Waislamu wagombea Msikiti wa Wilaya ya Nyamagana, Ngumi zaibuka Waumini wadai BAKWATA imeundwa huu Msikiti wa Masjid Noor wameukuta!

Waislamu wagombea Msikiti wa Wilaya ya Nyamagana, Ngumi zaibuka Waumini wadai BAKWATA imeundwa huu Msikiti wa Masjid Noor wameukuta!

Bakwata imeanzishwa na nyerere Bakwata imejifunza unyanganyi kutoka kwa nyerere, Bakwata wanadhulimu mali za waislamu walioijenga kwa pesa zao wanazimilikisha Bakwata wanakula wao na familia zao. nyerere aliwanyanganya watu nyumba zao zimejengwa miaka hata nyerere hajazaliwa aliposhika urais kawadhulumu watu nyumba zao na kuipa NHC wakati nhc hawajajenga nyumba hata moja zoote za wahindi na waarabu dhulma hii ndio inayotutafuna na inaitafuna bakwata

Sera za ujamaa,mali zilirudi kwa serikali kunufaisha wananchi wote.
 
BAKWATA ndio chombo au taasisi madhubuti ya kutetea kulinda mali za Waislam wote Tanzania.

Hizi taasisi nyingine kama Shura ya Maimamu......... zinawakisha fujo na kutuondolea amani watanganyika.

Hao wote ni waganga njaa tu. Wanapambania chance ya kuwanyonyonya waislamu.
 
Mali ya waislam itaandikwaje kwenye hati ? Mfano Waislam wapo milioni 20 ama 30 na wanazaliwa na kufa kila siku

Si itakuwa vurugu mechi hiyo hati.

Hata Tanzania kwa mfano ardhi ni mali ya uma. Ila kisheria Rais ndie ana mamlaka ya kuisimamia hiyo ardhi ya uma akituwalilisha uma wa waTanzania . Ndie pekee ana mamlaka wa kuikopea ama kuiuza.

Hivyo Huwezi sema sababu mimi ni sehemu ya uma huu ni mmiliki wa hii ardhi nina mamlaka ya kuifanya chochote.

Bakwata ndie anawakilisha waislam. Mali zote za waislam zinapaswa zisimamiwe na bakwata kama muwakilishi wa hao waislam
Wafuate namna RC wanavyoandika hati za viwanja kulikojengwa makanisa..!! Hati inaandikwa body of trustees..!!
 
Back
Top Bottom