Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Kwa mujibu wa AG kwa sasa hata uthibitisho wa kujouzulu wa makamo hauhitajiki kufuatia kuvuliwa uanachama
Hivi kuna sehemu yeyote kwenye KATIBA imetamkwa Barua ya VP kujiuzulu ipelekwe kwa nani?

Na kwanini Rais aridhie kujiuzulu kwa mtu ambaye alipigiwa kura kama mate na sio kwa teuzi ya barua?
 
Ugumu wa kumpeleka Nchimbi mahakamani ni kwamba atakuwa anajua mambo mengi sana ambayo yanaweza kutoka katika cross examination.

Tayari wana kesi mbaya ya Lissu, wakiiongezea hii itawapa tabu sana.

Sasa hivi wapo katika hali ngumu sana kwa sababu hawawezi kumficha daima, na hawataki kumuachia.

Na kwa kumfukuza uanachama, ukiondoa suala la uhai wake na hayo mafao yao, hana cha kupoteza. Na Nchimbi ni mbishi tangu zamani hatakaa kimya. Na amepata support kubwa sana kitoka kwa watu wengibsana wanaoona anaweza kuwasaidia kuweka wazi madudi mengi aliyoyaona ndani ya CCM.

I was kind of disappointed kuona amejiuzulu kirahisi, lakini nikaanza kufikiri kama ulivyouliza, hivi tunajuaje hata kama amejiuzulu kweli?

Ikiwa Tanzania watu huwa wanateuliwa bila kukubali kwa kusikia redioni tu, kwa nini wasiweze "kujiuzulu" kwa kusikia redioni tu hivyo hivyo?

Angalau wamuachie tumsikie akubali mwenyewe kajiuzulu, sasa hivi hata kama habari aliyoitoa Jasusi Chahali kwamba ile barua hajaandika Nchimbi si kweli, ni vigumu kumbishia Chahali ikiwa Nchimbi mwenyewe hajulikani alipo na hata simu za watu hajibu.

Ngoja nitafute networks za watoto wa Oysterbay Primary maana wale wana za ndani za familia kabisa. Naona walikuwa wananitafuta hapa ila nilikuwa busy.
 
Kuna kitu hakipo sawa
 
Umeandika nini? Kwamba ndugu za makamu wa rais wajitokeze kudai ametekwa? Huwa una matatizo ya akili.
 
Katika threads zako za hivi karibuni unaonesha kupanic sana ...nakushauri uwe na utulivu ili ujadili hoja.
kwa kifupi niseme hakuna thread inayomhusu JPM humu jamvini sijaisoma sikumbuki kuona thread yako baada ta kisa cha Mtwara
Kwanini usi search..usiamini sana ubongo wako.
 
Kwani huwezi kuwa at gun point unaambiwa jibu hivi jibu vile wakisha jiridhish unapokonywa simu zote na vifaa vingine?
 
Mkuu, mbona Warioba hakumumunya maneno, lakini wewe anonymous unaumauma maneno why?

Warioba alisema wazi kuwa Nchimbi alinyang'anywa simu na kuwekwa kizuizini.
Jambo lililo wazi namna hiyo linahitaji mjadala na maswali swali?
 
Yawezekana wakati anapokea simubya mzee Warioba alikuwa chini ya ulinzi na alilaximishwa kukubali kuwa kajiuzulu.
 
Tunasubiri siku ya kukabidhi ofisi au huyu wa sasa hakabidhiwi anaingiabtu kimy kimya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…