Waislamu wako vizuri kwenye suala la ndoa

Kwani Kuna mtu anakuzuia kuoa muislam au kuhama dini?acheni hizo we uliona huko Kuna deso oa tu hata Kama utatengwa na ukoo mzima wewe Ni mtu mzima una maamuzi yako pia
 
Binti inaonekana Islamophobia inakutesa sana,haya komaa na Mumeo ili usije ukaachika.
 
Kwani Kuna mtu anakuzuia kuoa muislam au kuhama dini?acheni hizo we uliona huko Kuna deso oa tu hata Kama utatengwa na ukoo mzima wewe Ni mtu mzima una maamuzi yako pia
Suala lakuoa dini tofauti nisuala zito sana hasa hili lakutengwa naukoo mzima nikisanga hata mm bado niko dilemma naona kabisa unaweza kutengwa nandugu endapo ukioa jamii ambazo wao hawaziamini.
 
Quran 4:4

"Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha."

Mungu ametoa agizo kuwa wanawake wapewe mahari zao kabla ya kuolewa na hii haimaanishi kuwa mwanamke ni bidhaa ya kuuzwa bali ni heshima na kutukuzwa na ni ishara ya kuwa mwanaume amekubali kubeba majukumu yanayomkabili katika ndoa yake. Katika uislam Mahari haijawekewa kiwango maalumu ila ni makubaliano ya pande mbili tu na mahari ni ya mwanamke yeye ndie anawajibika kusema anahitaji kiasi/kitu gani ili aolewe. Mtume Muhammad akaelekeza zaidi kwa kusema kuwa

"Wanawake wengi watukufu wenye baraka ni wale wenye mahari yaliyo madogo" (Ahmad, al-Bayhaqiy na al-Haakim).

Hii haimaanishi kuwa endapo mwanamke atahitaji mahati kubwa asipewe la hasha!

Kiwango cha mahari kinapendeza kiwe cha wastani ili kurahisisha suala la ndoa na hii inapelekea kuondosha uzinifu katika jamii.
 
Unaongea mambo usiyokuwa na ujuzo wala elimu nayo infact ni Muongo!!

1: Uislam umeamrisha mwanauke atoe mahari kumpa mwanamke kwa kiwango walichokubaliana! Mwanamke akihitaji 100M ndio aolewe ni sawa na pia akihitaji pair mbili za viatu pia sawa ili mradi ameridhia mwenyewe.

2: NDOA za kiislam si za muda mfupi, Lengo la ndoa ni watu waishi muda mrefu, watengeneze vizazi na waishi katika misingi na maadili ya kiislam. Kuna mifano mingi ya ndoa za kiislam ambao wanandoa wameishi mpaka kuzikana pasi na kutalakiana.

3: Kuhusu kuoa wake wanne hilo jambo ni sheria na maamrisho kutoka kwa Mungu.Yeye ndie amehalalisha kuwa Muislam anaruhusiwa kuoa wanawake kuanzia mmoja mpaka wanne ili mradi awe muadilifu. Kuna mifano mingi ya kihistoria kuonesha kuwa Mitume na manabii walikuwa na wake zaidi ya mmoja.

Mfalme Suleimani na Daudi walikuwa na wake wengi, Mtume Ibrahim/Abraham (Baba wa Imani) alikuwa na mke zaidi ya mmoja.

Je hawa hawakumjua Mungu zaidi yako au tuseme wewe una imani kubwa kumzidi Ibrahim??
 
Ninyi kwa sababu mmekula kiapo hadi kifo... Kwenye uislamu ikifika mhali hamuezi tena kuishi pamoja kama mke na mume ni bora muachane kwa wema.. maana pia mlioana kwa wem
 
Karibuni kwenye uislamu
 
BIBLIA PIA IMERUHUSU TALAKA

Mathayo 5:32

"Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini."

Matthew 5:32 — King James Version (KJV 1900)


" But I say unto you, That whosoever shall put away his wife, saving for the cause of fornication, causeth her to commit adultery: and whosoever shall marry her that is divorced committeth adultery."
 
 
Na ndiyo wanaongoza kujaza single mothers mtaani
 
Asante Kaka,wanabisha wakati Mambo yapo wazi kabisa wanao January, February wanaacha March anaolewa mwingine.
 
kuna kipindi nilikua naangalia kwenye tv mwanamke analilia ndoa kwa mahari ya juzuu na msaafu aisee hapo ndonilipotambua vyarahisi havina thamani....chunga imani yako kijana
Laiti ungejua hiyo mahari ya Msahafu usingeandika haya

Mtu anapokuambia nipe msahafu kama mahari maana yake ni kubwa sana yaani lazima umfundishe na akariri na kuielewa Quran yote mkuu

Na sio kupewa kitabu na kukiweka kabatini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…