Waislamu wanajuaje majina ya Kaini, Habili na Hawa wakati hayapo kwenye Quran?

Waislamu wanajuaje majina ya Kaini, Habili na Hawa wakati hayapo kwenye Quran?

Ukiisoma kwenye tafsiri ya hizo aya kwenye Qur'an.

Imam Ibn Jarir Attwabari amepokea kutoka kwa Abdallah ibn Abbas kwamba: Qaabil alikuwa mkulima, na Haabil alikuwa mchungaji wa kondoo. Haabil akatoa kondoo bora, Qaabil akatoa mazao mabaya, ndipo sadaka ya Habil ikakubaliwa na ya Qaabil ikakataliwa.

Ibn Abbas ni swahaba wa Mtume.
Imam Attwabari ni mfasiri wa Qur'an.
Hizi hadith ni za kutunga miaka taktiban 200 baada ya mtume. Quran yenyewe iko kimya kuhusu swali la mleta uzi
 
Umejuaje watoto wa Adamu walikuwa wanaitwa Haabil na Qaabil?
Hayo majina yao Waislamu mliyapata au mnayapata wapi?
Kasome Qisas al Anbiya ,hizo simulizi / hadithi utazipata humo.
 
Ufahamu pia Bw. Yoda

Baada ya Haabil kuuawa ndipo Mungu akampatia Adam mtoto anayeitwa Sheeth.

Sheeth alikuwa ni mtoto ambaye alikuwa ni wa tofauti. Yeye ndiye binadamu wa kwanza kutokwa na ndevu, na ndiye mtoto aliyepokea kijiti cha Utume kutoka kwa Nabii Adam alayhi ssalaam.

Na ndiye binadamu wa kwanza kuunda jeshi na kupigana na upande mwengine: Qaabil alikimbia na Dada yake ambaye alikatazwa kumuoa kwa amri ya Mungu kwa nyakati hizo baada ya kumuua nduguye.

Akazaa naye na kizazi kikawa kikubwa. Kufupisha maelezo; hawa ndiyo watu ambao Nabii Sheeth alipambana nao baadaye kwa kusimamisha vita nao.
Huo upande mwingine umetoka wapi, hilo jeshi lilikuwa la mtu mmoja? baba yao basi hakuwa wa kwanza.
 
Waliondika hizo hadithi au Qisas wayapata wapi majina ya watoto wa Adamu?
Hayo mambo yalianzia mashariki ya kati kwenye hadithi zao za kale , Palestine ya kale na wayahudi wakale , wana share historia kama ndugu wa damu , toka kale za mababu zao hivyo sisi wamatumbi kuja kuhoji hayo kwa sasa ni kurukwa na akili tu
 
Nikisema mke Adam alikuwa anaitwa Lilith utapinga au kukataa?
Hayo ni mafundisho ya kiyahudi ambayo ndani ya ukristo wala uislamu hayapo , hivyo kwa imani kila mmoja yupo sawa tu
 
Kuna jambo linanichanganya Waislamu wanaposema Injili/Biblia na Taurati vimeharibiwa au kupotoshwa,

Ikiwa Qurani inasema mambo mengine waulizwe wayahudi au watu wa Kitabu wakati Taurati na Injili zinapingana nayo, basi Quran inajipinga na hivyo ni ya uongo. Ikiwa Taurati na Injili zimeharibiwa au zimepotoshwa, basi kwa mujibu wa hoja hiyo hiyo, Quran bado ni ya uongo kwa sababu inazithibitisha inapotumia baadhi ya rejea zake, huu ni mkanganyiko.

Mfano mmojawapo ni kwamba Kaini, Habili na Hawa hawajatajwa kwenye Quran hivyo ili Muislamu awajue anahitaji kuwasoma kwenye Biblia au Taurati, Sasa ukisema hivi vitabu vimeharibiwa ina maana huwezi kujua majina ya watoto na mke wa Adamu, ukiyakubali hayo majina yao ina maana Quran nayo pia inakuwa kwenye mkondo wa kuharibiwa au kupotoshwa.

Msikilize huyu mkristo mwenzako anavyosema

 
Mtume Muhammad alikuwa anatoa wahayi mwingine nje ya Quran kupitia hadithi?
Labda nikusaidie pengine unaweza ukashindwa kujibu.

Qur'an inasema:

"Na tumekuteremshia Ukumbusho (Qur'an) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao..."
Surat An-Nahl (16:44)

Hivyo, Sunnah ni ufafanuzi wa Qur'an. Kuna mifano kadhaa wa kadhaa nitakuonyesha.

Kwa mfano kwenye swala. Qur'an imeamrisha: "Na simamisheni Sala..."
(Al-Baqarah 2:443)

Lakini haikueleza rakaa za kila swala, namna ya kuswali, kusoma nini katika kila rakaa. Mtume akafafanua kwa vitendo katika hayo yote.

Mfano mwengine, ni kwenye Zaka. Qur'an imeamrisha kutoa zaka, lakini haikutaja kiwango cha kila aina ya mali. Haya yote yalifafanuliwa katika Hadithi.

Mfano mwengine, ni suala la Hija. Qur'an imeamrisha Hija lakini haikueleza kwa kina taratibu zake.
Mtume alisema:"Chukueni kutoka kwangu namna ya kutekeleza ibada zenu za Hija."

Kwa msingi huo, jawabu la swali lako ni kwamba; ufafanuzi wa Qur'an unapatikana katika sunnah. Halikadhalika, fafanuzi nyengine zinapatika kwenye Qur'an yenyewe imetafsiri. Vilevile, fafanuzi nyengine zinapatikana kutoka kwa maswahaba zake ambao kupitia yeye walielezwa hizo fafanuzi au walisikia kutoka kwake.
 
Kuna jambo linanichanganya Waislamu wanaposema Injili/Biblia na Taurati vimeharibiwa au kupotoshwa,

Ikiwa Qurani inasema mambo mengine waulizwe wayahudi au watu wa Kitabu wakati Taurati na Injili zinapingana nayo, basi Quran inajipinga na hivyo ni ya uongo. Ikiwa Taurati na Injili zimeharibiwa au zimepotoshwa, basi kwa mujibu wa hoja hiyo hiyo, Quran bado ni ya uongo kwa sababu inazithibitisha inapotumia baadhi ya rejea zake, huu ni mkanganyiko.

Mfano mmojawapo ni kwamba Kaini, Habili na Hawa hawajatajwa kwenye Quran hivyo ili Muislamu awajue anahitaji kuwasoma kwenye Biblia au Taurati, Sasa ukisema hivi vitabu vimeharibiwa ina maana huwezi kujua majina ya watoto na mke wa Adamu, ukiyakubali hayo majina yao ina maana Quran nayo pia inakuwa kwenye mkondo wa kuharibiwa au kupotoshwa.

Hivi unajua maana ya "kuharibiwa" kama ulivyo irudia, rudia...
Kwa kukusaidia, kuharibiwa maana yake; kitu kilikuwa kizuri ila wajuaji wakachakachua na kuandika vile wanapenda kuvisikia/ kikawa feki au kikaharibika. Hii ina maanisha ukipata orginal copy (kabla hakijarabiwa) kitakuwa kizuri sana...

Hivi unajua kuna toleo jipya la Biblia lipo jikoni, baada ya kuonekana kuwa kwenye Biblia zilizopo sokoni kuna baadhi ya vifungu havina ushahidi wowote kuwa ni mapokea ya mitume wa Yesu....
 
Hivi unajua maana ya "kuharibiwa" kama ulivyo irudia, rudia...
Kwa kukusaidia, kuharibiwa maana yake; kitu kilikuwa kizuri ila wajuaji wakachakachua na kuandika vile wanapenda kuvisikia/ kikawa feki au kikaharibika. Hii ina maanisha ukipata orginal copy (kabla hakijarabiwa) kitakuwa kizuri sana...

Hivi unajua kuna toleo jipya la Biblia lipo jikoni, baada ya kuonekana kuna vifungi vingi tu havina ushahidi wowote kuwa ni mapokea ya mitume wa Yesu....
Original copy ya Taurati waliyotumia Waislamu kujua watoto wa Adamu walikuwa wanaitwa Kaini na Habili ilienda wapi?
 
Mna bahati Hitler alishindwa vita kuu ya pili ya dunia, leo uyahudi au uislam usingekuwepo, Nazi manifesto ingekuwa ndio bible/quran ya leo na kila mtu angekuwa anaongea kijerumani na usipotii amri ni shaba tuu, na Hitler au mrithi angejulikana ndio mungu
 
Quran ilitumia rejea ya Biblia gani kati ya hizo kujua watoto wa Adamu ni Kaini na Habil, Kaini ndio alimuua Habil na jina la mke Adamu lilikuwa Hawa na sio Lilith??
Qurani haikuyataja majina hayo. Majina ya Kaini, Habili na Hawa katika Uislamu yanapatikana katika Hadithi na tafsiri za wanazuoni, si katika maandishi ya Qurani yenyewe.

Hivyo swali la 'ilitumia Biblia gani' halina msingi kwa sababu Qurani yenyewe haijataja hayo majina.
 
Back
Top Bottom