Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Kutafsiri Quran kwenye lugha nyingine haina shida,,,sala ya kiislam sio kusoma Quran peke yake kuna dua zingine ambazo zinatakiwa zitamkwe kiarabu katika sala na uzijue maana yake katika lugha yako.....Hilo lisikusumbue sana kwa sababu ndio uislam ulivyoelekeza na we we amini katika dini yako ilivyoelekeza.

Siku zote mkiulizwa maswali ya msingi, mnashindwa kujibu hoja.
Nauliza swali la iwapo kama swala zisizo fanywa katika lugha ya kiarabu zinakubaliwa. Jibuni swali, badala ya kung'ang'ania kutuambia ya kuwa wewe uamini dini yako. Dini haina mmiliki, kila mtu yuko huru kuingia ama kutoka katika dini yoyote ile.
 
Mafundisho ya swala katika uislam ni kutamka matamshi ya kiarabu tu hakuna nafasi ya lugha nyingine hilo ndo jibu japo tunalirudia rudia
 
Kwa hiyo swala katika uislam zikitamkwa kwa lugha nyingine zinakuwa hazina nafasi. Yaani hazikubaliki. Kwa hiyo Allah hakubali kuswali kwake kwa lugha nyingine, isipokuwa kiarabu? Tukisema allahu ni mbaguzi au ana uwezo wenye kikomo wa kujua lugha, tutakuwa sawa?
 
Nje ya swala kuna dua ambazo unaweza kuziomba katika lugha yoyote uitakayo and its ok ila swala imewekewa utararibu ambao ni uniform dunia nzima(Quran na adhkar za kiarabu )yaani muislam wa Kazuramimba unaweza kwenda Paris ufaransa au Madrid Spain ukaongoza swala bila shida au kuswali kama maamuma,na sio kwamba lugha nyingine hazina nafasi kabisa hapana baada ya swala kuna dua ambazo zinaombwa lugha yoyote.kulitafsiri hili kama ni ubaguzi kwa lugha zingine inabaki kuwa subjective opinion
 
Okay, nimekuelewa vyema. Kwa hiyo swala ambazo zinafanyika kwa kiarabu ni zile 5 tu za kukariri na kujirudia rudia ambazo lazima zifanywe msikitini na kwa kutumia vipaza sauti.

Swali la nyongeza, swala hizo zikisomwa kimya kimya msikitini Allah hazikubali? Lazima kuwepo na ma loudspeakers 📢 🔊 🔈.

Pia kama zile suala tano zinaweza kutafsiriwa kwa lugha ya wenyeji.
 
Wanakariri huwa hawaelewi kitu,jiuleze kwanini somo la arabic language na islamic religion ndio yanayoongoza wanafunzi wa kobazi kufeli.
 
Okay, nimekuelewa vyema. Kwa hiyo swala ambazo zinafanyika kwa kiarabu ni zile 5 tu za kukariri na kujirudia rudia ambazo lazima zifanywe msikitini na kwa kutumia vipaza sauti.

Swali la nyongeza, swala hizo zikisomwa kimya kimya msikitini Allah hazikubali? Lazima kuwepo na ma loudspeakers 📢 🔊 🔈.

Pia kama zile suala tano zinaweza kutafsiriwa kwa lugha ya wenyeji.
Swala ina nguzo na sharti zake na ila uwepo wa kipaza saut sio sharti la swala ishu ni kujua muda wa kila swala na kuswaliwa kwa muongozo wake na ndo maana hata umeme ukikatika swala zinaendelea
 
Waelimisheni waumini wenzenu kuwa loudspeakers siyo sehemu au miongoni mwa nguzo za swala 5. Ndiyo maana hata kipindi cha mgao wa umeme, swala ziliendelea. Hata wanaokaa maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme wa rea bado swala zinaendelea.
Loudspeakers 📢 🔊 🔈 zinaathiri afya ya jamii. Maana kupiga kelele alfajili ya saa kumi inaweza kuwaathiri wakazi wa jirani na maeneo hayo. Wazia kukiwa na wagonjwa, watoto au hata watu wa kawaida na makelele kama yale, unadhani watakuwa salama? Hilo la loudspeakers liangaliwe upya, linafanya watu wasiwe na mtazamo mzuri kuelekea swala 5 na uislam kwa ujumla.
 
Ibada ya sala katika uislam inatumia lugha ya kiarabu ili kufanya ifanane popote duniani,,utakavyosali Tanzania ndio hivyo hivyo utakavyosali nchi yoyote duniani,,,nje ya sala lugha yoyote inaruhusiwa.
Hata ya roma iko hivyo lakini bila kutumia lugha moja kwani ukisema mungu mkubwa bila allah akbal maana inabadilikaje hapo?
 
Swala ina nguzo na sharti zake na ila uwepo wa kipaza saut sio sharti la swala ishu ni kujua muda wa kila swala na kuswaliwa kwa muongozo wake na ndo maana hata umeme ukikatika swala zinaendelea

Kuna sehemu nilikokuwa nakaa Mfaranyaki Songea, umeme ukikatika muda wa swala nilikuwa nafurahi, maana makelele ya loudspeakers hayakuwepo.
😛
 
Hata ya roma iko hivyo lakini bila kutumia lugha moja kwani ukisema mungu mkubwa bila allah akbal maana inabadilikaje hapo?
Kama Roma wanafanya hivyo ni vizuri ila kwenye uislam swala inatumia lugha ya kiarabu,,,,,hata katika maisha ya kawaida kuna sehemu kinatumika kiingereza tu kama mahakamani na hospital.
 
Quran haikuletwa ili watu wakariri, bali kuisoma na kuielewa. Wengi waislam wamekariri bila kujua maana. Ni sio lengo la Quran kuhifadhi bila kujua maana.
Wewe hoja yako ilikuwa ni kuwa Quran ifundishwe kama Bilblia, yaani nilikuelewa unamaanisha eti ifundishwe Quran kwa Kiswahili, Quran iko katika lugha yake vile vile na watu wataisoma na kusomeshwa vile vile ilivyo.

Na kuhifadhiwa na watu kuanzia watoto wadogo mpaka wazee vifuani mwao huo ni katika muujiza na haiwezi kupotea hata Misahafu yote hii kama ikatokea kutoweka yote hii basi kwa sababu imehifadhiwa vifuani na mamilioni Quran itaweza haiwezi kupotea hata herufi.

Na husomwa Quran mara kwa mara, na kwa wingi.

Quran sio biblia, Quran ni Maneno ya Allah, kuyasoma tu kuna fadhila zake, kuyasikiliza hata kama huna huelewi kuna fadhila yake. Kuihifadhi ndio kabisa.

Na kuelewa maana yake ni jambo pia linasomeshwa na wanaosoma/wanaotafuta Elimu wanasoma.
 
Ni kutozingatia tu Quran. Hakuna sehemu yoyote kwenye Quran imeandikwa watu wa swali kwa kiarabu. Ni utamaduni tu watu wameiga. Mtu anaswali bila kujua anaongea nini na Mungu, swala gani hiyo.

Swala katufundisha Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Na tunaswali kama alivyotufundisha, nyinyi mnaojidai ni Quranists (Quranists ni makafiri) mko mbali mno na Quran. Quran imeamrisha kumfuata Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) nyinyi mnakataa kabisa asifuatwe Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Sisi tunamshukuru Allah kwa Neema tukufu mno kabisa ya Uislam na Sunnah, tunamshukuru Allah aliyeiteremsha 'Ibadah tukufu ya Swala na akmfunulia mafundisho ya Swala Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) na Mtume akatufikishia. Na Waislam wote Duniani tukawajibika kuswali kama alivyoswali Mtume. Leo nikienda Upareni au Helsinki, Finland, nikakuta Waislam basi Swala ni ile ile, Muislam hata akitoka Switzerland au China anaweza kuja Tanzania na akawaswalisha ndugu zake hata kama hazijui lugha zao mama, Alhamdulillah.

Halafu maneno yanayofundishwa katika Swala maana yake hufundishwa, ni wewe ndio hujui. Na Dua zilizokuja kutoka kwa Mtume pia hufundishwa hata maana zake na watu wanazihifadhi na wanaelewa hata kama hawawezi kuzungumza kiarabu.

Na katika Sijda ambapo imehimizwa kukithirisha kuomba Dua wasiojua kiarabu wanaweza kuomba kwa lugha wanazozijua wao wakamuomba Allah haja zao mbalimbali kwa sababu mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake akiwa katika Sijda.

Na nje ya Swala ndio kabisa mtu anaweza kumuomba Allah kwa lugha yoyote ile.

Namuomba Allah anifishe katika Uislam na Sunnah ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Allah akuongoze.
 
31st December 2024
Zanzibar, Tanzania

Ziara ya Dr. Zakir Naik mhadhiri maarufu wa dini ya kiIslamu duniani aliyoifanya nchini Tanzania hivi karibuni

View: https://m.youtube.com/watch?v=ipig0nJIhIc

Maoni: yaliyodhihiri
Walipaswa waweke mtu wa kutafsiri, hili ni jambo la msingi mmelipuuzia, lugha zilizo tumika na hao wageni Dr. Zakir Naik na mwanae Shaikh Fariq Naik ni Kiarabu na Kingereza, ilipaswa akiongea kila baada ya nukta, basi tafsiri inaletwa wangenufaika wengi zaidi na Kwa kiasi kile kile na Kwa hisia Ile Ile....lakini kutafsiri Kwa namna hii walio iweka, Ile ladha inapungua
 
Zakir naik mbishi sana, alikataa mambo ya kutafsir
 
Dr. Zakir Naik hakutenda haki, wengi walikosa kufaidika vilivyo na mihadhara yake kutokana na changamoto ya lugha za kimataifa inayoikabili umma mpana wa waTanzania.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Wewe hoja yako ilikuwa ni kuwa Quran ifundishwe kama Bilblia, yaani nilikuelewa unamaanisha eti ifundishwe Quran kwa Kiswahili, Quran iko katika lugha yake vile vile na watu wataisoma na kusomeshwa vile vile ilivyo.

Na kuhifadhiwa na watu kuanzia watoto wadogo mpaka wazee vifuani mwao huo ni katika muujiza na haiwezi kupotea hata Misahafu yote hii kama ikatokea kutoweka yote hii basi kwa sababu imehifadhiwa vifuani na mamilioni Quran itaweza haiwezi kupotea hata herufi.

Na husomwa Quran mara kwa mara, na kwa wingi.

Quran sio biblia, Quran ni Maneno ya Allah, kuyasoma tu kuna fadhila zake, kuyasikiliza hata kama huna huelewi kuna fadhila yake. Kuihifadhi ndio kabisa.

Na kuelewa maana yake ni jambo pia linasomeshwa na wanaosoma/wanaotafuta Elimu wanasoma.
Sahihi kabisa, lakini muongezee utasomaje na kuelewa kabla hujakarir? Asilete matakwa yake waislamu wanafata matakwa ya dini inavyosema, kabla ya chochote ni Muislamu ajue kusoma vizur Qur aan.
 
Ki

Wapi imeandikwa Quran isomemwe kama ilivyo?
 
Sahihi kabisa, lakini muongezee utasomaje na kuelewa kabla hujakarir? Asilete matakwa yake waislamu wanafata matakwa ya dini inavyosema, kabla ya chochote ni Muislamu ajue kusoma vizur Qur aan.
Ndio maana wengi hawajui content ya Quran, wamekariri bila kujua maana yake.
 
Back
Top Bottom