Waislamu wanaamini Wakristo hawaendi Mbinguni na Wakristo wanaamini waislamu hawaendi Mbinguni. Vita ni kali sana

Kwa Mungu hakuna dini ya kikristo wala ya kiislamu.Kuna ufalme aliowekewa Adam kabla ya kumwasi Mungu.Baadaye alitoa msamaha kwa sadaka ya kumtoa mwanae wa pekee Yesu.Yesu Kristo hakuleta dini alitumwa kuturejesha uhusiano na Mungu.Endapo binadamu watapokea offer hii na kuyafanya mapenzi yake,ataingia katika ufalme wake.
 
1) UISLAM
Ukiwa Muislam una uwanda mpana wa kufanya analysis ya mafundisho ya Mungu pamoja na manabii Kwa sababu uislam unaamini na kuwakubali manabii wote pamoja na vitabu vyao
Hivyo Muislam hana limitation katika mafundisho ya manabii na vitabu vyao

Siku mtume Muhammad alipofunuliwa habari za Musa kuhusu kugawanyisha bahari Kwa fimbo yake akasema Ee Allah hawa watu wangu nikiwapa hizi habari wataamini kweli maana kipindi hicho Kila alichokuwa anafunuliwa watu walikuwa wanamuona Muongo
Allah akamwambie waulizeni wanaojua ikiwa nyinyi hamjui Yani wawaulize Wana wa Israel kuhusu hizo habari

2) UKRISTO
Ni dini ambayo Ina limitation nyingi katika kuamini kwao na mafundisho Yao na haya yanatokea Kwa sababu dini yenyewe imeanzishwa Kwa ujanja ujanja na ndio maana ukimbana sana mkristo Kwa maandiko anakimbilia Kwa roho mtakatifu kuwa ndio anayewaongoza
Wakati roho mtakatifu alishamaliza kazi zake za kuleta ufunuo Kwa manabii
Ukichukua wakristo 100 ukiwauliza Yesu ni nani Kila mmoja atatoa jibu lake wapo watakao Sema
A)Yesu ni mwana wa Mungu
B)Yesu ni Mungu
C)Yesu ni mmoja katika Miungu 3
D)Yesu katumwa na Mungu aje kufa
E) Yesu ndio Mungu mkuu

Hi ni Kwa sababu walioanzisha hii dini Kuna vitu wamevificha Ili malengo Yao yafanikiwe
Yesu ameishi Nazareth Kwa muda wa miaka 33 lakini Bibilia inamuelezea Yesu Kwa maisha yake ya miaka 3 tu vipi hi miaka 30 ya nyuma alikuwa anafanya Nini?

Hakuna sehemu katika Bibilia inayosema kuwa Yesu alikuwa anatumwa dukani na mama yake akanunue unga wa ngano na mafuta ya taa

Hakuna sehemu yoyote inayosema kuwa Yesu alikuwa anacheza kombolela na watoto wenzake katika mitaa ya Galilaya

Sio kama walisahau kuweka historia ya maisha ya Yesu Kwa kuanzia mwaka 0 Hadi 30 ila ni mpango mkakati

3) UYAHUDI
Uyahudi ni uislam uliokataa kufuata mafundisho ya mtume Muhammad
Wayahudi wanajua kuwa ukristo ni dini ya uongo na uislam ni dini ya kweli kinachowafanya wasifuate mafundisho ya mtume Muhammad ni jeuri tu hakuna kingine

Wakati mtume Muhammad anafunuliwa kitabu Cha Quran
Makafiri wa Maka walienda Kwa Wayahudi kutaka ushauri watumie njia gani ilikuthibisha kuwa Muhammad ni mtume wa Mungu au anawadanganya
Wayahudi wakawapa mbinu wakawambia muulizeni habari za watu wa mapangoni kama atakujibuni basi yeye ni mtume kweli

Watu wa mapangoni ni wachamungu ambao walichukia maasi katika mji wao wakaenda kuishi mapangoni Mungu akawalaza usingizi Kwa muda wa miaka 300 na hili jambo halipo Katika vitabu vya kale ila ni jambo maharufu ambalo wayahudi wote walikuwa wanakijua

Allah alimfunulia mtume Muhammad kuhusu hawa watu habari zote
Hiki kisa kipo katika surati Ka hafu

Kwahiyo wayahudi wanajua kabisa kuwa Muhammad ni mtume wa Mungu na Quran ni kitabu Cha Mungu ila jeuri ndio inayowasumbua
 
Yesu ni njia yakwenda mbinguni,
Ila chakushangaza uislam ni dini ya haki na ni dini ya mwenyezi mungu,
Sasa ukitaka kuwaweza waambie hakuna mungu , wataungana kukusema weeeeeeee, ala chorus, wapigie Yesu ni Mungu, afu ondoka verse ya pili watapiga wao
 
Hii vita ni kali sana ambayo haina mwisho wake, Hiyo ni mpaka pale mtu utakapo kufa ni either ujue ukweli au upotee as kabla haujazaliwa.
Wale wasiojiamini katika imani hasa wale watumiao nguvu kueneza imani yao.
 
Kwa ujinga huu uliouandika sidhani kama kuna jambo lolote lingine huko uliko unalifanya kwa ufasaha. Kiwango chako cha elimu ni kidogo sana.
 
Kwa ujinga huu uliouandika sidhani kama kuna jambo lolote lingine huko uliko unalifanya kwa ufasaha. Kiwango chako cha elimu ni kidogo sana.
Isije ikawa wewe ndio mjinga

Maana mjinga namba Moja ni mtu ambaye hata Mungu wake aliyemuumba hamjui

ebu niambie wewe unaamini lipi kati ya haya Ili tuone wewe ni mjinga au sio mjinga

A)Yesu ni mwana wa Mungu
B)Yesu ni Mungu
C)Yesu ni mmoja katika Miungu 3
D)Yesu katumwa na Mungu aje kufa
E) Yesu ndio Mungu mkuu

Mimi ni Muislam naamini Yesu ni binadamu kama Mimi tu ila yeye ni nabii wa Mungu
 
Mzeebaba hapo sahihi ni A tu, halafu hapo D unaposema ametumwa kuja kufa, ni nini sasa hiyo! Yaani Yesu aje Duniani sababu yake ya kuwepo hapa ni kufa tu! Haupo serious wewe, hebu weka maelezo vizuri pengine utaeleweka.

Ubinadamu wa Yesu ni WA kipekee kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi kwenye hii Dunia.
 
Hii vita ni kali sana ambayo haina mwisho wake, Hiyo ni mpaka pale mtu utakapo kufa ni either ujue ukweli au upotee as kabla haujazaliwa.
Wote hawaendi mbinguni. Anayekwenda mbinguni ni yule tu aliyetubu, kumwamini na kumpokea Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wake binafsi. Mungu hajaleta dini yoyote kwa wanadamu bali alikuja yeye mwenyewe. Hivyo asiyemkubali hawezi kuingia mbinguni maana Yesu ni njia. Sasa bila njia utafika vipi mbinguni?
 
Hivi nyie mngezaliwa miaka ya 1900 mngekuwa dini gani??

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kila mtu aamini anachokiamini..
Tusibishane ktk imani.
Imani n ya mtu binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…