi za kufundisha kwa lugha za wenyeji na sio kukariri. Asilimia kubwa ya waislam hawajui content ya Quran sababu wamekaririshwa badala ya kusoma nankuelewa.
Hiyo ya kukaririshwa unasema wewe umahiri wa kufasiri na kukariri Quran hauwezi kuwa sawa kwa wote ila Quran za tafsiri za kiswahili zipo vp useme mtu anakaririshwa haelewi
 
Wakiristo waliosoma Magomeni Mwakinya St Joseph secondary school wakienda ulaya wanaongea kidhungu? Au ndio hello hello
Hii inatoa Elimu ya Kikristo kwa Kiingereza? Maana hapa sijaona logic (if you know the meaning of Logic)
 
Ukiukiza inabidi ujibiwe, kwa ueleo wangu

Hapana ndugu yangu Somo la Quruani linajitegemea ni kiarabu kinajitegemea ingawa maneno yanaingiliana tena yanaingiliana na kiswahili
Quran imeandikwa kwa lugha gani?
 
Swali, Biblia ya Wakristo wa Uarabuni imeandikwa kwa kiarabu, sasa kwa nini Wakristo wa Uarabuni hawajui kusoma Qur'an na imeandikwa Kiarabu?
Sifahamu sana lakini nadhani kutakua na utofauti lugha zina badilika kidogo lakini Qursn imebaki vilivile lakini hatokua sawa na asiyefahamu kabisa kiarabu
 
Swali, Biblia ya Wakristo wa Uarabuni imeandikwa kwa kiarabu, sasa kwa nini Wakristo wa Uarabuni hawajui kusoma Qur'an na imeandikwa Kiarabu?

Wanajuwa kuisoma, kuielewa ndio wanaweza wasielewe.
. Hilo ni hata kwa Waarabu wasio wakristo.

Qur'an imeshushwa ili iwe mwongozo kwa watu wote.
 
Hiyo ya kukaririshwa unasema wewe umahiri wa kufasiri na kukariri Quran hauwezi kuwa sawa kwa wote ila Quran za tafsiri za kiswahili zipo vp useme mtu anakaririshwa haelewi
Ukwali lazima usemwe. Hata mimi nilikaririshwa nikiwa mdogo na mpaka leo mengi niliyokarurishwa siyajui. Waulize waislamu wengi hata maana ya ile aya ya kwanza wanaijua?
 
Hiyo ya kukaririshwa unasema wewe umahiri wa kufasiri na kukariri Quran hauwezi kuwa sawa kwa wote ila Quran za tafsiri za kiswahili zipo vp useme mtu anakaririshwa haelewi
Mkuu hoja ya kukariri, inahitaji busara kuijadili ni tatizo ambalo lipo, nikupe challenge ya kulibaini?
 
Wanajuwa kuisoma, kuielewa ndio wanaweza wasielewe.
. Hilo ni hata kwa Waarabu wasio wakristo.

Qur'an imeshushwa ili iwe mwongozo kwa watu wote.
Quran iko waziwazi, sidhani kama mtu anaweza kujui kuisoma kwa kiarabu na asielewe maana. Wengi wamekariri tu maana hawajui lugha.
 
Hii ingesaidia sana kama kungekuwa na juhudi za kufundisha kwa lugha za wenyeji na sio kukariri. Asilimia kubwa ya waislam hawajui content ya Quran sababu wamekaririshwa badala ya kusoma nankuelewa.

asilimia kubwa ya waislamu wa wapi ndugu sio unazungumza kwa unavyohisi wewe, vema uwe na facts..
Kijana akianza kujifunza kiingereza akiwa darasa la tatu akifika form two au form four akisoma kitabu cha kingereza anaelewa isipokuwa kuna maneno yatamshinda kuelewa hadi uchukue kamusi..

Ndio hivyo hivyo kwenye kiarabu. Mimi sijakariri (kuhifadhi kwa kichwa) Quran lakini nikiisoma naelewa ninachosoma isipokuwa sehemu chache ndio sielewi mpaka nisome tafsiri ya kiswahili.

Hebu acheni mambo ya kuhisihisi kuhusu dini yetu, sisi wenyewe tunajua tunachofanya.,..
 
Mkuu hoja ya kukariri, inahitaji busara kuijadili ni tatizo ambalo lipo, nikupe challenge ya kulibaini?
Mfia dini hawezi kukuelewa, mimi secondary school niliachana na science kwa sababu ya kukariri shule haina hata maabara, unasoma kitu unakalili hujui hata kinafananaje.

The same na madrasa wengi wanakaririshwa tu.
 
Wanajuwa kuisoma, kuielewa ndio wanaweza wasielewe.
. Hilo ni hata kwa Waarabu wasio wakristo.
Kama wanajua kuisoma Quran bila kukariri kwa sababu wanajua kiarabu basi wanailewa pia.
 
Nimejaribu kufatilia huu mjadala toka mwanzo sijaona jibu la mwislamu yeyote kutoa jibu fasaha kuhusu lugha iliyoandikwa kwenye korani inaonekana wengi wenu ni wale fata mkumbo au umezaliwa ktk familia ya kiislamu lakini ukuwai kudadisi masuala ya dini yako uliyoirithi toka kwa wazazi wako.
Nilijaribu kuwauliza marafiki zangu waisalamu kwenye kijiwe cha kahawa .
Kuna ustaadh mmoja hivi anajua sana masuala ya dini anatokea msikiti maarufu kwa jina la ngamia mburahati.
Alinijibu kwamba Korani imeandikwa kwa kutumia lugha ambayo ipo ktk jamii fulani kwenye kijiji na hadi leo hii hiyo jamii hipo na wanazungumza hiyo lugha, tufanye hapa wangechukua mfano lugha ya( kizanaki) ingetumbukizwa kwenye korani ingekosa irabu a,ei,o,u
 
Mfia dini hawezi kukuelewa, mimi secondary school niliachana na science kwa sababu ya kukariri shule haina hata maabara, unasoma kitu unakalili hujui hata kinafananaje.

The same na madrasa wengi wanakaririshwa tu.
Mimi nikiona muislamu anapinga hoja ya kukariri au hata kufanyq kama ilo tatizo hakuna kabisa hua nashangaa sana ,najiuliza anaishi ulimwengu gani
 
asilimia kubwa ya waislamu wa wapi ndugu sio unazungumza kwa unavyohisi wewe, vema uwe na facts..
Kijana akianza kujifunza kiingereza akiwa darasa la tatu akifika form two au form four akisoma kitabu cha kingereza anaelewa isipokuwa kuna maneno yatamshinda kuelewa hadi uchukue kamusi..

Ndio hivyo hivyo kwenye kiarabu. Mimi sijakariri (kuhifadhi kwa kichwa) Quran lakini nikiisoma naelewa ninachosoma isipokuwa sehemu chache ndio sielewi mpaka nisome tafsiri ya kiswahili.

Hebu acheni mambo ya kuhisihisi kuhusu dini yetu, sisi wenyewe tunajua tunachofanya.,..
Huu ujinga ni mzigo mzito kwako, mimi najifunza imani ya kiislamu bila kujuwa kiarabu, nasoma aya za Quran kwa kiswahili na nimefaidika na mafundisho mengi mazuri yaliyopo kwenye kitabu ch Qur'an.

Utang'ang'ania vipi kujifunza kitu kwa lugha usiyoijuwa? Ina Mungu hatambui lugha ya kiswahili?

Tunakoenda mtakwenda msikitini na mtaswali kwa kiswahili hapo ndio mtaanza kuwavutia vijana wa kiislamu kwenda kuswali na kuipenda dini yao, lakini mkiendeleza huu utumwa wa lugha ya Waarabu Uislamu hauna nafasi kwa vijana wa kizazi kipya wenye uwezo wa kutumia app zao kupata wanachotaka.
 
Kwa hiyo suala la msingi sasa ni lipi ndugu zetu kukariri kiarabu au tofauti ya Quran na kiarabu naona kama mnatoka nje ya mada sasa inafika point mnafananisha Quran na physics 😀😀
 
Back
Top Bottom