Waislamu wanajuaje majina ya Kaini, Habili na Hawa wakati hayapo kwenye Quran?

Sadaka ya nani haikukubaliwa?
Sadaka ya nani ilikubaliwa?
Nani alimuua mwingine?
Nani aliuliwa na mwingine?
 
Si Waislamu wanaoamua, Qurani ndiyo huwa kigezo, kile kinachoafikiana na Qurani hakipingwi, kinachokinzana nacho hukataliwa, na kile ambacho Qurani haijakithibitisha wala kukikana hakijengwi juu yake aqida( imani)
Katika kisa cha Watoto wa Adamu Qurani inasema Sadaka ya nani haikukubaliwa? Sadaka ya nani ilikubaliwa? Nani alimuua mwingine? Nani aliuliwa na mwingine?
 
quran na kitabu kitakatifu cha Biblia vinanikumbusha kitabu kama Physics mtunzi A.F.Abbott halafu unakuta kuna kijipamphlet cha physics kina makosa kibao nacho kimekopiwa kwenye Abbott na aliyekopi anaita pamphlet lake kitabu kizuri sana cha fizikia na anataka watu wakipuuze kitabu cha Abbott na kusema kina makosa mengi na vingi vya uongo na so watu wafuate kijipamphlet chake.

​

 
Katika kisa cha Watoto wa Adamu Qurani inasema Sadaka ya nani haikukubaliwa? Sadaka ya nani ilikubaliwa? Nani alimuua mwingine? Nani aliuliwa na mwingine?
kile ambacho Qurani haijakithibitisha wala kukikana hakijengwi juu yake aqida( imani)


Huu mstari wa mwisho ulitosha kujibu ulichouliza ila sijajua kwa nini umeuliza tena
 
Ukisoma kitabu chenye makosa ukapata taarifa moja sahihi, je kitabu kizima kinakuwa sahihi?
Umejuaje kuwa ni sahihi wakati mtume wako kakikataa ? Maagizo ya mwisho ya Mungu ni injili kabla ya msahafu je kwa nini Muhammad hakufuata injili kabla ya kupewa utume na kwa hiyo ndiyo afikie daraja la utume ?
 
Sadaka ya nani haikukubaliwa?
Sadaka ya nani ilikubaliwa?
Nani alimuua mwingine?
Nani aliuliwa na mwingine?
Sadaka ya Haabil ilikubaliwa
Sadaka ya Qaabil haikukubaliwa

Qaabil alimuua Haabil
Haabil aliuliwa na Qaabil.
 
kile ambacho Qurani haijakithibitisha wala kukikana hakijengwi juu yake aqida( imani)


Huu mstari wa mwisho ulitosha kujibu ulichouliza ila sijajua kwa nini umeuliza tena
Watoto wa Adamu wana majina yao?

Waislamu mliyajuaje /mnayajuaje majina ya watoto wa Adamu?
 
Umejuaje watoto wa Adamu walikuwa wanaitwa Haabil na Qaabil?
Hayo majina yao Waislamu mliyapata au mnayapata wapi?
Ukiisoma kwenye tafsiri ya hizo aya kwenye Qur'an.

Imam Ibn Jarir Attwabari amepokea kutoka kwa Abdallah ibn Abbas kwamba: Qaabil alikuwa mkulima, na Haabil alikuwa mchungaji wa kondoo. Haabil akatoa kondoo bora, Qaabil akatoa mazao mabaya, ndipo sadaka ya Habil ikakubaliwa na ya Qaabil ikakataliwa.

Ibn Abbas ni swahaba wa Mtume.
Imam Attwabari ni mfasiri wa Qur'an.
 
Abdallah Ibn Abbas swahaba wa mtume aliyajuaje majina ya watoto wa Adamu?
 
Ufahamu pia Bw. Yoda

Baada ya Haabil kuuawa ndipo Mungu akampatia Adam mtoto anayeitwa Sheeth.

Sheeth alikuwa ni mtoto ambaye alikuwa ni wa tofauti. Yeye ndiye binadamu wa kwanza kutokwa na ndevu, na ndiye mtoto aliyepokea kijiti cha Utume kutoka kwa Nabii Adam alayhi ssalaam.

Na ndiye binadamu wa kwanza kuunda jeshi na kupigana na upande mwengine: Qaabil alikimbia na Dada yake ambaye alikatazwa kumuoa kwa amri ya Mungu kwa nyakati hizo baada ya kumuua nduguye.

Akazaa naye na kizazi kikawa kikubwa. Kufupisha maelezo; hawa ndiyo watu ambao Nabii Sheeth alipambana nao baadaye kwa kusimamisha vita nao.
 
Abdallah Ibn Abbas swahaba wa mtume aliyajuaje majina ya watoto wa Adamu?
Qur'an inatafsiriwa kwa namna tatu.
1) Qur'an bi Qur'an
2) Qur'an bi Sunna
3) Qur'an bi swahaba

Mapokeo mengine wanayapokea kutoka kwa Maswahaba ambao wao walitafsiriwa na Mtume au kufafanuliwa na Mtume maana ya aya. Hiyo, ndiyo tafsiri ya Qur'an kutoka kwa swahaba.

Hivyo, Ibn Abbas ndivyo alivyonukuu kama alivyopooea naye.
 
Sasa utajuaje nani alimuua mwenzake??
Muhimu ni kujua kuna mmoja alimuua mwenzie na ni yule ambaye haikupokelewa sadaka yake kama inavyoelezwa kutokujua majina yao hakipunguzi chochote na kama kipo kinachopungua kitaje
 
Muhimu ni kujua kuna mmoja alimuua mwenzie na ni yule ambaye haikupokelewa sadaka yake kama inavyoelezwa kutokujua majina yao hakipunguzi chochote na kama kipo kinachopungua kitaje
Majina yao nyie Waislamu mliyajuaje?
 
Mtume Muhammad alikuwa anatoa wahayi mwingine nje ya Quran kupitia hadithi?
 
Watoto wa Adamu wana majina yao?

Waislamu mliyajuaje /mnayajuaje majina ya watoto wa Adamu?
Urudie huo mstari wa ufahamu, nimejibu kama msomaji wa vitabu na sio mwislamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…