Kinachotushangaza ni kwamba wanakimbilia kwa walewale wanaowaita makafiri na hawataki kabisa kwenda kwenye nchi yoyote ya kiislamu kwa sababu wamechoka kuendeleza utamaduni wa kiarabu wanaoona haufai katu katika dunia ya kisasa.
Katika nchi za kiarabu na hizo zinazojiita za kiislam watu kulazimishwa kuswali kitu ambacho binadamu wa kileo hapendi.
Mabinti hulazimishwa kulinda ubikra hadi siku ya kuolewa na wengi leo wanashindwa na kulazimika kufanya ngono kinyume cha maumbile ili tu kulinda ubikra maanake akishindwa kulinda ubikra na kugundulika siku ya kuolewa kwamba sio bikira basi uwezekano mkubwa ni kuuwawa kwa madai kwamba amemdhalilisha familia.
Sasa mambo ya kipumbavu kama hayo hufanya waarabu wengi kuamua kuzamia katika nchi za magharibi ambapo wengi wa hao wazamiaji waliokimbia nchi zao huamua kuachana na imani za kidini na kuishi kivyao wakiwa huko ughaibuni.