Waislamu wanajuaje majina ya Kaini, Habili na Hawa wakati hayapo kwenye Quran?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Kuna jambo linanichanganya Waislamu wanaposema Injili/Biblia na Taurati vimeharibiwa au kupotoshwa,

Ikiwa Qurani inasema mambo mengine waulizwe wayahudi au watu wa Kitabu wakati Taurati na Injili zinapingana nayo, basi Quran inajipinga na hivyo ni ya uongo. Ikiwa Taurati na Injili zimeharibiwa au zimepotoshwa, basi kwa mujibu wa hoja hiyo hiyo, Quran bado ni ya uongo kwa sababu inazithibitisha inapotumia baadhi ya rejea zake, huu ni mkanganyiko.

Mfano mmojawapo ni kwamba Kaini, Habili na Hawa hawajatajwa kwenye Quran hivyo ili Muislamu awajue anahitaji kuwasoma kwenye Biblia au Taurati, Sasa ukisema hivi vitabu vimeharibiwa ina maana huwezi kujua majina ya watoto na mke wa Adamu, ukiyakubali hayo majina yao ina maana Quran nayo pia inakuwa kwenye mkondo wa kuharibiwa au kupotoshwa.
 
Mudi's fairytale story book.
 
In the Quran (Surah Al-Ma'idah 5:27-31), the story of Adam’s two sons—traditionally known in Islamic tradition as Qabil (Cain) and Habil (Abel)—serves as a timeless moral lesson on jealousy, the sanctity of life, and the consequences of unchecked anger. [1, 2, 3]
 
Ukisoma kitabu chenye makosa ukapata taarifa moja sahihi, je kitabu kizima kinakuwa sahihi?
Waislamu wanaamuaje na kwa kutumia vigezo gani kipi kimepotoshwa na kipi ni sahihi katika Injili/ Biblia na Taurati?

Kuna uhakika gani Kaini, Habili na Hawa ni majina sahihi na hayajapotoshwa kama mambo mengine?
 
Hiyo sura kwenye Quran inasema tu watoto wawili wa Adamu, haitaji majina yao wala kusema yupi alimuua mwenzake.
 
Al-Ma'idah aya ya 27:

"Na wasomee kwa haki habari za wana wawili wa Adam, walipotoa sadaka. Ikakubaliwa kutoka kwa mmoja wao, na haikukubaliwa kutoka kwa yule mwingine. Akasema: 'Hakika nitakuua.' Akasema: 'Hakika Mwenyezi Mungu huwapokea (matendo) kutoka kwa wenye kumcha.'" (Qur'an 5:27)


Aya ya 28:
"Ukikinyoosha mkono wako ili kuniua, mimi sitanyoosha mkono wangu kukuua. Hakika mimi namuogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu."

Aya ya 30:
"Basi nafsi yake ikamshawishi kumuua ndugu yake, akamuua, na akawa miongoni mwa waliopata hasara."
---‐--------------

Haabil na Qaabil wamezungimziwa hapo!!!

Ufafanuzi kwenye hiyo aya ili kuwafahamu unaipata kwenye tafsiri.

Na tafsiri kwenye Qur'an inapatikana kwa: Qur'an kwa Qur'an, Qur'an kwa Sunnah na Qur'an bi swahaba.
 
Waislamu wanaamuaje na kwa kutumia vigezo gani kipi kimepotoshwa na kipi ni sahihi katika Injili/ Biblia na Taurati?

Kuna uhakika gani Kaini, Habili na Hawa ni majina sahihi na hayajapotoshwa kama mambo mengine?
Si Waislamu wanaoamua, Qurani ndiyo huwa kigezo, kile kinachoafikiana na Qurani hakipingwi, kinachokinzana nacho hukataliwa, na kile ambacho Qurani haijakithibitisha wala kukikana hakijengwi juu yake aqida( imani)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…